Mkoa wa Njombe umetajwa kuongoza kuwa na asilimia 11.4 ya watu wanaishi na virusi vya UKIMWI

Hivi ni kwa nini Njombe inaongeza kwa kuwa na 11.4% ya watu waishio na UKIMWI? Kwani nijuavyo Njombe ni moja ya Mikoa yenye neema hivyo hata umaskini si kihivyo.
Baridi mkuu na wagaeni wengi pale
 
Njombe barid inawaponza.. Na vile hawajui kukataaga aiseee watakufa km kuku wenye kideri
 
Miongoni mwa sababu kule Njombe ni kiwango kidogo cha tohara kwa wanaume. Lakini pia mtungi, wale watu wanapiga mtungi hatari sana, ingawa baridi nayo yachangia.
 
Takwimu za mwisho zilionesha Njombe, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Tabora na Dar zinashika chati za juu kimaambukizi, hali ikoje kwa sasa, kuhusu mikoa gani inayoongoza?
 
huwa najiuliza sana WHY NJOMBE kila mwaka..
Tatizo ni elimu?
tatizo ni baridi?
tatizo ni mila na desturi za wakazi wake?
KWANINI KUSIFANYIKE KAMPENI MAALUM
 
Hizo Takwimu ni za uongo.
Uchukuaji wa Sample kwa mkoa ni mobovu sana.
 
Ndo hali halisi
 

Attachments

  • IMG-20171201-WA0042.jpg
    IMG-20171201-WA0042.jpg
    64 KB · Views: 80
Miongoni mwa sababu kule Njombe ni kiwango kidogo cha tohara kwa wanaume. Lakini pia mtungi, wale watu wanapiga mtungi hatari sana, ingawa baridi nayo yachangia.
Ukizungumzia mitungi hakuna wanaokunywa tungi kama moshi na arusha na kwa baridi moshi arusha ipo ya kufa mkuu sema hawajui kukataa alafu.magomvi mengi sana hawatahiriwi hawa viumbe
 
Hii mikoa ya nyanda za juu pombe hasa ulanzi ni kisababishi kikubwa. Watu wakilewa ni kubanduana tu.
 
Kama baridi ndio chanzo cha ukimwi ilitakiwa nchi za ulaya ziongoze.

Dar kuna joto ila nimiongoni mwa mikoa yenyeemaambukizi ya juu
 
Tatizo la UKIMWI tz ni kubwa kuliko linavyoelezwa ki takwimu.

Sidhani kama kuna familia ambayo jamaa zao hawana tatizo hili.

Athari za Ngoma ni kubwa mno ki uchumi, kijamii na kiafya

Issue sio ARV zinatolewa bure, ukiwa na ngoma unapatwa na magonjwa nyemelezi mengi sana amabayo dawa zake nyingi hazipatikani kwenye hospitali zetu, hivyo kulazimika kuzinunua Pharmacy, jambo ambalo linahitaji pesa

Ugonjwa huu auui ghafla, hivyo ukiupata unavyonza uchumi wako wote na kuacha umasikini wa kutupwa kwa familia yako.

Nimeona wengi wakitelekezwa, na kunyanyapaliwa na Ndg kutokana na gharama za matibabu na maisha Kwa ujumla.


Nitoe wito kwa kila mmoja wetu kujitahidi kujikinga na ugonjwa huu.


Acha faraja zote na kutiwa moyo ngoma ni Janga kubwa, kwako, kijamii na kitaifa.
 
Back
Top Bottom