salisalum
JF-Expert Member
- Oct 27, 2010
- 418
- 136
Hii kama ni kweli basi inatakiwa kuona ni jinsi gani watu hawa walivyo wanafiki na wazandiki! Hii ni kuwachuza wale anaowaongoza....kwanini akasaini ikiwa wamekubaliana kugoma?!
Ina maana, ikiwa serikali itaamua kuchukua hatua; yeye aseme "sikugoma, si mnaona hata kwenye kitabu cha mahudhurio nipo!" Kama ni kweli, basi huyu mzee Ni Kenge Mzee ndani ya msafara wa Mamba Vijana!! Huu ni usaliti wa hali ya juu!
Usaliti ambao walimu wanapaswa kufahamu wazi kwamba, wao wametangulizwa mbele kama ngao! Hakika; kama walimu wangekuwa wanafahamu wanachokifanya, basi wangekutana mapema iwezekanavyo na endapo itabainika ni kweli Mukoba amesaini kitabu cha mahudhurio basi wampige chini bila kuchelewa. Yeye alitangaza wazi kwamba walimu wote wabaki nyumbani; sasa amesaini vipi wakati yupo nyumbani?!
Hofu yangu nyingine ni kwamba, habari hii inaweza isiwe ya kweli....inaweza isiwe kweli kwamba Mukoba amesaini. Lakini kama kweli amesaini, basi anastaili kuondolewa kwenye nafasi yake bila kusubiri!
Siyo ya kweli. Mkoba hafundishi, ni mwajiriwa wa TTU, labda kama amesaini kuingia ofsini kwake. Hizi propaganda zitaisha lini? Walimu shirikianeni kutatua matatizo yetu badala ya kugawanyika.