Mkopo wa Tsh 403,792,494,592 Hauna Manufaa Kwa Watanzania Masikini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkopo wa Tsh 403,792,494,592 Hauna Manufaa Kwa Watanzania Masikini.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MsemajiUkweli, Oct 31, 2012.

 1. MsemajiUkweli

  MsemajiUkweli JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 8,911
  Likes Received: 12,091
  Trophy Points: 280
  Ukweli husemwa:

  Mchumi Milton Friedman alisema, "There ain't no such thing as free lunch".

  Viongozi wetu kila kukicha ni kutembeza bakuli na kukopa. Deni la taifa kwa sasa ni Tsh 22,000,000,000,000. Hii mikopo inaisaidia nini jamii ukilinganisha kwa sasa kila Mtanzania kinadharia anadaiwa karibia Tsh 500,000 wakati hata hawezi kuingiza Tsh 1,500 kwa siku.
  Hii serikali inaiacha nchi na watu wake katika hali ya umaskini usio na tiba kizazi hiki na kijacho. Ni jambo la ajabu sana kwa serikali kukopa mabilioni ili yatumike kuboresha usimamizi wa hizo fedha wanazozikopa. It's sad if not fun.

  Habari kamili hapa chini;

  Benki ya Dunia kuikopesha serikali ya Tanzania Tsh 403,792,494,592 ili kuboresha usimamizi wa fedha na utoaji wa huduma katika serikali za mitaa, Tanzania yenye watu zaidi ya milioni 42 ni moja kati ya nchi zinazoongoza Afrika kwa upokeaji wa misaada inayotolewa na benki ya dunia. Taarifa ya benki iliyotolewa jumatatu imebainisha.

  Katika bajeti yake ya 2012/13 yenye jumla ya shilingi 15,120,000,000,000, Tanzania imatazamia kupata shilingi 3,160,000,000,000 ambayo ni karibia 21% ya bajeti kupitia misaada na mikopo yenye masharti nafuu.

  Umaskini bado ni kubwa licha ya utendaji imara katika nyanja ya kiuchumi. Tanzania ni nchi ya pili kubwa kiuchumi katika nchi za Afrika ya Mashariki. Kiasi cha asilimia 25 ya watu kwa sasa wanaishi mijini na kiasi hicho kitaongezeka na kufikia asilimia 40 ifikapo 2030.

  Philippe Dongier, Mkurugenzi wa benki ya dunia nchini Tanzania, anabainisha na kusema, "Uboreshaji na upatikanaji wa huduma katika maeneo ya mijini ni muhimu kwa ajili ya kuboresha ubora wa maisha ya wananchi wa kawaida wa Tanzania ili kupunguza umaskini.

  Taarifa nyingine kutoka benki ya dunia inabainisha kuwa, jumla ya Tsh 39,587,500,032 zimetengwa ili kuboresha usambazaji wa mbegu na mbolea kwa wakulima wanaokadiriwa kuwa Laki tatu (300,000), pia kiasi cha Tsh 47,504,998,400 kimetengwa ili Kusaidia upatikanaji wa dhana mpya na bora za kilimo na umwagiliaji wa kisasa.

   
Loading...