Mkuchika: Walimu waliokimbia na fedha za serikali wazirudishe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuchika: Walimu waliokimbia na fedha za serikali wazirudishe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mtweve, Apr 29, 2011.

 1. mtweve

  mtweve Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa na tawala za mikoa,kapten George mukuchka amewataka walimu walio chukua fedha za kujikimu na mishahara na kisha kukimbia nayo walirudishe kabla ya hatua kali kuchukuliwa. Hii ni mara ya kwaza walimu kudaiwa na serikali badala ya serikali kudaiwa na walimu
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nawaunga mkono walimu..........
   
 3. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri kila halmashauri isomeshe walimu wake ambao watakuwa tayari kufanya kazi katika halimashauri husika. Walimu watarajiwa waombe kupitia halimashauri ili kuweza kupata walimu wanayoyafahamu mazingira wanayotarajia kufanyia kazi. Mtu amekulia Dar leo unampeleka Ishinabulandi, inahitaji saikolojia ya hali ya juu kumshawishi akae huko lasivyo atakimbia tu.

  Naomba kutoa hoja.
   
 4. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hao walimu wacha wakimbie tu huko wanakopelekwa hakuna NYUMBA za kukaa wakakae juu ya miti!!? Wanatumia wiki nzima kufuatilia mishahara wilayani. Wanatumia nusu ya mshahara kama nauli kufuatilia salary wilayani .hapo bado chakula hadi maji ya kununua! Usafiri nao kasheshe. Kabla ya kutoa vitisho watatue matatizo hayo.la sivyo watoto wa walalahoi watazidi kudidimia kielimu
   
 5. Mvuni

  Mvuni JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huyu mkuchika anafikili kweli?? Nadhani ni mvivu wa kufikiri huyu jamaa. sasa anadai walimu hivyo vijisenti, kwaani lazima kuendelea kufanya kazi hata kama mazingira ya kazi hayaridhishi? Alipaswa kujiuliza kwanini walimuu wake wameacha kazi ili aweze tatua tatizo lililopo. Hajui kuwa globalization allows job mobility? Askari wa jk wavivu wa kufikiri...
   
 6. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  hilo nalo neno
   
 7. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Badala ya Waziri kutafuta Sababu za Walimu kukimbia ang'ang'ania Fedha Kurudishwa....Na wale wanaoripoti na Kutopewa Mafao yao waziri atawalipa Fidia?
   
 8. O

  Olecranon JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,371
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Ingawaje siungi mkono watu kukimbia na pesa za serikali, bado ninapenda kujua hawa waalimu kama wamekimbia na mabilioni zaidi ya yaliyochotwa kule BOT na ndio maana huyu Mkuchika amesimama kidete kutaka wazirudishe wakati hazungumzi kabisa kuhusu mafisadi papa.
   
 9. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Hawa waalimu wajifiche kwa makini kwa maana serikali iliyoshindwa kupambana na mafisadi inaweza kujitafutia ujiko kupitia kwao.
  Usishangae wakabambikizwa hata kesi za EPA kisha tukaambiwa wao ndio mafisadi papa tuliokuwa tunawatafuta.
   
 10. mtweve

  mtweve Member

  #10
  Apr 29, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Pesa ambayo wamekimbia nayo haizidi milioni,mimi mwenyewe mwl,nakumbkua wakati naajiliwa nilipewa elfu thelathini kwa siku saba na kilicho ongezeka kwa sasa ni vijisenti vya mizigo na mshahara wa mwezi wa kwanza ambao haizid laki nne
   
Loading...