Mkoa wa Kinondoni kanda ya Dar es salaam CHADEMA watoa tamko kali sana kuhusu Lema kuwa magereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkoa wa Kinondoni kanda ya Dar es salaam CHADEMA watoa tamko kali sana kuhusu Lema kuwa magereza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Henry Kilewo, Nov 1, 2011.

 1. Henry Kilewo

  Henry Kilewo Verified User

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 889
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Mkoa wa Kinondoni kanda maalum ya Dar es salaam umetoa tamko kali sana leo walipo kuwa wakiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi za chama hicho zilizopo maeneo ya mwananyamala ujiji.

  Tamko hili hapa.  MKOA WA KINONDONI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM

  Tamko la katibu wa mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum ya Dar es salaam

  [​IMG]

  Ndugu zangu wanahabari

  Nimewaita hapa leo kwa lengo la kuwapa watanzania msimamamo wangu na wa chama ngazi ya mkoa kuhusu tukio la kukamatwa na kupelekwa magereza kwa Mhe. Godbless Lema Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini.

  Imekuwa ikizoeleka kwa muda mrefu sasa kwamba waheshimiwa wabunge wa CHADEMA na wale wanaaotokana na vyama vya upinzani wamekuwa wakinyanyaswa sana kwa lengo la kuwafanya wajute kuingia katika siasa za upinzani Tanzania.

  Hii kwa CHADEMA haitokei tu kwa waheshimiwa wabunge bali hata kwa viongozi wa ngazi zote. Inaonekana kuwa sasa serikali ya Chama Cha Mapinduzi imeamua kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kuwatesa kwa siri na kwa wazi wale wote wanaoipinga siasa kandamizi na zisizowalazimisha watawala kuwajibika kwa wananchi.

  Mkakati huu umetungwa na CCM, unasimamiwa na usalama wa taifa na unatekelezwa na jeshi la polisi. Kwa hakika hatuhoji tena kwamba jeshi la polisi ni kitengo cha kusimamia maamuzi na maelekezo ya CCM badala ya kulinda raia na mali zao.

  Mheshimiwa Godbless kama mbunge wa wananchi wa jimbo la Arusha Mjini amekuwa akifuatwafuatwa na jeshi la polisi kila mara na kufanyiwa vitendo vingi vya udhalilishaji na unyanyasaji hasa kwa kupitia OCD wa Arusha Mjini Zuberi.
  Mathalani wiki iliyopita siku ya ijumaa tarehe 28/10/2011 Mhe. Godbless lema akitoka mahakamani alisindikizwa na wananchi wake kutoka mahakamani hadi ofisini kwake. Wafuasi wake walipomfikisha ofisini waliondoka na kurejea makwao. Huko ofisini aliwakuta wananchi wakimsubiri ili awahudumie kama mbunge wajimbo lao. Wakati akiongea na wananchi ghafla polisi walifika na kuwakamata wananchi wote waliokuja kuomba usikivu wa mbunge na kuwapeleka kituo kikuu cha polisi.

  Mbunge Lema alipokwenda kituo cha polisi kwa lengo la kuwawekea dhamana naye aliwekwa chini ya ulinzi kwamba eti amefanya maandamano bila kibali.

  Tunahoji: Ni maandamano yapi hayo ambayo Lema aliyafanya na wananchi wake akiwa angali ofisini kwake? Je maandamano wanayoyazungumzia ni kuondoka na wananchi mahakamani hadi ofisini kwake? Je kama kuondoka kwake na wafuasi wake mahakamani ni kosa kisheria; Je kwa Mhe Ole Sendeka alipokuwa akitoka mahakamani, alikuwa akiondoka na kundi kubwa la wafuasi wake na kusindikizwa na OCD huyu huyu? Vile vile Mwenyekiti wa UV-CCM mkoa wa Arusha amekuwa akienda kituo kikuu cha polisi akisidikizwa na kundi kubwa la wafuasi wake wa CCM. Polisi hawakuwahi kuwakamata wala kuwaonya. Sasa haya yote yalikuwa maandamano ama matembezi ya hisani? Maana Arusha kuna msiba mkubwa wa CCM kukataliwa na wananchi.

  Kwa hakika tukio la kukamatwa kwa Mhe Lema, kupelekwa mahakamani na hatima ye kupelekwa gerezani ni ushahidi wa kutosha kwamba jeshi la polisi sasa linakamilisha sehemu kubwa wa wajibu wake wa kuibaka demokrasia.

  Hata hivyo tunalitaka jeshi la polisi na serikali ya CCM wajue kwamba kitendo cha kumpeleka Lema magereza ni ushindi tosha katika harakati za ukombozi wa taifa hili. Maana hakuna silaha yoyote duniani ama jeshi la polisi popote pale duniani ambavyo viliweza kushinda vita dhidi ya ukweli, haki na uwazi.

  Ndugu zangu watanzania
  Tunawaunga mkono wana Arusha kwa kumpata mbunge ambaye anayatetea maslahi yao kwa mzigo hata pale inapobidi kwenda gerezani kwa ajili ya watu wake na hata ikibidi kifo anaweza kusimamia hilo. Alisema Martin Luther King Jr. 1963 "A man who wont die for something is not fit to live" na akaendelea kusisitiza "Nobody can give you freedom, nobody can give you justice or right or anything. You take it!" (STAND UP; STAND UP 4, UR RIGHT) Hayo yalikuwa maono ya bob marley ambayo aliyaona mwaka wa 1973,baada ya kuwa amekaa katika mto mmoja huko jamaica akaona samaki wanapita katika maji lakini samaki wakubwa wakawa wanawaonea samaki wadogo,hivyo akaona hata hapa duniani hata wa2 walio juu wanawaonea watu wa hali ya chini.

  Kwa watu wanaopinga ama kukejeli maamuzi ya Godbless lema kukataa dhamana, Wathubutu kufanya ziara huko Mahospitalini wavae sura za uhasilia wa kibinadamu wakaone watu waliokuwa kama wao jinsi wanavyotaabika kwa kukosa matibabu ile hali ni walipa kodi wa taifa hili. Kwanini Godbless asiende jela wakati anasimamia mambo ya msingi na hayatekelezwi, tukiandamana tunaonekana tunavunja sheria ni afadhali kwenda sehemu wanayodhani tunaogopa kuliko kukaa kimya kumbe hatuogopi. Mungu yupo upande wetu na tunaelekea kushinda unyanyaswaji huu.

  Kama ambavyo alivyowahi kusema Martin Luther king jr, ndivyo tunavyo wahakikishia wana wa Arusha, we will work together; we will stand up together, we will go to jail together, until justice runs down like water. maana mateso tunayoyapata ni makubwa kuliko huko jehanam tusipopajua.

  Kwa kuonyesha tuko pamoja katika harakati hizi za kudai demokrasia ya kweli tunampogeza Godbless lema mbunge wa Arusha mjini kwa kupeleka ujumbe kwa watawala wanaodhani wanaweza kutumia magereza kama sehemu ya vitisho kurudisha harakati zozote zile nyuma.

  Ujumbe huu uwafikie watawala yakuwa jela sisehemu ya kumtishia mtu yeyote Yule mwenye akili timamu, mpenda haki bali ni sehemu ya kawaida ambapo binadamu yeyote Yule anaweza kwenda.

  ASANTENI ASANTENI NA MUNGU AWABARIKI WATANZANIA WENZANGU!


  Henry J Kilewo
  KATIBU (M) Kanda Maalum
  01/11/2011
  maoni yangu:

  Maoni yangu haya matamko siyo ya kupuuzia hata kidongo, lazima tuwaunge mkono hawa makanda.
   
 2. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  yah ni kweli hawa watu ni wa kuungwa mkono kwa kweli
   
 3. bmx

  bmx Member

  #3
  Nov 1, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  peoples power inakuja hawawezi kuizuia,
   
 4. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mwanza, musoma,Tarime,Iringa,Mbeya,Shinyanga,Kigoma,Kagera,Igunga,Kilimanjaro,Rukwa, Bavicha mpo?
   
 5. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kaazi kwelikweli!
   
 6. Kisima

  Kisima JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 3,768
  Likes Received: 2,227
  Trophy Points: 280
  Aluta contınua!
   
 7. A

  ACTIVISTA Member

  #7
  Nov 1, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  lema kaonyesha mfano.... tumuunge moono vijana..... wote tunaoona tunaonewa waziwazi tumunge mkono jamaaa...... nakumbuka Tunisia mwaznoni mwa mwaka kuna kijana alijichoma moto Hadharaniikiwailikuwa namna ya kufikisha ujumbe juu ya Tatizo la ajira na ajira za upendeleo...jamii ilihamasika na mapinduzi tumeyaona ....tujuitoe muhanga namna hii ukombozi tutaupata
   
 8. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,997
  Likes Received: 2,653
  Trophy Points: 280
  Mheshimiwa Lema ameenda kuwapa elimu ya uraia pamoja na kuzijua haki zao za msingi wafungwa, namuunga mkono kwa ujasiri aliouonyesha mheshimiwa Lema CCM wao mawazo yao wanadhani labda kuwapeleka Jela wana CDM ndio watafanikiwa,hapo ndipo wanapokoleza moto kwa Petrol bila kujua OLE WAO WANAOJIFANYA WABABE KWA SASA,wajiandae kuwa wanyonge baadae.
   
 9. RUMANYIKA

  RUMANYIKA JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 315
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani tuambiane kama safari ya kukutana A-twn tayari maana naona strategy zote zipo kwenye utekerezaji.
   
 10. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kazi ipo.
   
 11. L

  Lua JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2011
  Joined: May 19, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  tuache ujasili na harakati za kwy mitandao, kama vp tuingie barabarani. lema ameshaanza.
   
 12. 2

  21DEC2012 Senior Member

  #12
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  MUNGU atuokoe bomu hili wanalolitengeneza.Hawataweza kuirudisha imani ya wananchi juu ya hiyo serikali yao kama wataendelea na tabia hii.

  Nchi ina matatizo mengi kama ukame,ukosefu wa maji kwenye maeneo mengi,uhaba wa chakula,mfumuko wa bei,ufisadi ,ajali za kila siku,bidhaa mbovu(Counterfeit Product) kutoka nje ya nchi,madawa feki, huduma mbovu za afya,elimu,ukosefu wa ajira,umeme migogoro ya ardhi,ujambazi,mauaji ya albino,ukosefu wa miundo mbinu kama barabara na mengine mengi mfano hayo yanayozunguka maeneo unayofanyia kazi au kuishi.
  Muda na nguvu zinazotumika kuwafanyia ukatili viongozi wa wananchi (CHADEMA) na wapinzani kwa ujumla ni bora wangezitumia kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayotukabili kama taifa.

  Hii itakuwa kiama kwa nchi.Mwl Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema ''Mkiendeleza tabia hizi za kuwabagua kwa sababu wao sio wenzenu(adui zenu),wakishajitega mtaendelea kubaguana wenyewe kwa wenyewe'' Haya yameshaanza kujitokeza;kuwekeana sumu reffer kauli ya J Kikwete ''Hatuaminiani,Hauwezi hata kuacha glass ya maji ya kunywa ukayakuta salama'' yuko wapi Mwakyembe na Mwandosya,kuvuana MAGAMBA, uadui usiokwisha,fitina za kila aina Ole Millya v/s Ole Sendeka.

  Vijana lazima tulikomboe taifa letu bila kujali itikadi.Huo ni mpango wa mafisadi kutugawa ili waendelee kuneemeka.Wakishatuibia rasilimali zote wataondoka watatuachia nchi yetu ukiwa haina chochote.si mnasikia na kuona kila siku wanashutumiana kwamba mgombea fulani si rai wa nchi hii na sasa wanataka urai wa NCHI MBILI ili iwe raisi kwao kutoroka.
  Vijana,wazee,watoto tuamke...tutetee TAIFA letu hatuna pa kukimbilia.Tusiwaachie hao wanyang'anyi TAIFA letu.Lets fight for our freedom.
  Lema na Makamanda wengine wameshatuonesha njia,sasa ni muda wa kamua.Tunalipenda TAIFA letu au hatutaki liendelee kuwepo.
  viva CHADEMA.
   
 13. MANI

  MANI Platinum Member

  #13
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  "A man who wont die for something is not fit to live" na akaendelea kusisitiza "Nobody can give you freedom, nobody can give you justice or right or anything. You take it!"

  Maneno murua hayo
   
 14. U

  Uyole12 JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 586
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  mie kesho naingia barabarani nipo dodoma nimechoka huu uonevu.
   
 15. U

  Uyole12 JF-Expert Member

  #15
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 586
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hivi jamani naweza pata wapi mabom hi tz hata la kujitoa muhanga hakuna haja ya kuishi wakati naona kuna wa2 hawatendi haki.
   
 16. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #16
  Nov 1, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Unaona sasa wanatengeneza TZSHAABAB, Police msituleteeni balaa hapa, kuweni na busara.
   
 17. n

  never JF-Expert Member

  #17
  Nov 1, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Namtakia maisha marefu huyu kamanda maana ni miongoni mwavijana wa chadema wa chache wanaojitolea kwa jambo lolote lile, hongera lema, hongera arusha, hongera kilewo, hongera chadema.
   
 18. T

  Topical JF-Expert Member

  #18
  Nov 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Akichoka kukaa huko atatoka mwenyewe..

  Salmin aliwahi kumuweka ndani (Duni Haji) akaombwa sana kwasababu jamaa ni ndugu

  Salmin aliwaambia kwani duni ni papai kwamba ataoza jela..lema si papai akichoka fursa ipo wazi..

  Lakini kuharibu amani ya nchi haikubaliki..ajifunze ustaarabu Tanzania siyo somalia..ok
   
 19. U

  Uyole12 JF-Expert Member

  #19
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 586
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  hata kama akitoka atakuwa kawafundisha nyie mnaomtishia jela. Kwa kuwa kila m2 anaweza kuishi huko hata wewe sema muda tu.
   
 20. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #20
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mpuuzi, makalio ya shngazi yako
   
Loading...