Mkuchika na Mhagama hivi hii hali inayoendelea kwa watumishi wa umma nyie mnaiona sawa?

digodigo

Senior Member
Dec 2, 2010
178
225
Mimi ningependa kuuliza kwa Wah. Mawaziri Mkuchika na Mhagama hivi hii hali inayoendelea kwa watumishi wa umma nyie mnaiona sawa? Iwapo juhudi za mheshimiwa Rais zinaonekana mbona zenu hatuzioni? sisemi mengi kwa Mh Jafo kila mtu anaona matunda.

Nashangaa sasa yapata miaka minne wafanyakazi utafikiri mligombana nao. Wengi kila kukicha ni vilio mioyoni mwao hakuna kupanda madaraja, vyeo, watu wanakaimu zaidi ya 4 years what a pity?

Mtu anastaafu kwa cheo ambacho hakustahili hata ILO sidhani kama wanasapport hili, mimi sioni kama haki inatendeka sijui wenzangu wanalionaje hili.

Nyie kutwa mnazunguka nchi nzima lakini hatuoni mabadiliko Ma HROwa wizara mbalimbali mbona muda mrefu tu washawasilisha status za wafanyakazi hivi hazifiki au hamuzioni?

Wizara ya maji, afya, kazi na nyinginezo kuna watumishi kibao wana kilio hiki. Basi ni bora likawekwa wazi suala hili kulikokuishi kwa mategemeo ya ahadi zisizotekelezeka.
 

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
4,665
2,000
Kipindi hiki performance ya watumishi siyo kipaumbele, wao wanapata huduma first class na kama haipo hapa nchini wanaenda ng'ambo. Kuna shule wanalipia watoto wao ada hadi million 5, nenda kaangalie hali kwenye hizo shule wanazoita za kata, eti elimu bure
 

Grahams

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
1,540
2,000
Kuna watu watashauri hapa kwamba watumishi wajiongeze kwenye kufanya ujasiriamali. Lakini kilichowakuta watumishi wa kusini huku walioamua kujiongeza kwenye biashara ya korosho ni kuitwa Makangomba baada ya kuingia benki kukopa na kufanya biashara.
 

Mponda 02

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
509
500
Umeeleza jambo la maana sana. Lakini kwa hao viongozi sidhani kama wana uchungu na hili, maana aliyeshiba hamjui mwenye njaa!
Wao wameshiba na matumbo yao yamejaa ndio maana ni miaka minne sasa wapo kimya!

Wale wote wanaliokandamiza haki za wengine kwasababu tu wao ni viongozi, waelewe kuna maisha baada uongozi wao.
Uwe Rais, Waziri Mbunge au nani, tambua cheo chako kwa Mungu hakipo.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
5,521
2,000
Mtoa mada usisahau sababu mojawapo inayolifanya bara la Afrika kuendelea kuwa maskini ni kutokana na aina ya viongozi tulio nao! Kiufupi tu wamejawa na ubinafsi na roho ya kwa nini!
 

mopee9

Member
Jul 24, 2019
32
125
Mtoa mada usisahau sababu mojawapo inayolifanya bara la Afrika kuendelea kuwa maskini ni kutokana na aina ya viongozi tulio nao! Kiufupi tu wamejawa na ubinafsi na roho ya kwa nini!
Hata kusoma mwenyewe ukienda na kujilipia ukirudi ndo waanze kuhesabu upo kazini baada ya miaka 5 ndo wafikirie kukupandisha cheo .tafakari chukuwa hatua!
 

Diason David

Verified Member
Aug 2, 2018
7,567
1,995
Wewe sio mzalendo kabisa wa jiwe kweli kweli wanakuambia mshahara wanaolipwa unatosha mpaka wa michepuko yao mkuu usiwe na hofu juu yao we komaa na maisha yako we wangalie uwapotezee wapo right track mbele kwa mbele
 

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
19,182
2,000
Wanabana hivyo na ajira pia ila kesho kutwa ajira zitamwagwa na watumishi kupandishwa vyeo na madaraja alafu akiomba tena kura mumpe kwa furaha ya vyeo mlivyopewa
 

steveachi

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
6,855
2,000
Wanaoogopwa ni wanajeshi tu mkuu ktk nchi zenye dalili za tawala za kidikteta,wao kila mwaka mwake tu,ongezeko la salary ni lazima kwani wasipoongezewa watawala wanaogopa watakinukisha kwani wataungana na wananchi kuangusha tawala zao.

Hao ndio wafanyakazi wanaothaminiwa na Tawala za kidikteta,wafanyakazi wa kada zingine wengine wote ni wasindikizaji tu na hawana umuhimu wowote kwao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom