Mkono: Wafanyabiashara ni Kundi Rasmi, CCM Haina Budi Kutambua

Mafuchila

JF-Expert Member
Apr 29, 2006
751
65
Rostam, Chenge, waonyesha jeuri ya fedha kwa John Cheyo
Na Anceth Nyahore
18th January 2010

Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, ni miongoni mwa waliochangia fedha na kushiriki katika harambee maalum iliyoandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bariadi, ambayo inadaiwa kuwa ina lengo la kulikomboa Jimbo la Bariadi Mashariki. Jimbo la Bariadi Mashariki kwa sasa linashikiliwa na Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP), John Momose Cheyo.

Hata hivyo, uongozi wa CCM Wilaya ya Bariadi umesema kuwa lengo la harambee hiyo ni kuhakikisha kwamba chama hicho tawala kinafanya vizuri katika uchaguzi mkuu hususan wilayani Bariadi.Katika harambee hiyo, chama hicho kimefanikiwa kujipatia zaidi ya Sh. milioni 190 ambapo kati ya hizo, Chenge pamoja na marafiki zake takriban 10 akiwemo Rostam, walichangia Sh. milioni 55.

Harambee hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Musoma Vijijini, Mkono, ilifanyika mwishoni mwa wiki. Hata hivyo, Katibu wa CCM mkoani Shinyanga, Mohamed Mbonde, aliliambia Nipashe kuwa harambee hiyo iliyoandaliwa na chama hicho, ni kwa ajili ya kufanikisha gharama za uchaguzi mkuu na ujenzi wa jengo la CCM la Wilaya ya Bariadi.Lakini Katibu wa CCM Wilaya ya Bariadi, Jumanne Kasote, alisema harambee hiyo ni kwa ajili ya kukijengea uwezo chama hicho kuwa na fedha katika uchaguzi mkuu na ujenzi wa ofisi ya CCM ya Wilaya ya Bariadi.

Jumla ya Sh. milioni 69.368 fedha taslimu zikiwemo hundi, zilitolewa na ahadi ya Sh. milioni117.705 na mabati 2,000 yenye thamani ya Sh. milioni tatu yalipatikana.
Habari kutoka kwa baadhi ya wanachama, wakereketwa na wapenzi wa chama hicho waliopewa kadi za mwaliko wa harambee hiyo zilidai kuwa lengo lake ni kuhakikisha CCM kinalirudisha mikononi Jimbo la Bariadi Mashariki.

Mbali na mkakati wa kumg’oa Cheyo, pia lingine ni kuhakikisha kuwa CCM inaibuka na ushindi mnono katika uchaguzi wa madiwani wa halmashauri hiyo yenye kata 23. Katika Halmashauri ya Bariadi, UDP ina kata 12 na CCM kata 11 na hivyo halmashauri hiyo kuongozwa na chama hicho cha upinzani.

Katibu wa CCM Wilaya ya Bariadi, Kasote alisema harambee hiyo iliwashirikisha Mbunge wa Viti Maalum, Anna Lupembe kutoka mkoani Rukwa, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Yohana Balele, Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga, wanachama, wakereketwa na wapenzi wa CCM na baadhi ya wafanyabiashara maarufu wilayani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Balele, aliahidi kutoa Sh. milioni tano, Mweka Hazina wa CCM Wilaya ya Bariadi, Emmanuel Silanga, alitoa Sh. milioni 10 yeye na marafiki zake wengine 10 ambao kwa pamoja walitoa Sh. milioni 20 akiwemo mfanyabiashara Njallu Silanga ambaye ni ndugu wa Mweka Hazina wa CCM wa wilaya hiyo.

Aidha, mwanachama mwingine, Martine Makondo, anayedaiwa kulinyemelea Jimbo la Cheyo, alichangia Sh. milioni tatu huku akitoa fedha taslim Sh. milioni moja na ahadi ya Sh. milioni mbili.Christina Chenge ,ambaye ni mke wa Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, alichangia Sh. 500,000.

Aidha, mgeni rasmi katika harambee hiyo, Nimrod Mkono, alisema wakati umefika kwa CCM kuwa na mafiga matatu kwa kuwa na makundi ya wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara na siyo wakulima na wafanyakazi tu.

Alisema katika harambee hiyo yeye kama mmoja wa wafanyabiashara sasa CCM haina budi kulitambua kundi la wafanyabiashara.

Cheyo akizungumzia mkakati na harambee hiyo, alisema kamwe haoni jambo jipya kwake na kwa chama chake kwa kile alichodai kuwa hata mwaka 2005, CCM ilichanga mamilioni kwa ajili ya mgombea wao, Danhi Makanga lakini yeye alimbwaga kwa kura nyingi.
Hata hivyo, Mbunge huyo amewatahadharisha wananchi kutoruhusu kununuliwa kwa fedha kutoa kura zao kwa viongozi wasio waadilifu.
CHANZO: NIPASHE
 
mkono alikuwa amelewa nini, sisiemu inawatambua wafanyabiashara-mafisadi tangu azimio la zanzibar.
 
Halafu tunadanganyana humu eti oh wako wapiganaji, nani kasema?
 
Haya ngoja tuone namna ya mafiga matatu ya CCM yanavyofanya kazi.
 
Sidhani kama wafanyabiashara ni tatizo kutambuliwa na CCM. Tatizo wafanyabiashara wengi ni wezi lakini wanajificha nyuma ya mgogo "BIASHARA"! Na hapo ndio CCM inafulia.
 
Wafanyibiashara na Siasa haviwezi kutenganishwa. Hata kwenye mataifa makubwa yaliyoendelea na kuwa na demokrasi iliyobobea, wafanyibiashara ni sehemu muhimu katika siasa.
 
Ndo maana watu kama Berluscon wanapeta huko Italy, kisiasa na kibiashara
 
Hili kundi la wafanyabiashara, wanafanya biashara gani? Hivi tuongee ukweli hasa ...ok mkono mwanasheria....chenge je anafanya biashara gani? Na mzee wa caspian je? Na anonymous mamluki wanafanya biashara gani?

Biashara...enh wafanya biashara? Uuups!!!!!!!!!!!!

Hilo kundi hilo...sijui!!!!!!!!!!!!!!
 
Pathetic swindlers! Where did they get all that money if not through using government machinery at the expense of suffering, poor taxpayers?!
 
Kweli kabisa wafanyabiashara ni kundi kubwa ambalo wana sehemu ya ku-share katika kuendeleza nchi lakini hawakusema kwamba wafanya biashara wa nchi kubwa duniani wanalipa kodi bila mkwaruzo wowote na wanajulikana kila mwaka wanalipa kiasi gani cha kodi na statistics zipo.

Je, wanaweza kutuambia hao wafanya biashara wanaokumbatiwa na Chama Cha Majambazi wanalipa kodi kiasi gani? Je, wameweza ku-declare mapato yao pasipo udanganyifu wowote? Je, yeye binafsi Mkono na kampuni zake anaweza kusimama na kusema amelipa kodi halali kwenye biashara zake zote na mapata haramu aliyolipwa kutoka BOT?
 
Rostam, Chenge, waonyesha jeuri ya fedha kwa John Cheyo
Chenge pamoja na marafiki zake takriban 10 akiwemo Rostam, walichangia Sh. milioni 55.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Balele, aliahidi kutoa Sh. milioni tano
Mweka Hazina wa CCM Wilaya ya Bariadi, Emmanuel Silanga, Sh. milioni 10

Mimi naomba tu TRA wapitie makbrasha yao kujiridhisha kuwa hawa watu kwenye TIN zao inaonekana bayana wanavyolipa kodi. Tukikubaliana katika hilo hakuna wasi kabisa, waendelee tu kuchangia hata mara 100 zaidi.
 
Back
Top Bottom