Mkopo kwa continuous students

kunta93

JF-Expert Member
Nov 9, 2015
750
1,482
Jaman wapendwa,Mimi Ni mmoja WA continuous students walio omba mkopo niko Udsm mwaka WA pili,nilikua nauliza kama Kuna mtu Ana taarifa juu ya hatma yetu atujuze hapaa plzz
 
swali la nyongeza kuna continuous yeyote aliye pata mkopo kwenye hizi lots zao??? heslb watufikirie katika hili aisee dah
 
Mimi ni mwanafinzi wa second year na wazazi wote walisha fariki ila Sijui hatima yangu kama nitapata mkopo baada ya awamu zote 3 kupita bila kupata mkopo
Au ndo tumesaulika?
 
Mie pia nipo second year BED, UDOM. Mwaka jana sikuomba ila mwaka huu nimeomba na mpaka sasa naona empty!! kusoma bila mkopo ni zaidi ya mateso aiseee. Kama kuna continous aliyapata mkopo atupe moyo basi!!!!!
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa imetoa orodha ya Awamu ya Tatu yenye jumla ya waombaji wa mwaka wa kwanza6,915waliopangiwa mikopo.
Kati ya waombaji hawa waliopangiwa mikopo, waombaji4,642ni wale wanaojiunga na shahada ya kwanza katika vyuo mbalimbali nchini na waombaji2,273ni wanafunzi wanaojiunga na Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa masomo ya sayansi na hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Kwa msingi huo, Bodi inapenda kuufahamisha umma kuwa hadi sasa imekwishawapangia mikopo jumla ya waombaji mikopo wenye sifa47,751wa mwaka wa kwanza. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji12,282; Awamu ya Pili wanafunzi28,554na Awamu hii ya Tatu wanafunzi6,915wamepangiwa mikopo.
Majina yote ya waombaji waliofanikiwa kupangiwa mikopo kutoka katika awamu zote tatu yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi waolas.heslb.go.tzna tovuti ya Bodi ( Higher Education Students' Loans Board -HESLB). Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.
Mwisho.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Novemba 13, 2015
 
Back
Top Bottom