Mkoa wa Tabora kugawanywa na kuwa mikoa miwili

Mapengo 17

R I P
Mar 28, 2014
1,232
609
Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora imependekeza kuugawa Mkoa wa Tabora ugawanywe na kuwa mikoa miwili ,kutokana na ukubwa kuliko yote nchini,kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi kwa urahisi na ufanisi zaidi.

Akisoma mapendekezo hayo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora , Bibi Kudra Mwinimvua amesema, Mkoa wa Tabora una eneo la Kilomita za mraba Elfu-75 na 865, ukiwa na wakazi milioni- 2, laki 2 Elfu-91 na 623.

Unapendekezwa kugawanywa katika mikoa ya Tabora ukiwa na wilaya saba na mkoa wa Nzega ukiwa na wilaya nne.
 
  • Thanks
Reactions: cmp
kidogo watu wa Tabora wataelimika na kuacha kuikumbatia CCM miaka nenda rudi pasipo kupelekewa huduma mhimu???
 
Mh, hapo sioni cha umuhimu,ukiugawa sawa lakin jua hata Urambo nayo watadai iwe mkoa kwahio utakua mwendo wa mikoa km 90 mkoa yanini
 
Hawa ndiio viongozi tulio nao. Waliopachikwa kwenye madaraka kwa misingi isiyo na tija kwa taifa, hawawezi kuwa na mawazo yenye tija kwa taifa.

Kuongeza mzigo kwa serikali ndiyo kuleta maendeleo ya watu? Kama tungekuwa na serikali ambayo proactively iko responsive, kuna haja gani ya kuwaza kutakuwa na que ue ya watu kurundikana ofisi ya mkoa ama kusafiri mwendo mrefu kufuata huduma makao makuu ya mkoa? Kwa nini huduma zote za watu zirundikane katika ofsi ya wakuu wa mikoa kiasi cha kuona umbali wa mtu na ofisi ya mkuu wa mkoa ndio umbali wa mtu na maendeleo yake?

Uwepo wa ofisi za wakuu wamikoa katika makazi ya watu kuna automate vipi maendeleo yao?

Mtazamo huu ndio uliom cost Sadam Hussein.

Hatutaki ma mikoa ya kisiasa. Kama hana ubunifu wa kufikisha huduma muhimu za jamii na mendeleo katika maeneo ya watu, aachie ngazi waje viongozi wenye maono sahihi.

BtW, kazi ya mkuu wamkoa ni nini kwanza?
 
Mkoa wenyewe hauna changamoto kila kitu ndiyo baba ccm. Angalia mikoa yote inayo ongozwa na wanawake haina changamoto tofauti na umasikini uliokithiri. Waugawe ili wachangamke.
 
Pale butiama ni wilaya. Hakuna hata choo cha mkurugenzi. Vyote walivyokuta ni mali ya kijiji. Hizi wilaya na mikoa kuanzishwa kwa sifa tu ni janga.
 
Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora imependekeza kuugawa Mkoa wa Tabora ugawanywe na kuwa mikoa miwili ,kutokana na ukubwa kuliko yote nchini,kwa lengo la kutoa hudum a kwa wananchi kwa urahisi na ufanisi zaidi.

Akisoma mapendekezo hayo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora , Bibi Kudra Mwinimvua amesema, Mkoa wa Tabora una eneo la Kilomita za mraba Elfu-75 na 865, ukiwa na wakazi milioni- 2, laki 2 Elfu-91 na 623.

Unapendekezwa kugawanywa katika mikoa ya Tabora ukiwa na wilaya saba na mkoa wa Nzega ukiwa na wilaya nne.

we dont need more regions, we need something different

Kazi zinawashinda, wanaishia kutugawagawa kama chapati

Its a system failure tu!!!
 
Hivi kuna improvement kwenye maisha ya wananchi sehemu ambazo wamegawa mikoa na wilaya? mwenye mfano atusaidie hapa.

Kitu cha uhakika wakigawa mikoa na wilaya japo si la mara zote, ni watu fulani kunufaika kwa tenda za ujenzi wa makao makuu ya wilya au mkoa husika. Guest House au Lodge za waheshimiwa kupata biashara ya uhakika wakati wilaya au mkoa unaanzishwa sehemu fulani ambako tayari wametegesha vitu vyao.

Hizo hela za wilaya au mkoa mpya wakipeleka kwenye huduma za afya au mashule katika maeneo hayo itakuwa bora zaidi.
 
Huduma za jamiii jamani ziwafikie wanachi naungana sekretariet ya mkoa kwa mapendokezo yao kuugawa mkoa wa tabora ni mkoa mkubwa sana.wewe ambae unabisha bisheni kwa hoja jamani na so kujibu hovyo kama hamjisikii kuchangia mada
Ya msingi kama hiyo ni afadhali ukalale tu
 
Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora imependekeza kuugawa Mkoa wa Tabora ugawanywe na kuwa mikoa miwili ,kutokana na ukubwa kuliko yote nchini,kwa lengo la kutoa hudum a kwa wananchi kwa urahisi na ufanisi zaidi.

Akisoma mapendekezo hayo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora , Bibi Kudra Mwinimvua amesema, Mkoa wa Tabora una eneo la Kilomita za mraba Elfu-75 na 865, ukiwa na wakazi milioni- 2, laki 2 Elfu-91 na 623.

Unapendekezwa kugawanywa katika mikoa ya Tabora ukiwa na wilaya saba na mkoa wa Nzega ukiwa na wilaya nne.
hahaha!! eti "kutokana na ukubwa kuliko yote nchini". kwa hiyo wakishafanya hivyo na baadae ikaonekana mkoa fulani ni "mkubwa kuliko yote nchini", watagawa tena!!? kisha wakaona mwingine ni "mkubwa kuliko yote nchini", watagawa tena, na tena, na tena, mpaka mikoa yote ilingane ukubwa!!!
 
Back
Top Bottom