Mkoa wa Kwale nchini Kenya kuanza kuuza majani ya baharini nchi za ulaya, je tuna jifunza nini kutoka kwao.

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Nchi ya Kenya wanajitahidi sana kufikiria na kupanga kipi wanachoweza kuuza katika nchi za ulaya na kwingineko,

Kikundi cha C-Weed Company and women members of the Kibuyuni Seaweed Farmers group ambao watakuwa wana safirisha tani 30-60 ya mazao hayo ya baharini kila mwezi kwenda nhci za Ufaransa, Marekani, Ubeljiji na kwenye masoko mengine ya Ulaya na kwingineko sasa serikali ya mtaa ya Mkoa wa Kwale imewaunga mkono na kukubali kuwasaidia maana imekuwa ni sehem ya utekelezaji wa sera ya Blue Economy ambayo walikubali iwe mkakati wa kukuza uchumi wa Kenya, hii ni hatua kubwa sana kwa wananchi na serikali yao katika utekelezaji wa sera ya blue economy, hii itaongeza ajira na kuongeza kipato kwa mmoja mmoja.

Wameanza na kusafirisha tani 100, usafirishaji huo umezinduliwa na moja wa wakurugenzi wa Wizara ya biashara na utalii na wengine walio shiriki ni pamoja na mwakilishi wa shirika la Food and Agriculture Organisation (FAO), Kenya Marine and Fisheries Research Institute (KEMFRI), mzigo huo ulipakiwa kwenye lory katika kijiji cha kibuyuni huko Kwale. Lengo ni kusafirisha tani 100 kila mwaka hii imekuwa fursa kubwa sana kwao.

Nimejifunza kwamba lazima sisi watanzania tujifunze namna wengine wanavyokuza uchumi wao kwa kukuza sera mbalimbali ambazo zitalenga maeneo mengi yakiwemo ya kibiashara maana biashara ipo katika maeneo mengi sana. Tuache kuweka siasa au kuipa siasa kipau mbele tufikirie uchumi wa nchi hii na tupange tunavyotaka uwe.

16114410_10208401044248213_9184695350480460919_n.jpg
51308545_545078819235371_3048593857152286720_n.jpg
51677761_545078869235366_7572042280744255488_n.jpg
 
Hicho kilimo kipo Sana Zenji, maeneo ya Bweleo na Fumba. Wanauita mwani
 
Wananchi wenzetu huku wamekalia kueneza chuki na husuda baina yetu na wanaAfrika mashariki tu
 
Back
Top Bottom