Mkoani si Rais ataleta maendeleo.....

akili

Member
May 5, 2008
68
0
NINAWASHANGAA wanaojiandaa eti kwenda kupiga kura ya Urais, yaani, rais wa nchi awe nani (siku zote aliye mbali na wao na hajui kinachowazunguka na kuendelea katika mkoa wao mpaka adanganywe na wakuu wake wa mkoa na wilaya na kufanyia kazi habari za uongo badala ya kweli) au mbunge (ambaye keshatangaza kwamba maslahi yake kwanza, na akichia ubunge ndio atafikiria maslahi ya watu wengine) badala ya rais/waziri mkuu wa mkoa wao awe nani ?

BILA ya kuwa na MKUU WA MKOA au GAVANA anayechaguliwa na wananchi wa mkoa husika sahauni Watanzania kapsa kapsa kupata maendeleo mpaka mwisho wa dunia.

Kwa maoni yangu, Uchaguzi Mkuu nchini uahirishwe mpaka tutakapokuwa na Katiba Mpya ambayo pamoja na mambo mengine itakuwa imetambua haki ya wakazi wa kila mkoa kuchagua viongozi wao wote wa mkoa kisiasa ikiwemo Gavana wa Mkoa wao.

Hii ina maana Mkoa wa Kagera unaweza ukawa na Gavana toka CHADEMA; Mkoa wa Kusini Pemba ukawa na Gavana kutoka CUF; mkoa wa kIlimanjaro ukamchagua Ndesamburo kuwa Gavana wake; Mkoa wa Kigoma ukamchagua Ndugu Zitto kuwa Gavana wake naye akitokea CHADEMA au CCJ na kadhalika.

Amkeni Watanzania hamtopata maendeleo na viraka vya pancha vinavyoitwa wakuu wa mikoa na wilaya katika miaka hii. Maana kila Mkoa unastahili kuwa na Gavana na Baraza lake la Mawaziri ambao pamoja na mambo mengine watachangia kuwaamsha wananchi kutowabeba wabunge wasiowawakilisha wananchi ipasavyo katika bunge la taifa;

kuhakikisha kila mkoa unatunza fedha zake katika Benki yake Kuu ya Mkoa na sio kubaki BOT ambako kuna mifuko inayovuja kila siku; kadhalika vijana kupata ujuzi wa kuongoza kuanzia wilayani na mkoani na kuliandaa taifa kupata kizazi bora cha viongoz wa kitaifa toka kwenye mashina na matawi kuanzia sasa.
 
Back
Top Bottom