Mkombozi wa Tanzania huyu hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkombozi wa Tanzania huyu hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ufunguo, Oct 28, 2012.

 1. Ufunguo

  Ufunguo JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  1. Tuwe na vyama vya siasa visivyozidi 3.
  2. Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi marufuku kuwa wanasiasa wala kuteuliwa katika nyadhifa mbalimbali ndani ya serikali.
  3. Tubadili mfumo wetu wa elimu kutoka huu wa kinadharia kwenda wa kivitendo zaidi ili tuondoe utegemezi wa kitaalamu hasa katika sayansi na teknolojia.
  4. Elimu ya Uraia ipewe kipaumbele ili wananchi wote wajue haki na wajibu wao kama raia wa Tanzania.
  5. Makosa yote ya Rushwa adhabu yake iwe kifo (am serious), maslahi ya Taifa mbele..
  6. Nafasi zote za taasisi za serikali, mikoa, wilaya, ukatibu mkuu, n.k zitangazwe na watu wote wenye sifa waombe na wafanye kwa mikataba ya miaka 3 baada ya hapo wapimwe utendaji kazi wao, wasipokidhi malengo yaliyowekwa wawekwa pembeni.
  7. Kila mtanzania awe na kadi ya kupiga kura maana hiyo ndo nguvu yake pekee na ashiriki kikamilifu zoezi la kupiga kura mahali popote alipo ili mradi tu kadi yake imethibitishwa kuwa halali (kumlazimisha mtu apige kura mahali alipojiandikisha ni kuingilia haki na uhuru wa mtu binafsi, ibara ya 15 ya katiba).
  8. Kuwe na kura ya maoni ya watanzania wote hasa tunapoona utendaji wa Rais hauridhishi kama ulivyo kwa sasa ili kumwadabisha.
  9. Kuwe na mgombea binafsi maana wagombea wa vyama wengi wanaingizwa kwa fedha za mafisadi, hivyo uwezo wa kuwashughulikia mafisadi wanakuwa hawana (Mkono unaokulisha huwezi kuung’ata, vinginevyo utakuwa kichaa).
  10. Apatikane kiongozi ambaye atakuwa tayari kufa kwa ajili ya maslahi ya nchi (awe tayari kufumua mizizi yote ya chama tawala ndani ya taasisi mbalimbali kama jeshi, usalama wa taifa, mahakama, bunge n.k )
  11. Maliasili zote za nchi ziwanufaishe kwanza wananchi wa mahali husika, pia mikataba yote ya wawekezaji ipelekwe bungeni na baadae kwa wananchi husika ili wajue kilichoko ndani ya mkataba kama kina maslahi kwao ama la na wananchi ndo wawe waamuzi wa mwisho.
  12. Tanzania kama nchi tuwe na vision, mission, goals n.k ambapo serikali yoyote itakayoingia madarakani lazima itekeleze mambo ya msingi ya nchi. Sio kama sasa ambapo kila anayeingia madarakani anaweza tu kubadilisha mifumo mbalimbali kwa maslahi yake binafsi. Kama ilivyotokea waziri alivyofuta somo la kilimo mashuleni na kuondoa michezo!
  13. ……..
  14. ……..

  Je wewe mwanajamii unasemaje?, naruhusu mjadala na mapendekezo mengine zaidi….

  Aluta continua.
   
 2. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Well, mimi nadhani mkombozi wa Tanzania ni wewe mwenyewe. Ili yote uliyorodhesha yaweze kufanya kazi ni lazima mimi na wewe tubadilike kwanza kwa mtazamo wa kujikomboa wenyewe. Tuondoke kwenye kutazama serikali kama engine for change, we are the engine for change and not the government. Mfumo uliopo hauwezi kubadilika wenyewe kwa kuandika humu JF, tunahitaji kuonyesha sisi wenyewe tumebadilika kwa vitendo. Kwa hiyo tuanze kwanza sisi kunadilika na baadaye mfumo utafuata vinginevyo ni blaa blaa tu hizi.

  Mwisho nakushauri upeleke maoni yako haya kwenye tume ya mabadiliko ya katiba.
   
 3. Ngagarupalu

  Ngagarupalu Senior Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ufunguo:
  12. Tanzania kama nchi tuwe na vision, mission, goals n.k ambapo serikali yoyote itakayoingia madarakani lazima itekeleze mambo ya msingi ya nchi. Sio kama sasa ambapo kila anayeingia madarakani anaweza tu kubadilisha mifumo mbalimbali kwa maslahi yake binafsi. Kama ilivyotokea waziri alivyofuta somo la kilimo mashuleni na kuondoa michezo!


  Hii utaipataje...... na inakuaje ukombozi.
   
 4. Ufunguo

  Ufunguo JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nachotaka kusema ni kwamba kusipokuwa na mipango ya muda mrefu na mifumo endelevu tutaishia kuzunguka duara na kujikuta tuko palepale miaka yote.
   
 5. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Aisee mimi nimekuunga mkono na kukupa hongera sana . Ila hapo 9&10 kw anchi hii haiwezekenaki kabisaa. Ukiruhusu mgombea binafsi, basi nchi za kiarabu kama vile Iran, Oman na Saudi Arabia lazima zitamfinance mtanznaia awe Kibaraka. Upende usipende . hapo lazima utampata raisi kibaraka wa nchi za kiarabu.
  Harafu kumpata mtu atakaye weza kufia maisha ya Mtanznaia, kwa hivi sasa haitatokea tena kumpata mtu kam vile sokoine au enze za lyatonga akiwa waziri wa mabo ya ndani.

  Kuna kitu kiichwacho, the world of matealiristic. Karibia kila mwansiasa hapa tanzania, antaka kuwa na nyumba nzuri , magari manne manne ya kifahari, na kusomesha watoto nchi za nje. huu ugonjwa umewambukiza wote wazuri na wabaya na hautibiki kabsaaaaaa! Dawa yake ni sisi kupigania kifungu cha adhabu ya kifo kwa wala rushwa n wezi wa mali ya umma. halafu kifungu kimkingacho raisi asishitakiwe lazima kifutwe na kiwekwe kile kitakacho mshitaki raisi akienda kinyume na cha katiba. mimi na wewe tupiganiye haya mawili tuu, utaona jinsi nchi itakavyoo katika mfumo wa ligi kuu za kujenga uchumi duniani.

  nakuhakikishia kuwa , ukitoka tuu nje ya nchi, tanznaia tuna jina baya sana haswaa ktk uwezo wa kujenga uchumi na kupunguza ukosefu wa ajira kwa watu wake.
   
 6. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  halafu sera za tanzania za nchi za nje zinainfluence kubwa sana kutoka nchi za kiarabu. Hii inatutibulia sana wawekezaji wa maana kutoka western europe na marekani pamoja na Israeli. Yaani huu utumwa wa kuogopa nchi za kiarabu kama tukienda Israeli kuomba misaada , ni kutesa wananchi kuliko kuwanufaisha waarabu. Ukosefu wa jira lazima upiganiwe kufa na kupona ili watu wapate kazi baada ya kutapeliwa na siasa ya ujama anakujitegemea kwa miaka 40.

  Kumkomboa Mtanznaia ktk ukosefu wa ajira, lazima tusingumane na waarabu ktk chuki zao kwa mataifa ya west europe , Israel na marekani. Ukifika hivi sasa vietnam, au Jordan, utakuta karibia viwanda vyote vya magari vya kimarekani vinatoa ajira ktk nchi hizo.
  Hapo west bank palestina, unemployment ni 10% jinsi mataifa ya west na marekani yanavyo saidia wapalestina. Sasa mtanzania bado anichukia Israel kwa sababu ya mahangaiko ya wapalestina, huku mpalestina tayari anakura kuku za wamarekani na waulya magharibi. Unaona jinsi waarabu walivyo na influence mbaya katika sera zetu za mambo ya nje? nchi haitaki kubadilika mpaka leo, je tutafika kweli?
   
 7. Ngagarupalu

  Ngagarupalu Senior Member

  #7
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo kama hiyo No. 12 itafanyiwa kazi tutafungua ukurasa mpya na hama chochote kutuzuia kuanzia No.1-11, vinginevyo ni cycle tu!!! hapo tuposawa.

  Kama mm ningeulizwa leo, binafsi kabla ya katiba ni Vision, Mission na Objective za taifa kwa raia na maliasili zao kwa vizazi vyao reviewable every 25 years.
   
 8. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  -Bungeni, wale wote watakao onekana wanalala, hawapo(kwa visingizio vya vikao), kuipga kura kwa jambo wasilolijua kwa kuwa walikuwa nje,.angalau zaidi ya ara nne..kuadhibiwa!Tunawaadhibu watoto mashuleni tukiwafundisha UTII, si mbaya tukikumbushana.

  - Kiongozi anapohujumu uchumi, afilisiwe...na si kujiuzulu na kuendelea kupokea 80% ya mshahara wa awali akiwa hafanyi lolote.
   
 9. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,739
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  nenda darasani tena ukajifunze nchi nyingine duniani zimepataje. wazo la mtoa mada liko bayana kuwa kama NCHI ni lazima tuwe na mambo tunayo yaheshimu na kuyatekeleza hatua kwa hatu bila kujali ni chama gani kipo madarakani.kwa mfano elimu,elimu itolewayo ni lazima iendane na kasi ya mabadiliko ya dunia. ili kfikia hapo ni lazaima kuwekeza katika elimu say 2% ya gdp.viwanda vya kuboresha thamani mazao,miundombinu,lazima viundiwe sera bora za kuzisimamia na kuziendeleza. SIYO KA SASA KILA RAIS ANAKUJA NA MAMBO YAKE.
   
 10. Ufunguo

  Ufunguo JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli wadau,
  Ebu niambie Tango73, hivi kweli sera zetu za nje ya nchi ni za kimkakati kama za wenzetu?. Wenzetu wanaona mbali sana, kwa mfano, baadhi ya nchi za kimagharibi zinajifanya kutoa misaada mbalimbali kama kusomesha watanzia, kujenga madaraja n.k lakini they know exactly what they are doing, after some years wanakuja na kuomba kuwekeza kwenye sekta za madini kwa fimbo hiyo ya msaada, halafu wanachota trillions of dolars. Halafu kibaya zaidi hawatupi technolojia maana wanajua tukishapata teknolojia basi hatutakuwa tegemezi. Ina maana viongozi wetu hawalioni hilo?. Hata picha tu hawasomi kwa mataifa mengine?
   
 11. Crocozilla

  Crocozilla JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 474
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 60
  You have said all!
   
 12. S

  STIDE JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe mkuu, ila namba 1 na 9 zinapingana!! Nadhani lengo la hoja ya kwanza(1) ni kutaka kupunguza matumizi mabaya ya kodi zetu na kuongeza ufanisi ktk siasa zetu. Lakini ikiwa tutaruhusu namba 9 ifanye kazi, itaharibu kabisa lengo la hoja ya kwanza!!

  Kichwa cha habari kinasema "Mkombozi wa Tanzania huyu hapa" well, hapa unamaana kwamba huu utitili wa vyama ni blaa blaa ukizingatia watanzania njaa sana (wachumia tumbo), wanatusariti wakati tunawalipa, hebu tafakari huyo mgombea binafsi (ambaye atategemea msaada kutoka nje itakuwaje!! Mkuu huoni tutatengeneza Uhamsho nyingi Tz?

  Ndugu yangu, mi napinga sana Mgombea binafsi kwa nchi kama Tz!! Watanzania tu wabinafsi, wanafiki, wachumia matumbo na hatujiamini!!
   
 13. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Tupate FALSAFA KUU, tuifanye kuwa IMANI ya TAIFA, na kila raia afundishwe na hata kushinikizwa kuiishi IMANI hyo!
  Imani hiyo itujengee kwanza UZALENDO/Utaifa utakaozaa Kujali na kuthamini taifa letu(watu, mali, nk.), uzalendo utatujengea pia moyo wa Uwajibikaji na kujituma(KAZI). Imani hiyo pia ituondolee aina yoyote ya UBINAFSI/UMIMI...itufanye TUFIKIRIANE! Tu-share furaha, vikwazo na njia za utatuzi!
  Iwe IMANI above all beliefs we have now!
  TUZO na ADHABU zipimwe kwa IMANI hiyo!
  Wanaafrika wenzangu...KAMWE tusidhani haya mambo yanawezekana kirahisirahisi tu, WATU WENYE AKILI NYINGI WALIKAA CHINI WAKASUGUA BONGO ZAO WAKAPANGA NA KUPANGUA, WAZA NA KUWAZUA "WAKATUFIKISHA HAPA TULIPO LEO" ni HESABU KALI ZILIZOPIGWA! Nasi basi HATUNA BUDI KUKAA CHINI, KUUMIZA VICHWA KATIKA TAFAKARI YA KINGA, TUTEGUE HESABU WALIZOTUFUNGA NAZO NA TUTEGE HESABU ZETU, KIZAZI HADI KIZAZI! Tuna IMANI nyingi sana, na kila imani inakinzana na nyingine, na MAENDELEO hayaletwi na MTU, ila WATU! So, ni lazima TUWE na imani moja kuu itakayoondoa UKINZANI katika siasa, uchumi na tamaduni zetu!
  HUMANITY is more than stable and sustainable Economy, culture anda Politics to Real Development!
  Lets live LOGIC-AFRICAN LOVE!
  Mungu wetu anaita sasa!
   
 14. Ufunguo

  Ufunguo JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [Ndugu yangu, mi napinga sana Mgombea binafsi kwa nchi kama Tz!! Watanzania tu wabinafsi, wanafiki, wachumia matumbo na hatujiamini!![/QUOTE].

  Nakubaliana na hoja yako na sababu ulizozitoa. Wazo langu la msingi ni kwamba kwa sasa inaonekana kuwa ngumu kupata mkombozi wa taifa hili kwa njia ya vyama, kwa kuwa navyo vinafadhiliwa na mafisadi. Nikawaza kwamba kama tutapata Mtanzania atakayekuwa tayari kuifia nchi yake lakini hana chama na hataki influence zozote kutoka kwa watu basi mgombea huyo binafsi tumfadhili sisi watanzania kwa kumpa kula ili asiwe na kigugumizi chochote anapotaka kufanya maamuzi (theoretically speaking).
   
 15. S

  STIDE JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ufunguo

  Nakubaliana na hoja yako na sababu ulizozitoa. Wazo langu la msingi ni kwamba kwa sasa inaonekana kuwa ngumu kupata mkombozi wa taifa hili kwa njia ya vyama, kwa kuwa navyo vinafadhiliwa na mafisadi. Nikawaza kwamba kama tutapata Mtanzania atakayekuwa tayari kuifia nchi yake lakini hana chama na hataki influence zozote kutoka kwa watu basi mgombea huyo binafsi tumfadhili sisi watanzania kwa kumpa kula ili asiwe na kigugumizi chochote anapotaka kufanya maamuzi (theoretically speaking).[/QUOTE]

  Mkuu, mawazo yako ni mazuri sana tena sana lakini si ktk Tz yetu!! Mkuu unamkumbuka Mh. A. Lyatonga Mrema? Mtu huyu alikuwa na msimamo balaa!! Angalia kilichofanyika baada ya hapo!! Pia mkuu nadhani mimi nimeshaathirika si rahisi kunishawishi kumuamini m-Tz (mgombea binafsi)!!

  Jamani haya mambo ya mgombea binafsi tusiyakurupukie tu tutakujashutukia nchi tumewakabidhi Freemasons!!

  Ningekuwa na uwezo ningepiga hata marufuku yeyote kutamka neno MGOMBEA BINAFSI kwa nchi kama Tz!! Wote hao unaosikia kila siku wanapigia chapuo Mgombea binafsi ni kwa ajili ya maslahi binafsi tu!!
   
 16. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Tuing'oe kwanza CCM madarakani ndipo tutakapofanikisha hayo. Otherwise tunatwanga maji kwenye kinu!
   
Loading...