Mkonga wa taifa ni nini ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkonga wa taifa ni nini ?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Ami, Jun 29, 2011.

 1. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Napenda nisaidiwe kujua huu mkonga wa taifa ni nini?. Una tofauti gani na mikonga mingine tuliyonayo.

  Hapo hapo kuna faida gani kuwa na mikonga na kutokuwa nayo.
   
 2. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  kabla ya kukujibu ili uelewe labda nikuulize . Hiyo mikonga mingine tulinayo ni ipi? Unaweza kutoa mfano
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Ujue huyu jamaa mkonga wa taifa anajua ni kama ile milingoti ya vodacom,tigo, ttcl nk...hahaaa!!
  Ngoja tuwasubirie wengine.
  Kwa mm ninavyojua, mkonga wa taifa ni system ya mawasiliano itayosambaa tanzania nzima, mawasiliano yake ni kwa fibre cables ambazo zinapitia chini ya ardhi na nyingine baharini, na uchimbajiwa wa hizo bomba unaendelea nchini

  Ombi: Nilipenda nijiuinge na hawa jamaa wa uchimbaji wa mkongo, mwenye kujua pa kuanzia aniPM tafadhali.
   
 4. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Hapo kwenye red upo sahihi kabisa.

  Kwa kifupi ni kwamba mkonga ni neno la kiswahili lililoongezwa kwenye kamusi miaka ya karibuni kumaanisha optics fiber kwa lugha ya kigeni.

  Kwa faida ya wengine, Fiber optics ni aina ya waya (cable) kama hizi tulizozizoea za kupitisha umeme au simu ambazo kwa kawaida huwa zinatengenezwa na madini ya shaba (copper) ila sasa, mkonga (fiber optics) unatengenezwa na aina ya material kama inayotumika kutengeneza kioo (glass),

  Kwa hiyo ni cable ambayo ni kioo na hutumika kusafirisha mawimbi (signal) ambayo yamegeuzwa kuwa mwanga (light). Hiyo cable ambayo ni kioo ni nyembamba sana, unene wake ni kama unene wa unywele wa mwanadamu na ndio maana inaitwa fiber (fibre) na kwa sababu mawimbi yanayosafirishwa ni mwanga (light/ optic) ndio maana inaitwa fiber optic.

  Kumbuka kwa kuwa fiber ni nyembamba sana na delicate huwa inawekewa protection kubwa sana kuizunguka (insulation) ndio maana unaiona imekuwa ni cable nene.

  Kuna aina kuu mbili ya kusafirisha mawimbi ya mawasiliano. Moja ni kwa kupitia hewani (wireless network) na nyingine ni kwa kupitia kwenye waya (cable or wired network) ambayo kwenye hiyo njia ya kwanza kuna technolojia nyingi sana kama microwave antennas ambayo ndiyo makampuni ya simu km Vodacom, Tigo, Zain network yao kubwa inatumia hii technolojia,

  pia ipo sattelite communication ambayo vituo vingi vya redio na Tv vinatumia, pia kuna technolojia ya wifi na nyingine nyingi sana.

  Kwenye hiyo technolojia ya pili inategemea zaidi ni aina gani ya cable unaitumia, inaweza kuwa shaba (copper) kama kwenye simu za landline za TTCL au inaweza kuwa mkonga (optic fiber) kama ambayo sasa serikali imeamua itumie kwenye hiyo network ya taifa ya mawasiliano ambao wanauta sasa Mkonga wa Taifa ambayo kwa mujibu wa malengo yao ni kuunganisha wilaya zote za nchi hii (sasa sijui itawezekana maana umeme tu ni tatizo na hata ikiwezekana bila umeme sijui zitatumika kufanya nini !!).

  Huo mkonga wa Taifa kuna sehemu umepita ardhini na pia kuna sehemu nyingine umepita kwenye gridi ya taifa ya umeme. Kama ukipita sehemu yenye nguzo za umeme za gridi ya taifa kutokea ubungo kwenda mikoani utaona cable mbili juu kabisa hizo ndio mkonga wa taifa (achana na cable tatu za chini ambazo ni za umeme).

  Mkonga wa taifa umeunganishwa na fiber ya TTCL baadhi ya sehemu na pia unaunganishwa na fiber ya makampuni mengine inayopita baharini kuelekea nchi zingine. Kitu cha kunote ni kwamba, mkonga uliopita baharini sio mkonga wa taifa, ule unamilikiwa na makampuni binafsi.

  Maelezo ni mengi, ila nadhani kwa haya mafupi umepata angalau hints.

  Cheerz.
   
 5. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mkonga wa taifa kwenye network kwa kimombo tunaweza kuita Network backbone. In this case in internet backbone Na backbone tafsiri yake ni uti wa mgongo. Soma hapa http://en.wikipedia.org/wiki/Backbone_network hasa kipengele cha Internet backbone unaweza pata picha

  Kama ulivyo uti wa mgongo wa wanyama ulivyo muhimu bila uti wa ngongo basi hata mikono miguu haiwezi kufanya kazi basi hata huo mkonga wa taifa ukikamilika kwenye mikoa yote basi bila wenyewe hata ISP.

  So wanchofanya ni Kutandaza cable ya Tier-1 Tier 1 network - Wikipedia, the free encyclopedia amabayo ndio kama uti wa mgongo . From hiyo tier 1 ISP na makampuni wengine watachukua na wenyewe kugawa au kuuza kwenye makampuni.

  Hope kama sijakuchanganya umeelewa.
   
 6. mchapa shughuli

  mchapa shughuli JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 529
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 80
  Angalizo:mkongo
   
 7. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kwani vipi?.Mimi sijafahamu.
  Nyaya kama zile za simu za TTCL zinazopita juu ya maguzo na nyengine kuingizwa kwenye mashimo tunapoona mafundi wakishinda kutengeneza ndio najua ni mikonga.Sasa hii mingine ina umuhimu gani?.
   
 8. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Observer2010

  Cheerz.[/QUOTE]
  Naomba usichoke kunijibu kwani tupo wengi wa aina yangu.
  Jee sisi watz ni wangapi duniani kuweka huu mkonga au mkongo?.Jee tayari umeanza kutumika sehemu yoyote kule ulikokwisha kupita?.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #9
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Usichoke kuuliza, maana kuuliza ni kuelewa. Mawasiliano ya fiber optics yalianza kutumika nchi zilizoendelea miongo kadhaa sasa takribani tokea miaka ya 1980's kabla ya hapo mawasiliano yalikuwa yanatumia copper cable. Kumbuka cable za baharini (copper) zilianza kutumika miaka mingi sana iliyopita zaidi ya miaka 150 iliyopita, na cable ya kwanza kabisa ya baharini iliunganisha Uingereza na Ufaransa.

  Baada ya kuona sasa usafirishaji wa mawimbi ya mawasiliano (transmission signal) kupitia kwenye copper kuna kabiliana na matatizo mengi ikiwamo upotevu mkubwa wa mawimbi na pia uwezo mdogo wa copper kubeba mawimbi mengi (limited bandwidth) watafiti ndio wakaja kugundua fiber optics. Hii cable ina uwezo mkubwa sana wa kubeba mawimbi (unlimited bandwidth) na pia mawimbi hayapotei kwa urahisi na pia haiathiriiwi na mawimbi ya umeme sumaku (electromagnetic waves) hii ndio maana zinaweza kufungwa kwenye nguza za umeme mkubwa (high voltage transmission lines).

  Kwa kifupi maeneo ya mashariki mwa Afrika (ikiwemo Tanzania) ni ya mwisho mwisho kabisa kuanza kutumia hii technolojia kati ya maeneo yote yanayopakana na bahari (ukiondoa land locked countries). Cable hii ilishakuwepo southern Africa, western Africa, Asia, Far East, Europe na Amerika (north and south) kwa miaka mingi tu.

  Hope nimekujibu swali lako.

  Cheers !!
   
 10. Mushi92

  Mushi92 JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2014
  Joined: Oct 5, 2013
  Messages: 2,782
  Likes Received: 1,191
  Trophy Points: 280
  1 Una maanisha huo mkongo wa taifa utakuwa unatumiwa na makampuni ya simu....au itabid nijiungr nao ili kupata mawasiliano...?
  2. Hizo cables zina unganishwa bahari nzima.. kama nyaya za umeme...?
   
Loading...