Hivi karibuni, kuna taarifa zilizowekwa wazi kwenye baadi ya vyombo vya habari, juu ya mgawanyo wa mikopo ya nje, kati ya Tanzania bara na Zanzibar.
Mkopo wa pesa ya Uviko 19, tunaambiwa Zanzibar ilipata 18%. Mkopo wa kutoka Japan, tunaambiwa Zanzibar imepata 30%.
Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, umeweka wazi kanuni ya mgawanyo wa mikopo na misaada kutoka nje, ambapo Zanzibar inastahili kupewa 4.5%.
Kama ni kweli Zanzibar ilipata 18% badala ya 4.5%, na pia ilipata 30% badala ya 4.5%, waliohusika wote, wakiongozwa na Waziri wa Fedha na Katibu Mkuu Wizara ya fedha, walistahili wasimamishwe mara moja, na kama tungekuwa na Bunge, lilistahili kuunda kamati kuchunguza ukweli wa jambo hili, na kuchunguza uhusika wa Rais katika ukiukaji huu wa kanuni za Muungano.
Jambo la kujiuliza:
1) kwa hali hii ya sasa, ambapo nchi haina bunge linalowakilisha wananchi, nani ataihoji serikali?
2) kama trend itaendelea hivi, mpaka kufikia 2025, hali itakuwaje?
3) kama hiki ndicho kinachoendelea, hatuoni kuna njama za kuitumia Tanganyika kuijenga Zanzibar, na kuifanya Tanganyika kuwa 'kubwa jinga?'
4) Hali ikiendelea hivi, na bunge hatuna, nani ataweza kuhoji juu ya jambo hili?
5) Je, hatuoni kuwa kama hali hii ni kweli, mikopo hii inailenga Zanzibar, na Tanzania bara inatumika tu kama daraja, huku kisheria deni likiwa la kwake?
6) Japo hatuombei, kama kukiwa na njama ambazo zikafanya siku moja Muungano ufe, hatuoni hasara itakayokuwepo kwa Tanzania bara kwa sababu madeni haya yote mkopaji ni yeye, na hivyo ndiye atakayewajibika kulipa?