Mkongoro, Kigoma: Watu 7 wamefariki katika ajali iliyohusisha gari aina ya Scania Lori

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,495
Watu 7 wamefariki katika ajali iliyohusisha gari aina ya Scania Lori iliyotokea katika kijiji cha Mkongoro Kigoma. Chanzo cha ajali, ni Dereva wa Lori kushindwa kulimudu gari wakati akishuka kwenye mteremko uliokuwa na kona kali na kumgonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka.
aj.jpg
aj2.jpg
 
Pole Kwao, ni watu wa CHAMA gani?

Je , walikuwa wanakwenda kununua madiwani? Ili tujue kama Mungu kawalipa ama tutoe pole
 
ILO Lori lilikuwa na sticker YA usalama barabarani kweli au Chuma chalavuuuuu kwa sababu ajali Zipo nyingi Lakin ihiii Kila kitu kipo kivyakeeeeee... Inaonyesha gari ilikuwa imechoka sanaa
 
Taarifa zilizoifikia TBC hivi punde kutoka ofisi ya RPC Kigoma zinasema watu 7 wamefariki baada ya lori walimokuwamo kupinduka na mmoja alikuwa ni mpita njia. Source TBC
Mkuu ofisi ya RPC ndio ilitoa taarifa kama hii ilivyo?!

Hii taarifa inaacha maswali mengi kichwani;
-Kigoma ni kubwa, ilikuwa eneo gani?
-Sababu ya lori kupinduka?
-Lilikuwa linatoka wapi?
-Majina ya marehemu?
 
mmmh ajali sio kitu poa asee yaan scania imefumuka fumuka hivyo daaah R.I.P
Mungu tuepushe na janga la ajali
 
Wazee wa ujiji washafanya yao maana ajali ya nne hii kutangazwa. Poleni wafiwa
 
Back
Top Bottom