Kama kuna watu walikuwa wanafikiria kwamba kuwabana upinzani, wanahabari na watoa maoni kutafanya chochote kiweze kufanyika wafiliri tena. Dunia ya siku hizi tunategemeana sana kiasi kwamba mtu wa kawaida tu ana uwezo mkubwa sana kuleta na kuzuia mambo mengi kama hamjakubaliana pamoja kama nchi. Angalieni wanaharakati kwenye hili ya mkopo wa shule walivyokuwa na nguvu bila mambo ya ubunge au chama.
Serikali zote sio Tanzania tu zijue wananchi wana uwezo mkubwa sana wa kusimamisha shughuli kupitia migomo ilimradi iwe na hoja tu. Kampuni za ndege kubwa ni mbili tu wanaharakati wana uwezo wa kuzuia ununuzi kwa kuongea na kampuni kama wana hoja.
Mitandao yote ya simu inatumia sofware za kampuni za hao tunaowaita mabeberu kwa urahisi tu wanaweza kusimamisha chochote lakini vilevile Dunia nzima manunuzi na malipo ya kimataifa ni kwa dollar na ndiyo maana US wana nguvu sana kwenye kuweka vikwazo maana ndiyo wenye dollar ni lazima uchukuwe kwa bank za US yaani bank to bank. Hivyo kuna mbinu nyingi sana zinaweza kutumika kuzuia vitu.
Kibaya huwezi kusema kama zamani hatuhitaji mabeberu. Uchumi wetu karibu wote unategemea mabeberu. Madini tuna mikataba na mabeberu, kampuni za simu mikataba na mabeberu, miradi bank za mabeberu, technologia ni za mabeberu, ndege zinatengenezwa na mabeberu, elimu yetu misingi yake ni ya mabeberu, dawa karibu zote zimegunduliwa na mabeberu za India wanapewa leseni tu ya kutengeneza.
Hivyo hii Dunia imekuwa yote ya kibeberu na wanaosema tofauti ni siasa tu. Mitandao yote hii ukiangalia ni kampuni za kibeberu hata hizo barua za serikali na wakaguzi wanatumia micro soft ambayo ni kampuni ya US. Technology ya nishati ya gas na umeme ni hao hao.
Ni muhimu sana kama nchi tujasiliane maana viburi na kutokuelewana ndiko kutaleta haya majanga ya bank ya dunia. Wakati wa Kikwete alikuwa anaongea na watu na wapinzani kwa sababu ya vitu kama hivi. Haya mambo tujue tu yataongezeka kama hatuko wamoja.