Mkosamali (MB) kuhamia CHADEMA

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
KUNA kila dalili ya kufanyika kwa uchaguzi mwingine mdogo kwa upande wa Tanzania Bara, baada ya mbunge wa NCCR-Mageuzi Jimbo la Mhambwe, Felix Mkosamali kuanza mazungumzo na Chadema kwa lengo la kutaka kuhama chake cha sasa.

Tayari taifa lilishuhudia uchaguzi mdogo wa Igunga uliofanyika Oktoba mbili kujaza nafasi ya Rostam Aziz aliyejiuzu nyadhifa zote ndani ya CCM ikiwamo na ubunge kwa madai kuwa chama chake kinaendesha siasa za uchwara.

Wakati uchaguzi huo wa Igunga ukitajwa kutumia rasilimali nyingi za vyama vya siasa ikiwamo mabilioni ya fedha, Mkosamali ambaye ni mbunge kijana wa NCCR-Mageuzi anatajwa kufanya mazungumzo na Chadema na huenda akatangaza kujiuzulu wadhifa huo na unachama wa chama chake cha sasa wakati wowote.

Kwa mujibu wa washirika wa karibu wa Mkosamali, uamuzi huo unatokana na kile kinachoelezwa ni msuguano wake wa chini kwa chini na mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Washirika hao wa karibu wa Mkosamali, walifafanua kwamba msuguano huo umemfanya mbunge huyo kufikiria uamuzi huo wa kuhama chama chake na kujiunga Chadema ambako anaamini anaweza kutimiza malengo yake kisiasa.

Hata hivyo, alipoulizwa mwenyewe kwa njia ya simu, alijibu kwa kifupi, "Kaka una haraka gani? Si unisubiri kesho (leo) unipigie? Kesho nitakwambia kila kitu. Kwanza nani kakupa hizi taarifa,? Aliuliza Mkosamali

Naye rafiki yake wa karibu Metusela Mawazo aliiambia Mwananchi kwamba naye amesikia taarifa za Mkosamali kutaka kuhamia Chadema kutokana na hali inayoendelea ndani ya NCCR-Mageuzi.

"Kimsingi nimezipata taarifa za Mkosamali kuanza harakati za kuhamia Chadema, zimenistusha sana. Ni taarifa za kweli na kama unavyojua mwananchi yoyote anaweza kuhamia chama anachokitaka," alisema Mawazo.

Alisema kwa jinsi anavyomjua Mkosamali kimsimamo hayuko tayari kufanya kazi akiwa NCCR-Mageuzi. "Ni rafiki yangu wa karibu sana, hayuko tayari kufanya kazi akiwa NCCR-Mageuzi, ni mpambanaji na nina uhakika atashinda uchaguzi mdogo," alisema Mawazo ambaye aligombea ubunge kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi Jimbo la Buyungu Kibondo na kuchuana vikali na mgombea wa CCM, Christopher Chiza.
Mbatia akana msuguano

Hata hivyo, Mbatia alipoulizwa kuhusu hilo, alistuka huku akisema, ''Mimi sina msuguano na Mkosamali kwani hata juzi tulikuwa naye kwenye kikao. Tulifanya nae kikao na tukazungumza vizuri tu, hilo la msuguano ndiyo nasilikia kwako".


Mbatia alisema mwisho jana, aliwasiliana na Mkosamali ambaye alimtumia ujumbe mfupi wa simu akimwomba mwenyekiti huyo afuatilie vema kuhusu kesi yake ya jimbo la Mhambwe na kutaka chama kilijadili vema.

"Sasa nashangaa unavyoniambia anataka kuhama au nina msuguano nae. Leo (jana) alinitumia ujumbe mfupi kuhusu kesi ya uchaguzi jimbo lake la Mhambwe. Alitaka chama kijadili vema hilo na nikamwambia sawa," alisema Mbatia.


Hata hivyo, vyanzo zaidi vilivyo karibu na Mkosamali vilidokeza jana usiku kwamba Mbatia ameomba kukutana na mbunge huyo leo kwa ajili ya kujadili zaidi suala hilo ambalo linaweza kuwa pigo kuu kisiasa kwa NCCR-Mageuzi.

NCCR-Mageuzi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kilipata viti vinne vya majimbo ambavyo ni Kigoma Kusini kwa David Kafulila, Mhambwe kwa Mkosamali, Kasulu Vijini Zaitun Buyogela na Kasulu Mjini kwa Moses Machali.

::Mwananchi::
 
Daaa kila Mtu ana akili zake lkn ni vyeema Mtu ukakaaa mahala ambapo utapata aman ya Moyo wako na ukafanya kazi vile ulivojaaliwa.Ushauri atulie na kuyamaliza na Mwenyekiti wake ikishindikana kabisa basi ndio afanye Uamuzi huo
 
Daaa kila Mtu ana akili zake lkn ni vyeema Mtu ukakaaa mahala ambapo utapata aman ya Moyo wako na ukafanya kazi vile ulivojaaliwa.Ushauri atulie na kuyamaliza na Mwenyekiti wake ikishindikana kabisa basi ndio afanye Uamuzi huo
Inawezekana imefikia kwenye hatua ya kushindikana kabisa.
 
Siasa za Mbatia hazielewekielewki vile! Yaani yupoyupo tu. Ondoka kijana hamia kwa wapambanaji wa ukweli.
 
Hizi chaguzi ndogo gharama zake tunalipia sisi wananchi.....sio fair kuwa kila mbunge akijiskia kuhama chama wananchi tugharimike
 
mambo ya siasa, waachie wanasiasa!'""""" Mbatia sio mwanasiasa, chama amekiua..... alaf, huyu ndie aliemfanyia fitina Mrema akatoka kwenda NCCR??????
 
Chadema kuweni makini na watu kama kina Mkosamali. Asije akawa kama Shibuda.
 
Hizi chaguzi ndogo gharama zake tunalipia sisi wananchi.....sio fair kuwa kila mbunge akijiskia kuhama chama wananchi tugharimike

unalipia bei gani mkuu? Ufanyike usifanyike wewe kama wewe unapata nini? Hao waliotumia bilioni 3 igunga wasingetumia wangekugawia ya mboga nyumbani?
 
Huyu kijana alikuwa Chadema kabla ya kuhamia NCCR-Mageuzi muda mfupi baada ya Kafulila kuhamia huko, sasa inaonekana amegundua kulehakumfai ndiyo maana anataka kuhama. Anyway ana haki ya kufanya hivyo na uchaguzi mdogo ukifanyika tusiogope gharama kwa demokrasia ni gharama. Lakini pia hilo ni tatiz la kikatiba kuzuia wagombea huru
 
Haya mambo ya chaguzi ndogo yanatuingiza katika gharama kubwa sana. Kwa nini asisubiri hadi 2015?
 
Naomba kueleweshwa, Kuna kipindi nilisikia Juu ya vijana wawili kukihama CHADEMA baada ya kutofautiana..
Kumbukumbu zinaniambia kuwa walihamia NCCR na kuna aliyeukwaa Ubunge,
Hivi huyu Jamaa hakuwa miongoni mwa hao vijana kweli?
Kama ndiye, je ana uhakika ataweza kuyala matapishi yake mwenyewe?
 
Naomba kueleweshwa, Kuna kipindi nilisikia Juu ya vijana wawili kukihama CHADEMA baada ya kutofautiana..
Kumbukumbu zinaniambia kuwa walihamia NCCR na kuna aliyeukwaa Ubunge,
Hivi huyu Jamaa hakuwa miongoni mwa hao vijana kweli?
Kama ndiye, je ana uhakika ataweza kuyala matapishi yake mwenyewe?
kafulila
 
nadhani ana kila sababu ya kutulia mpaka uchaguzi wa 2015 iwapo tu hiyo kesi inayotajwa haitamwondoa katika ubunge wake. kama kesi hiyo nayo tungejulishwa, nadhani angepewa ushauri mzuri na wa kufaa zaidi.
 
Naomba kueleweshwa, Kuna kipindi nilisikia Juu ya vijana wawili kukihama CHADEMA baada ya kutofautiana..
Kumbukumbu zinaniambia kuwa walihamia NCCR na kuna aliyeukwaa Ubunge,
Hivi huyu Jamaa hakuwa miongoni mwa hao vijana kweli?
Kama ndiye, je ana uhakika ataweza kuyala matapishi yake mwenyewe?

aliyahama CDM ni David Kafulila wa kigoma kusini, na alipata ubunge kupitia NCCR-Mageuzi
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom