Mkosamali ashikiliwa na Polisi kwa kufunga kituo cha kuandikisha wapiga kura

Stanley.

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
660
298
Mh. Mbunge wa Muhambwe (Nccr) Felix Mkosamali anashikiliwa na Polisi kwa madai kuwa majira ya saa 10 leo alifunga kituo cha kuandikisha wapiga kura na kurejesha vitabu kwa Mkurugenzi.
========================
Mkosamali atiwa mbaroni Kigoma

KWA UFUPI
Akizungumza kwa simu akiwa katika Kituo cha Polisi Kibondo jana, Mkosamali alisema aliamua kuchukua hatua hiyo kutokana na wasimamizi kukataa kuwaandikisha wananchi ambao si wanachama wa CCM.

Kibondo. Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kuchukua madodoso ya kuandikisha wakazi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Taarifa zilizopatika jana usiku wakati tukienda mitamboni na kuthibitishwa na Mkosamali na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamoto zilidai kuwa mbunge huyo alichukua madodoso hayo katika Kijiji cha Kumuhasha, Kata ya Murungu.

Akizungumza kwa simu akiwa katika Kituo cha Polisi Kibondo jana, Mkosamali alisema aliamua kuchukua hatua hiyo kutokana na wasimamizi kukataa kuwaandikisha wananchi ambao si wanachama wa CCM.

"Ni kweli ninashikiliwa polisi kutokana na kuchukua madodoso baada ya kuona mkurugenzi hataki kuwaandikisha watu ambao siyo wanaCCM," alisema Mkosamali.

Naye Mwamoto alisema mbunge huyo alifanya fujo kwa kuwa hoja zake hazina mashiko. Alisema Mkosamali alichukua madodoso ambayo baadaye aliyawasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibondo.

CHANZO: Mwananchi (25/11/2014)
 
​kwani kituo hakina walinzi???wakati anafanikisha yote hayo waandikishaji hawakutoa taarifa pahala husika???
 
mwambie aje kufunga hapa mwanza kwa kiwia maana greng gard wanawimbo wao mzuri sana wangemwimbia wakati akichukua vitabu hivyo
 
Duh hizo zote ni hasira za Escrow sipati picha hio jumatano itakuaje
 
Kituo kinapaswa kufungwa muda gani?

Na ni nani mwenye dhamana ya uandikishaji pamoja na ufungwaji vituo?
 
BREAKING NEWS!!!!!!!!!!!!!!''

Mh Felix Mkosamali mbunge wa Muhambwe wilayani Kibondo mkoani Kigoma anashikiliwa na polisi na kulala lockup,akiongea na mwandishi wa habari hii,katibu wa mbunge ambaye pia ni katibu wa CUF ndugu Vedasto Pesa Mbili, amesema chanzo cha mh Mkosamali ni kupishana maneno na mkurugenzi mtendaji wa wilaya ambaye pia ndo msimamizi mkuu wa uchaguzi serikali za mitaa,inadaiwa mh Mkosamali alikwenda kuhoji ni kwa nini wakazi wa kitongoji cha Nduta wanazuiwa kuandikishwa kwenye zoezi linaloendelea sasa,ndipo ambapo kukatokea kutokuelewana kati yao na mkurugenzi huyo kuita polisi waliomkamata mh Mkosamali.

kwa upande wake mkurugenzi wa walaya hiyo,amesema mh Mkosamali alivunja sheria ya uchaguzi kwa kitendo chake cha kwenda katika kituo cha uandikishaji katika kijiji cha Kumhasha katika kata ya Murungu wilayani hapa na kuamrisha kituo hicho kifungwe mara moja kwa madai kwamba kuna wananchi wa kijiji jirani cha Nduta wamezuiwa kuandikishwa,mkurugenzi huyo ameendelea kusema kwamba alichukua vitabu hivyo vya kuandikisha navyo na kuondoka navyo na kuvibwaga ofisini kwake,hali iliyomlazimu kumwita OCD na hatimaye mbunge huyo kukamatwa, Juhudi zinaendelea kumtafta OCD ili kupata maelezo zaidi,kwani alipotafutwa awali hakuweza kupatikana,Inadaiwa kwamba kitongoji hicho cha Nduta inadaiwa ni ngome nzito ya chama cha NCCR MAGEUZI ,Mkosamali ameendelea kushikiliwa mpaka sasa
 
Ukiona hivyo ujue ushindi umekaribia.

Katu siwezi mpatia pole. Kijana na mbunge mwenye umri mdogo kuliko wote bungenj, ila mwenye akili kubwa kuliko ma bunge yote ya maccm.

Nampongezi kukaa lock up. Hiyo ni ishara ya ushindi ni ushara ya maccm kuanguka.

Wanatumia nguvu ya dola na iman nayo hivi punde itaanguka.

Hongera Mkosamali pambana mpaka kieleweke viva UKAWA.
 
mwambie aje kufunga hapa mwanza kwa kiwia maana greng gard wanawimbo wao mzuri sana wangemwimbia wakati akichukua vitabu hivyo

Umehama matejoo leo uko mwanza?
Team buku saba bana mnajisahau same ID differ in users
 
Kila uchaguzi ni mizengwe tuu CCM watu wa ajabu sana. Hata usimamizi wa vyoo vya stand ungekuwa unafanywa kwa itikadi lazima ccm makao makuu wangetoa agizo "hakikisheni mnafanya kila muwezalo vyoo vyote tusimamie sisi"
 
Back
Top Bottom