Mkoba: Nitalishtaki HabariLeo kwa kunisingizia; akanusha kusaini kitabu cha mahudhurio

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Rais wa CWT amekanusha kile kilichoripotiwa na gazeti la serikali la Habari Leo kwamba Mwalimu Gratian Mkoba alihudhuria na kusaini kitabu cha mahudhurio Shuleni. Amesema atalishtaki gazeti kwa uzushi na amesema atakuwa wa mwisho kurejea kazini.

Source: Clouds FM Mkoba yuko Live
 
Tangu wa register mgogoro hadi wanagoma ni siku 52!

Walimu waliwahi pata posho kipindi cha Mwinyi mkapa kaja kuzitoa,ana hoji haya ni madai mapya kivipi???
 
Tangu wa register mgogoro hadi wanagoma ni siku 52!

Walimu waliwahi pata posho kipindi cha Mwinyi mkapa kaja kuzitoa,ana hoji haya ni madai mapya kivipi???
 
Wekeni vitu basi kwani kila mtu anasikiliza?
Ansema Mgomo ni halali, umefuata hatua zote za kisheria wao walichagua sheria ya ajira na uhusiano kazini ya 2004 ambayo ni shortcut badala ya ile ya majadiliano ya pamoja katika Utumishi wa Umma yenye mlolongo. Kura za kuunga mkono mgomo zilipigwa kwa siri sawa na katiba ya CWT
 
namsikia anatiririka vilivyo hando anajitahidi kumbana aonekane kakosea lkn sheria inamlinda vizuri tu! Hii kitu iungwe mkono na wafanyakazi wote tz
 
MKOBA ni jembe! TUCTA mpo wapi? waungeni Mkono Walimu hata kwa kauli za hapa na pale. Serikali lazima ifahamu kuwa watumishi wote Tanzania wapo pamoja. MSHIKAMANO DAIMA
 
Eti twende kazini,mgomo ni batili....nosense!
Hata yule asiyeunga mkono mgomo atashindwa kufika kazini coz hadi sasa salary haijaingizwa akountini.......atafika vipi shule!
"NIMELALA ZANGU NYUMBANI"
 
Anasema "Wanaowashawishi wanafunzi kuandamana ni wale waliopo shuleni, wanaojiita Wazalendo"
 
Hongereni sana walimu kwa kufuata sheria...nimemsikiliza Mkoba.... serekali imefanya delaying tactics sana kwenye negotiation na ndio maana wamekwama mahakamani.....
 
magamba hawana sera, zaidi ya uzushi! yaani hichi chama sijui nani alikilaani, laana imewashika! kabla 2015 tutaona na kusikia mengi!
 
Washtaki baba... Wamelifungia Mwanahalisi ili hawa wazidi kupotosha mambo...
 
Walimu waliopo kazini wanajiita wazalendo, hao ndio wahusishwe na kuwashawishi wanafunzi kuandamana maana waliogoma wapo nyumbani.
 
Kuna baadhia ya watu walizaliwa wakiwa wasaliti... walinyonya maziwa yenye usaliti ndio maana wameendelea kwenda shuleni wakati wa mgomo
 
Walimu na wadau wengine wanapiga simu kumpongeza mgomo... Anasema "mgomo huu sio wa Mkoba ni wa Walimu"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom