mkopo wa million 6 za haraka haraka

Mrekebishaji

Senior Member
Mar 19, 2009
168
63
wadau,
Wana JF, nimekuja kwenu nina shida ya millioni 6, nitarudisha kwa miezi miwili, nitaweka rehani kadi ya gari yangu Rav 4, Milango 4. Naombeni msaada mwana jamvi mwenzenu, kuna jambo maji yapo shingoni.

Natanguliza shukrani.
 
mi mtakupa ila unaacha gari na kadi ya gari, riba 10% kwa mwezi, huduma hii inapatikana Mosh na Dar es salaam
 
nashukuru sana kwa msaada wako, mimi nio Dar es Salaam, mikocheni B, kwa Warioba. Natanguliza shukrani.
 
Hizi kazi ni ngumu jamani!!!...kadi aache na gari aache atafanyaje mishemishe zenyewe?....na ukikubali kadi bila gari mtu umefahamiana naye JF tu ni mtihani pia!!! Ukiniacha unaniogopa, ukinipiga unanionea!! Unaonaje ungeenda Benki mkuu, au ukamwona rafiki au ndgu wa karibu!
 
Mkuu, kuna jamaa wapo hapo katibu na kwa warioba, wanakopesha kwa rba kidogo, lakini lazima uache gari na kadi, mnakubaliana unarudisha lini, na unachukua gari yako, au kama vipi unakuwa unawaletea riba yao, unaendelea kuzungusha mtaji. wana yard kubwa tu, na hawagusi gari.
 
Jamani, nadhani nitakuwa nilieleweka kuwa pesa inahitajika kwa haraka, ndo maana nikaomba msaada wenu. hoja zote nimezisoma na kuzielewa, lakini naamini gari ya kadi itafaa, na gari utaiona, naweza pia kuweka mdhamini. mimi ni mfanyakazi na biashara pia., email yangu, chrisjohnjune@gmail.com
 
Nikusaidia mzee kwa riba ya asilimia 15 kwa mwezi, ila kadi na gari unaviacha kwa mkopeshaji
.
ndugu Mlugwanza, naomba msaada wako, ila tu si kwa kuacha gari, ila nina nyumba, ambayo nipo tayari uione, pia uwe na shahidi. Unajua tena gari ndio natembelea, ila kadi nitakupa.
 
Back
Top Bottom