Mkoa wa Tabora hakuna mgao wa umeme

KELVIN GASPER

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,066
454
Takriban siku ya tatu leo tarehe 29/09/2011 mkoa wa tabora hakuna mgao wa umeme. Hii inawezekana ni moja kati ya kampeni danganya toto za ccm za kuwasahaulisha wana wa tabora mgao wa umeme ili ccm ipigiwe kura katika uchaguzi jimboni igunga. Wakuu hakuna kudanganyika mpaka kieleweke si mnajua tanesco wameshindwa kesi kodi zetu watalipwa dowans muda si mrefu.
 
Uchaguzi ukipita watawakatia wiki nne mfululizo. Hawana aibu, huo umeme wameutoa wapi? CCM kwa rushwa kweli nawaaminia. Wameshindikana!
 
hata mimi nimejiuliza vipi tena,mgao umeisha nini? Nazani hizi ni cheap political tactics za magamba.nahisi baada ya uchaguzi mgao utakuwa mkali zaidi kufidia hizo siku 4.
 
hata mimi nimejiuliza vipi tena,mgao umeisha nini? Nazani hizi ni cheap political tactics za magamba.nahisi baada ya uchaguzi mgao utakuwa mkali zaidi kufidia hizo siku 4.

Mwana nimekupata. Au ni kwa kuwa serikali imehamia igunga?
 
Dah kweli kaka npo nzega now kwa wiki nzima sasa sijaona umeme ukikatika kwa zaidi ya masaa mawili!
Taadhali: ukirudi n mgao juu ya mgao!
 
Nimefurahia sana.Leo ni siku ya 3 mfululizo nafanya kazi bila kuogopa mgao wa umeme.Kweli TABORA raha jaman.naomba uchaguzi usifike haraka ili tufaid umeme masaa 24.
 
mie nilikaa tabora mwezi june nahisi mgao wa huko hauna makali kama dar sijui kwa nini?
 
ngoja tucheki kama igunga wamekomaa au bado ni makinda ya ndege.
 
hehehehe mnachekesha kweli
hamuijui ccm????????????? sasa nawaambia
wakati wanachakachua kura watawazimia umeme
jazeni kandili zenu mafuta maana
hamjui siku wala saa ccm watakapowakatia umeme
huku segerea jamaa alituzimia umeme
kipindi cha kuhesabu kura na mpaka alipomaliza
shughuli yake ya ubakaji wa demokrasia ndo
akaurudisha,nawashangaa ninyi mnaokenyua
meno yote 32 ya mtu mzima !!!!!!!
labda ninyi wageni wa nji hii
lazma watawaumiza tu
 
Back
Top Bottom