Stanley.
JF-Expert Member
- Sep 6, 2011
- 660
- 298
Mh. Mbunge wa Muhambwe (Nccr) Felix Mkosamali anashikiliwa na Polisi kwa madai kuwa majira ya saa 10 leo alifunga kituo cha kuandikisha wapiga kura na kurejesha vitabu kwa Mkurugenzi.
========================
CHANZO: Mwananchi (25/11/2014)
========================
Mkosamali atiwa mbaroni Kigoma
KWA UFUPI
Akizungumza kwa simu akiwa katika Kituo cha Polisi Kibondo jana, Mkosamali alisema aliamua kuchukua hatua hiyo kutokana na wasimamizi kukataa kuwaandikisha wananchi ambao si wanachama wa CCM.
Kibondo. Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali amekamatwa na polisi kwa tuhuma za kuchukua madodoso ya kuandikisha wakazi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Taarifa zilizopatika jana usiku wakati tukienda mitamboni na kuthibitishwa na Mkosamali na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamoto zilidai kuwa mbunge huyo alichukua madodoso hayo katika Kijiji cha Kumuhasha, Kata ya Murungu.
Akizungumza kwa simu akiwa katika Kituo cha Polisi Kibondo jana, Mkosamali alisema aliamua kuchukua hatua hiyo kutokana na wasimamizi kukataa kuwaandikisha wananchi ambao si wanachama wa CCM.
"Ni kweli ninashikiliwa polisi kutokana na kuchukua madodoso baada ya kuona mkurugenzi hataki kuwaandikisha watu ambao siyo wanaCCM," alisema Mkosamali.
Naye Mwamoto alisema mbunge huyo alifanya fujo kwa kuwa hoja zake hazina mashiko. Alisema Mkosamali alichukua madodoso ambayo baadaye aliyawasilisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibondo.
CHANZO: Mwananchi (25/11/2014)