SoC01 Mkono Mtupu Haulambwi

Stories of Change - 2021 Competition

GoPPiii.

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
1,787
3,050

Nilibahatika kuitwa kwenye usaili wa kazi, kielimu nimehitimu mafunzo ya Udaktari mwaka 2018, na endapo ningefaulu usaili ule basi ningekuwa mkuu wa kitengo cha afya kwenye taasisi hiyo. Nilifanya maandalizi ya kutosha. Katika maswali niliyoulizwa nijieleze lilikuwa, “how well are you connected and informed” yaani “ni kwa namna gani nina fahamiana na watu na kuwa na taarifa sahihi?

Ukweli ni kuwa sikujua uzito na umuhimu wa swali hili, nilijua nimeulizwa kwa sababu ya umuhimu wa kazi na nafasi nilikuwa nimeiendea. Hakika ndilo swali lililochangia mabadiliko kwenye maisha yangu, mahusiano, uchumi na kisiasa.

Ni muhimu kujua katika maisha ya kila siku tunahitaji kufahamiana na watu mbali mbali haswa kwa nafasi mbali mbali kijamii. Ni ukweli usiopingika dunia ya sasa ni vigumu kuulamba mkono mtupu, unaweza sema sio utu lakini ndio tulipo sasa. Mara ngapi umehitaji huduma pengine uliipata kwa kuchelewa au hukuipata kabisa kwa sababu hukufahamiana na mtoa huduma hiyo?

Tumekuwa tukiwalaumu watu waliofanikiwa kimaisha, kisiasa na kiuchumi kuwa wanapendelewa, je tunajua ni juhudi kiasi gani waliweka ili kuwa well connected (kufahamiana) na hii yote ni kuendana na dunia ya sasa kuepusha usumbufu tunaouita kupendeleana sisi tusionacho.

Mara ngapi tumejihusisha na mikutano/semina zozote mfano za kidini,ujasiriamali,mambo ya kijamii (Zile za mashirika binafsi, Mabenki, vikundi vya kiharakati) hata zile zinazoandaliwa maeneo karibu na tunamoishi?, ushiriki wetu kwenye masuala ya kijamii kama sherehe,majanga, misiba, maendeleo ya mitaa yetu kama usafi, kuchimba mitaro, kupanda miti,upoje, je ni wa kuridhisha au hafifu kwa kupuuza kuwa hayatuhusu.

Mikutano hii ndimo tunakutana na watu mbali mbali wenye nafasi mbali mbali kwenye jamii, Waalimu, madaktari, wanasiasa,wachungaji,polisi,madereva,wafanya biashara,mahakimu/majaji hata wale wasiokuwa na kazi rasmi.Tusipojihusisha na hawa watu hii tutafahamiana vipi, ni nani atakayerahisisha jambo lako?

Ni bahati na sio bahati kwa baadhi yetu, bahati kwa wale waliokuta mazingira yako tayari yameandaliwa, familia zao ziko na zinafahamiana na watu mbali mbali, na ni bahati mbaya kwa wale wasiokuwa na haya maandalizi, hivyo ni jukumu letu kujiandaa na pengine kuandalia vizazi vijavyo.

Hizi ni baadhi ya mbinu nimetumia kuhakikisha najitahidi kufahamiana na watu;
  • Kuchangamana na kujihusisha na watu ninaokutana nao kataika harakati zangu za kila siku.​
  • Kutoogopa kuomba mawasiliano na kuwasiliana nao kadri ninavopata nafasi, sio tu ninapokuwa na shida.​
  • Kutokuwa mchoyo, kila ninapohudumiwa najitahidi kutoa shukrani kwa maneno au vitendo, kila binadamu anapenda kujihisi wa muhimu haswa pale anapotoa huduma. Hii shukrani sio Rushwa.​
  • Kujifunza ujuzi mbali mbali,nimejifunza japo kwa uchache,uashi, ufundi umeme, ufugaji (kuku, sungura, mbwa),nimejifunza masuala ya sharia,mpira, muziki,hii imenikutanisha na watu mbali mbali,tukajuana,tukashirikiana. Hii inafaida kwamba wengi wa watu mtakaokutana mtakuwa na jambo linalowaunganisha.​
  • Kusoma vitabu mbali mbali, hii imeniongezea maarifa, namna ya kujieleza na kufikiri,pamoja na upembuzi wa mambo.​
  • Kutii mamlaka za ngazi zote. Hii imeniepusha kuwa kwenye matata wakati wote.​
Ninaamini nawe utatafuta mbinu kuliweka hili suala sawa.


Kipengele cha pili cha swali kilisema “How well am I informed” kikiwa na maana ninakuwa na taarifa/maarifa au nina taarifa/maarifa kiasi gani.

Ni swali pana kidogo, ila linahitaji mambo yafuatayo;​
  • Je nahitaji taarifa/maarifa yoyote?​
  • Nahitaji taarifa gani au maarifa gani?​
  • Nitapata wapi taarifa/maarifa ninayohitaji?​
  • Nitazitumia vipi hizi taarifa au haya maarifa?​
Kitu cha kwanza ninachohitaji kujua ni kama ninahitaji taarifa au maarifa yoyote yale katika shughuli au maisha yangu ya kila siku, Kama ni NDIO basi je ni taarifa gani ninazohitaji au ni maarifa gani ninazohitaji. Hapa ni vema kuweka bayana ni kipi haswa unahitaji.

Kipengele cha tatu ni wapi nitapata hizi taarifa. Hapa ndipo ugumu huonekana. Mimi pia ilikuwa ikinitokea nilipohitaji kujua kuhusu biashara niliwauliza madaktari wenzangu. Hii imenipelekea kuwa na taarifa zisizo sahihi, au zilizo pungufu na zisizojitosheleza.

Wengi wetu tumekuwa wavivu wa kutafuta Expert opinion/review/advice yaani jicho la wataalamu.Hivi sasa wengi wetu hutafuta habari, tena zile nyeti kwenye vyanzo ambavyo sio rasmi. Tunakimbilia Instagram, kurasa za fesibuku, mitandao ya udaku, tunapenda vipindi vya udaku kwenye televisheni na radio,pengine ndizo taarifa tunazopenda, lakini je ni zile tunazohitaji kututoa sehemu moja kwenda nyingine?

Nimekuwa nikijitahidi kutafuta taarifa sahihi na maarifa sahihi,ziwe kuhusu chochote nilichohitaji. Hii imenisaidia kuwa na taarifa na maarifa sahihi.
  • Nilipohitaji mambo ya kisheria nilitafuta wanasheria.​
  • Nilihitaji taarifa za kisiasa nilifuatilia wanasiasa na taarifa zao.​
  • Nilipohitaji mambo ya biashara nilijitahidi kuwatafuta wafanyabiashara au wajasiliamali​
  • Nilihitaji ushauri wa kitaalamu haswa ufundi niliwatafuta mafundi na walinisaidia.​
  • Nilipohitaji kilimo niliingia shambani kwa msaada wa wakulima wazoefu.​
Mwisho haya yote niliyatumia kwa usahihi na hata pale nilipokuwa na watu wengine nilionekana nina kitu cha ziada, ilinirahisishia mahusiano na watu.

Dunia ya sasa inahitaji inahitaji kuhusaiana na watu kama vile tusemavyo “Nchi yetu sio kisiwa” Vile vile sisi na maisha yetu hatuko peke yetu, tunahitajiana yaani tuwe tayari pale tutakapohitajika kama vile tunavotaka wengine wawe tayari kwa ajili yetu. Mwisho tukumbuke mkono mtupu haulambwi. Tuhakikishe tuna taarifa au maarifa sahihi mda wote zitakapohitajika.

Hii huleta;​
  • Kujiamini.​
  • Huleta utofauti (Ukiwa kwenye kundi la wengi)​
  • Huongeza ufanisi kazini.​
  • Wengi watahitaji kujuana nawe.​
ASANTE.​
 
Back
Top Bottom