GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,277
- 6,673
Ili kuwasaidia wakulima (Kama ni kweli) Serikali ilianzisha mfumo
Wa uuzwaji wa mazao unaojulikana kama Stakabadhi ghalani. Ni
Mfumo maarufu ambao Chama cha ushirika kupitia kwa vyama
Vya msingi vya ushirika hukusanya mazao ya wakulima na kuyapeleka
Ghala kuu ambako huuzwa kwa mnada.
Tatizo lililopo ni kwamba mnada huo umekuwa ukiendeshwa kwa
Siri bila mkulima kufahamu mazao yake yamenunuliwa kwa bei gani
(Hapa nakusudia zaidi zao la korosho) Mwisho wa yote mkulima
Huambulia Tsh 800 mpaka 1000 tena siyo taslimu hulipwa kwa awamu
Tatu bila kuambiwa korosho zake zimenunuliwa kwa bei gani.
Baadhi ya wakulima wakaamua kuanzisha umoja wao wa wakulima wa
Korosho ili waweze kuuza wenyewe kwa mfumo huo huo ambao serikali
Inautaka. Umoja huo ukasajiliwa kwa Cert. no. S.A 16671. Umoja ukaanza
Kazi.
Jambo la kwanza lililofanywa na umoja huu ni kufichua bei ya zao hilo
Huko ghalani ambayo ilibainika wazi kuwa ni kubwa ukilinganisha na
Malipo yaliyokuwa yanamfikia mkulima. Kwa mara ya kwanza Mkulima
Ambaye ameuza kupitia umoja huo akalipwa pesa taslim Tsh. 1,800
Hapo ndipo miksukosuko ilipoanza. Serikali kama kawaida yake ikaanza
Kutumia mabavu kuuzuia umoja huu kufanya kazi hiyo. Baada ya
malumbano ya muda mrefu hatimaye umoja huo ukaruhusiwa kuuza
korosho zilizosalia.
Jambo la kushtusha ni barua ya hivi karibuni kutoka TAMISEMI ambayo
Inauzuia umoja huo kukusanya na kuuza korosho za wakulima wake.
Huu ni uonevu wa wazi ambao unanifanya mimi na wengine kuamini
Kuwa mkuchika na wote waliokuwa wanatajwa kunufaika na uuzwaji
Wa korosho kuwa Tuhuma hizo ni za kweli. Kwanini huu umoja unaandamwa
Kiasi hiki? Ni wazi kuwa serikali haina nia ya dhati ya kumtaka mkulima
Awe na maendeleo ya kweli.
Mkuchika tunaomba ujirekebishe, una tuhuma za mradi wa NDF, tunajua
Kuwa unapata fedha nyingi kutoka kwa wahisani kwa ajili ya maendeleo
Ya shule za sekondari zilizo chini ya NDF (Newala Development Foundation)
Tunajua kuwa fedha nyingi zinaingia mfukoni mwako. Hatutaki kukuumbua zaidi
Tunachotaka utuachie korosho zetu tufanye tunavyotaka la sivyo tutaanika
Uozo wako wote mpaka huko kwa wahisani wako.