Mkuchika anaweza kutuvuruga kama Mungai halafu huyo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkuchika anaweza kutuvuruga kama Mungai halafu huyo!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Magobe T, May 27, 2010.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Hivi karibuni kumekuwa na mjadala kuhusu kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia kuanzia elimu ya msingi na ikiwezekana hata chuo kikuu. Ni muhimu kutumia lugha yetu ya taifa siyo kwa sababu ya kuiga mataifa mengine ila kwa sababu Kiswahili ni lugha yetu na tunapenda tuiendeleze zaidi na zaidi.

  Ingawa baadhi ya wachangiaji wa hoja hii wamekuwa wakisema kuongea au kutumia Kiswahili ni muhimu, mimi nasema Watanzania wanaoweza kuongea au kutumia Kiswahili na lugha nyingine kama Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa, Kichina nk wako katika nafanzi nzuri zaidi kuliko wale wanaongea au tumia Kiswahili tu. Chukulia kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inakua. Zamani zilikuwa nchi 3 tu na sasa hivi ni 5 na hata Sudani na DRC wanataka kujiunga. Hii inaonesha kutumia lugha nyingi zaidi kuna faidi zaidi na hasa katika dunia yetu hii iliyojaa ushindani.

  Kitu cha kushangaza ni kwamba badala ya waziri George Mkuchika kuwashauri Watanzania wajiendeleze zaidi katika lugha mbalimbali yeye anaonekana kusema "kila kitu kiwe katika Kiswahili". Anaonekana akitumia nguvu nyingi katika hili. Lakini lugha zote ambazo zinatumiwa na watu huwa hazilazimishwi ila zinatokana na mahitaji ya jamii. Kama jamii inaona inahitaji Kiingereza, Kifaransa au Kijerumani hata Mkuchika afanyeje hataweza kuwalazimisha watu wasizitumie hizo lugha kwa kuwasiliana. Walau hataweza kwangu labda aingie kichwani mwangu.

  Ukienda Uingereza ni kweli utakuta watu wa kule wanaongea Kiingereza, ambayo ni lugha yao. Lakini nina mifano, ambayo hata Kiswahili kilikuwa kinatumika kwenye mikutano kwa wale waliokuwa wanataka kukitumia na hakuna mtu aliyekataza au kuweka sheria kuwa mtu akiwa Uingereza lazima atumie Kiingereza tu. Nafikiria kama Mkuchika angekuwa mkuu fulani huko Uingereza angelazimisha watu watumie Kiingereza tu. Pia katika chuo nilichokuwa ninasoma tulikuwa tunaombwa kwa wale wanaoweza kufundisha Kiswahili wafanye hivyo kwa malipo ya paundi 5 kwa saa na tulikuwa tunaruhusiwa kufanya kazi masaa 3 kwa siku.

  Sasa nirudi hapa Tz. Mkuchika anasema wale wanaoenda kufanya usaili kwa vile baadhi ya wanaosaili wanatumia lugha ya Kiingereza wasailiwa wengine wanashindwa kujieleza na hivyo kukosa kazi. Hapa anaonesha ana huruma kwa wale wanaokosa kazi kwa kutoelewa Kiingereza. Je, hana huruma kwa waajiriwa ambao watatumwa nje ya nchi kwenda kujifunza utaalamu fulani na kama wakienda tutaaminije kama wataelewa lugha za huko wanakoenda? Je, kwa hawa hana huruma?

  Binafsi nadhani kama tunataka kukiendeleza Kiiswahili cha kufanya ni kutunga vitabu vingi vizuri katika lugha ya Kiswahili, tuwe na Kamusi nzuri za Kiswahili na siyo hizi tulizonazo kw sasa maana hazina kitu, tuwe na methali, nahau na semi nyingi tu kwa Kiswahili. Hali hii itafanya watu wengi wapende kujifunza maneno au misemo mipya na kuonekana wanajua zaidi. Na ikiwezekana Mkuchika mwenyewe atunge vitabu vingi kwa lugha ya Kiswahili. Hapo ndipo tutakapoona anataka watu wajifunze na kukitumia Kiswahili na siyo kwa maneno matupu kama anavyofanya!

  Kwa kasi aliyonayo si asipopata tena uwaziri mwakani ndiyo kusema 'mbio zake za sakafuni zitakuwa zimeishia ukingoni' kama vile Mungai alivyoanguka chali na hasikiki tena licha ya kutuharibia mfumo wetu wa elimu? Tusipoangalia hata huyu Mkuchika atafanya hivyo. Atatuvuruga na kisha huyo, hatasikika tena na sisi tutabaki kwenye mataa. Watanzania tuwe macho na watu wanaotaka kuvuruga elimu yetu kwa kutuchanganya: mara hiki mara kile... Hatutaki!

  Tujifunze na kukitumia Kiswahili vizuri na pia tuendelee kutumia lugha zingine tulikowekeza. Ni juu yetu kuchagua lugha tunayopenda kuitumia kwa mawasiliano kwa wakati huo na siyo eti waziri ndiye atuchagulie/atulazimishe tutumie lugha gani. Lowassa alikuwa naye amevalia njuga 'mvua ya miujiza' - kama angebaki waziri mkuu sasa hivi tungekuwa tunatumia mihela mingi kununulia kemikali za hiyo mvua yake na kuwafanya watoto wakose kwenda shule na wagonjwa wakose matibabu kwa vile kungekuwa na bajeti ya hiyo mvua. Na kwa vile hata rais Kikwete amesema kwa wafanyakazi kulipwa kima cha chini 350/- haiwezekani hivi, Lowassa angekuwa bado waziri mkuu isingepatikana mihela kwa ajili ya kununulia kemikali kila mwezi au kila mwaka ili kutengeneza mvua? Sijui nayo ingekuwa na masika na kiangazi...
   
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Watanzania kwa ujumla hawana udhaifu wa msingi katika lugha ya kiswahili. Wana udhaifu tena mkubwa katika lugha nyingine za kimataifa. Huko ndiko kunakotakiwa mkazo, tena mkubwa, kwa vile mawasiliano ya leo hayajali mipaka.
   
 3. beth

  beth JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2017
  Joined: Aug 19, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 981
  Trophy Points: 180
  Ndugu George Mkuchika.. Kiongozi mwenye maamuzi tata na haiba ya jazba...

  Leo Rais Magufuli ameona ni vyema Mkuchika akarudi kuiongoza Wizara ya Utumishi na Utawala Bora. Analenga matokeo gani kwa mwenendo wa nchi?!

  Muda utaamua!
   
Loading...