Mkono: Kumekuwa na mchezo mchafu uliofanywa na kenya

UNO

Senior Member
Feb 3, 2012
197
19
Mheshimiwa Mkono; akichangia bajeti ya wizara ya ujenzi kuhusu ujenzi wa barabara ya Serengeti; ameonya jinsi Watz wanavyoshindwa kuendelea kujenga barabara ya Serengeti akisema kuwa Kenya imefanya mchezo mchafu ili kuzuia barabara hiyo kujengwa. Watz wana paswa kuamka na kufanya yale ambayo wanafikiri yatakuza uchumi wao. Ukijenga barabara hiyo ni wazi kuwa itaboresha utalii katika mbuga hiyo kwa kutumia muda mfupi kufika huko, na hivyo kuathiri upande wa wenzetu. Kwa hiyo watakazana kutoa sababu lukuki na kuwarubuni wanamazingira eti wanyama watakimbia. Mbona mbuga zao zimejaa majengo na mabarabara??? Maghufuli kuwa macho kwa hili uwafanyie watz kitu.
 
Kama serikali yetu in hekima kweli, basi haitakubali kupangiwa maeneo ya kuyaendeleze na majirani zetu. Kwanza Serengeti ipo Tanzania na siyo Kenya, tena ni mali na urithi wa watanzania na siyo wakenya. Kwanini watu wengine watuamulie mambo yetu ya ndani? Tukikubali tutakuwa wajinga kabisa. Na wakenya wameshakuwa wakitudhibiti kwenye maeneo mengi, walituzibia kuuza pembe zetu za ndovu ambazo ziko katika maghala yetu, sasa wanataka kutuzuia kujenga barabara Serengeti. Nina wasiwasi na hii serikali dhaifu kwamba itasalimu amri tu.
 
Back
Top Bottom