Mkoani Kagera: Yaliyojiri kwenye Ziara ya Rais Magufuli kwenye Uzinduzi wa Uwanja wa Ndege Bukoba Mjini

Roving Journalist

JF-Expert Member
Apr 18, 2017
474
1,000
Wadau,

Mhe. Rais wetu mpendwa Dr John Magufuli yupo mkoani Kagera kwa ziara ya siku 4.

Akiwa njiani amelazimika kusimama ili aweze kusalimiana na Wananchi wengi waliojitokeza kumsalimia na kumjulisha matatizo yao mbalimbali.

Tutaendelea kuwajuza juu ya kinachojiri kwenye ziara hiyo yenye lengo kuu la kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Karibuni.

UPDATE: Uzinduzi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba

Nawashukuru kwa kuachagua madiwani na wengi kutoka chama cha CCM, hata ambao hawapo CCM naamini watatekeleza ilani ya CCM

Napenda sana kumpongeza Mhe. Kikwete kwa kulianzisha hili na kuhakikisha uwanja huu wa ndege unapatikana. Mwakati Mhe Kikwete anaweka jiwe na msingi mbunge wa hapa alikuwa ni wa CCM ila sasa ni wa chama kingine

Hii ni kwa sababu maendeleo hayana chama, kama maendeleo yana chama kwa ubadilisho mliofanya hapa. Na sisi tungeweza kubadilika

Nampongeza Lwakatare anaweza kuwa wa chama kingine ila moyo wake ni kama wa CCM hivi
Thamani ya uwanja huu ni billion 31.95 na serikali imetoa billion 6, ila huu ni mkopo wa masharti nafuu na tutaulipa. Huwezi kumkopesha mtu asiyelipa. Wametukopesha pia billion ili kupanua bandari ya Dar 225

Uwanja huu una urefu wa Km 1.5 mimi napenda uwanja huu urefushwe Zaidi, na tunaweza tukapanua kuingia majini

Tanzania tuna eneo kubwa lakini haliwezi kuwa eneo la kuchungia mifugo toka nje. Ndio maana tunampango wa kusajili mifugo yetu yote

Mifugo yetu inayoenda nje ya nchi wakiishika huko aifanye chochote kwa mujibu wa sharia huko

Katika kubadili nchi kuna chmagamoto zake, na si kila mtu atazipenda ila matokeo yake mtayaona

Katika watumishi wanaodai billion15.2 kuna watatu na nitawasema hapa. Mmoja anaitwa Jackson Kaswahili anatai billion 7.7626 sehemu ya mishahara yake ameenda likizo na kadhalika anatoka Ukerewe, Utumishi wamekagua na kukuta hadai kitu. Mwingine ni Mwachano Ramadhani Msingwa anatoka Bagamoyo alisema anadai billion 1.754 Utumishi wamepitisha Wizara ilipe, ukaguzi ulivyofanyika ikakutwa anadai million 2 tu. Mwingine anatoka Mafya alikuwa amekaimu kwa nafasi hivyo anasema lazima kuna hela analipwa huyu anaitwa Gidion Zakayo anadai million 104

Utumishi waliopitisha maombi haya vyombo vya dola vianze kuwashughulikia

Rais: Mkugenzi wa Manispaa tuambie tumeleta kiasi gani hapa cha bajeti ya Manipaa ya Bukoba?

Mkurugenzi: Bajeti ya Manispaa ni Million 33, na mapato ya serikali kuu ni pamoja na sera hizi za elimu bure na fedha zilifika kwa wakati. Na fedha hizo zinakuja kwa wakati unaotakiwa

Rais: Fedha za road fund ni kiasi gani maana huwa zinapotea potea tu. Huzikimbuki.

Mkurugezi: Labda aje muweka hazina, ila siwezi kusema maana naogopa kusema uongo nina sehemu nyingi nashughulikia.

Rais: Huwezi kunijibu hivyo mimi. Nani anakumbuka fenda za barabara ni kiasi gani? Ninaweza kuteuwa Mkugenzi mpya leo

Mwenyekiti wa halmashauri: Millioni 500 tulizihamisha kwenda mfuko wa dharura kwa ajili ya barabara

Nilipokuja kuwaomba kura nilisema lazima nitanunua hela, fedha nitatoa wapi. Ni kwa mafisadi na teyari nimeshatenga billion 35 zipo pembeni

Uchumi haujengwi bila kuwasaidia wajenga uchumi

Meli ya Victoria na MV Butyama nazo tunazikarabati, nataka meli ziwe zinapishana hapa. Ninabana huku kwa mafisadi nalegeza kwa wananchi masikini. Nilichaguliwa na wananchi masikini

Najua Halmashauri hii ni ya CHADEMA, ila mimi ni rahisi wa wananchi, Mstahiki Meya nataka mkakae mkulima yeyote atatozwa kodi akizidi tani moja. Atakayetokea anadai mkulima ushuru na amebeba chini ya tani moja nataka vyombo vya dola mumuweke ndani

Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote mkasimamie hapa

Nataka wananchi masikini wakapumue

Ukitaka kuvua samaki wadogo tengeneza bwawa lako vua hata mayai. Ila samaki waliopo ziwani ni waserikali. Samaki mmoja nataga mayai million 1.5 ukimuua huyu unauwa na mayai.

Huwezi ukawa waziri wa biashara, Viwanda na Uwekezaji halafu huna hata kiwanda huku kwenu, leta viwanda huku nako ni Tanzania mimi sitasema umejipendelea

Weka hata kiwanda cha Lubisi

Niwahakikishie wafanyakazi wa Kagera na Tanzania nzima, mwisho wa mwezi huu tutaanza kulipa stahiki zao hata kama zilisimama kwa miaka 50. Tumetenga billion 159

Tunatengeneza mswada na tutapeleka Bungeni, badala ya kuwana utitiri wa Mifuko ya wafanya kazi tutakuwa nayo miwili tu. Mfuko wa wafanya kazi wa serikali na mwingine wa mfuko wa fanya kazi wa sekta binafsi

Na sasa tumetangaza nafasi 52,000, Kuna feki chache zimebaki na zitaondoka. Na mimi sitaki nipendwe na fanyakazi feki kwa sababu kwanza hawapo na hawakunipigia kura. Hewa ni hewa tu

Tumenunua ndege sita mpya, lakini mabeberu wa ajabu ajabu wamefungua kesi, walidhani tutawapa fedha. Wengine wamefungua Uingereza.

Kuna ndege tuliikodi kipindi cha akina Mataka ilipofika hapa ikaenda service wao wakasema wanatudai tu. Wakaenda kutufungulia kesi Uingereza wanatudai

Nimemuandikia barua waziri wa Canada kuwa hawawezi kushika ndege yetu wakati tulitaka iwe inakuja Bukoba

Kesho kutwa nitakuwa Uganda kuzindua ujenzi wa bomba la mafuta na litapita hapa. Naomba mjishughulishe kupata ajira katika ujenzi huo, mama Lishe na vijana. Watu wengi walitaka hili bomba lipite mahali kwao tumeshinda maana Mungu aliona lipite huku

Watakao ajiriwa tu ni Zaidi ya watu 15,000

Tumetoa billion 483 kwenye mikopo ya wanafunzi na Billioni 147 zimeshatolewa

Uwanja wa ndege upanuliwe na Waziri leta Consultants na pesa zitakazopungua nitaongeza serikali ni tajiri

Hii ni wiaka miwili bado miaka mitatu, Wenzetu watakuja kutuuliza tulifanya nini, tutawaeleza tunapanua hata stend ile pale panapojaa maji

Viongozi wenzangu wa Vyama vingine Tupendane hii serikali ni ya CCM hakuna mwenye serikali nyingine mimi sindio Mwenyekiti wa CCM na ndio rais, Ni serikali ya CCM

Kila kiongozi kwa wiki moja kwa siku moja, apange kukutana na wananchi na kusikiliza kero zao
 

Attachments

 • File size
  116.4 KB
  Views
  164
 • File size
  64.8 KB
  Views
  147

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
13,106
2,000
Wanajitokeza kushangaa haya
1.kwanini amelikana jina la kato na kuwakimbia
2.kwanini ajenge chato international airport badala ya omukajunguti
3. Kwanini amewadanganya meli,
4.Million 50 za kila kijiji hawajuhi kama zitakuja
5. Kamtelekeza na kuisahau familia ya mzee machalila, na kishao karagwe

,6. Dolla imefika 2600 leo

Hivyo kujitokeza kwa wingi haimaanishi.wanakukubali wanakuja kuangalia kama una aibu usoni

Kwanini Chato International Airport na si Omukajunguti international Airport? Kagera inaonewa sana
Cc

Pascal Mayalla
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,786
2,000
Na wakati wa majanga awe anakwenda, majanga kama mafuriko na tetemeko la ardhi awe anawatembelea kwa wakati na kutoa misaada
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
36,837
2,000
Wadau,

Mhe. Rais wetu mpendwa na kiboko ya mafisadi Dr John Magufuli yupo mkoani Kagera kwa ziara ya siku 4. Akiwa njiani amelazimika kusimama ili aweze kusalimiana na Wananchi wengi waliojitokeza kumsalimia na kumjulisha matatizo yao mbalimbali.

Tutaendelea kuwajuza juu ya kinachojiri kwenye ziara hiyo yenye lengo kuu la kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Karibuni.
Ni matumaini yangu makubwa kuwa ' Mjane ' atakayepangwa leo hapo Kagera hatokosea ' mahesabu ' yake kama yule wa wiki iliyopita kule Mwanza ili ' Sinema ' isiharibike kama siyo kushtukiwa na wenye akili zao timamu na zilizotukuka kabisa.
 

wasaa9

JF-Expert Member
Jun 9, 2017
534
250
Wadau,

Mhe. Rais wetu mpendwa na kiboko ya mafisadi Dr John Magufuli yupo mkoani Kagera kwa ziara ya siku 4. Akiwa njiani amelazimika kusimama ili aweze kusalimiana na Wananchi wengi waliojitokeza kumsalimia na kumjulisha matatizo yao mbalimbali.

Tutaendelea kuwajuza juu ya kinachojiri kwenye ziara hiyo yenye lengo kuu la kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Karibuni.
We ndo karbu kutujuza
 

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
11,213
2,000
Nasikia huko kwenye shule ya msingi ya Migango mwalimu mkuu amemtandika bakora mwalimu wa kawaida kwa kuiba sahani tano na nusu kilo ya sukari, ambavo vingetumika kwenye mahafali ya darasa la saba.

Hali ni ngumu sana.
 

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
755
1,000
Habari wakuu,

Kumekuwa na tabia ya wabunge wa upinzani hasa chama fulani kuwashambulia wabunge wa upinzani wanaohudhuria mikutano ya Rais Magufuli kwa kuwaita wasaliti. Wapinzani hao walimshambulia vikali mbunge wa Kigoma baada ya kuhudhuria mkutano wa Rais jimboni kwake ila kutokana na ukomavu wa Zitto kabwe akawapiga kijembe kwa kusema Zitto Kabwe: Kuna kachama kana mdomo mdomo maana K/njaro wana maendeleo. Hamkuchagua mbunge zwazwa.

Jamaa walitoa povu balaa sana.

Nasubiria kuuona msimamo wa wabunge wa upinzani wakimuita Lwakatare msaliti na kumtenga kabisa.
 

msafwa93

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,592
2,000
Wanajitokeza kushangaa haya
1.kwanini amelikana jina la kato na kuwakimbia
2.kwanini ajenge chato international airport badala ya omukajunguti
3. Kwanini amewadanganya meli,
4.Million 50 za kila kijiji hawajuhi kama zitakuja
5. Kamtelekeza na kuisahau familia ya mzee machalila, na kishao karagwe

,6. Dolla imefika 2600 leo

Hivyo kujitokeza kwa wingi haimaanishi.wanakukubali wanakuja kuangalia kama una aibu usoni

Kwanini Chato International Airport na si Omukajunguti international Airport? Kagera inaonewa sana
Cc

Pascal Mayalla
Machalila na kishao ndiyo nani.?na kawatekeleza kivipi.?

Hii ni forum sio mnaandika kama kila mtu yupo kichwani mwako
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom