Mkuchika kama waziri hakumsaidia Rais, inafaa awajibishwe. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuchika kama waziri hakumsaidia Rais, inafaa awajibishwe.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bulesi, May 1, 2012.

 1. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ripoti ya bunge ya serikali za mitaa imeonesha udhaifu mkubwa sana katika matumizi ya fedha na rasilimali nyingine zinazokadhiwa halmashauri. Mkuchika kama waziri alitakiwa achukue hatua stahiki pale ambapo mapungufu katika halmashauri hasa kuhusiana na matumizi mabaya ya fedha lakini hakufanya hivyo!!Hata pale ambapo hakuwa na mamlaka ya kuwaondoa wakuu wa wilaya waliodhihilika kuwa sio waadilifu hakuna hatua za kinidhamu zilizochukuliwa ingawa kulikuwepo na ushahidi tosha kuhusu tuhuma dhidi ya wakuu wa wilaya husika. Sisi hapa wilaya ya Hai mkoa wa kilimanjaro, mkuu wa wilaya amefisadi michango yetu ya kujenga shule za sekondari za Boma-Ng'ombe na Harambee na pia amehusika na kujitwalia ardhi wananchi ya mashmba kiujanja ujanja huko Mlima Shaba na kijijini Kamaya! Si hivyo tu kwa kumtumia afisa ardhi aitwae Mwarabu amekuwa akijitwalia ardhi kwa kutumia majina bandia ; yote haya yanafahamika kwa vyombo husika hasa kamati ya ulinzi na usalama na inasemekena vyombo vya juu husiska vina taarifa hizi lakini hatua stahiki hazikichukuliwa. Jinsi mambo yanavyoendeshwa hakuna jinsi watu wanaweza kuipenda serikali hii na chama tawala . Hatua stahiki zinafaa zichukuliwe haraka!!
   
Loading...