Mkoa wa Kilimanjaro washindwa kuingiza hata shule moja kwenye kumi bora matokeo ya darasa la Saba, 2021

Artificial intelligence

JF-Expert Member
Jan 28, 2021
1,262
2,191
Pamoja na kushika nafasi ya 6 kitaifa kama mkoa, Kilimanjaro katika matokeo ya mtihani wa taifa wa darasa la Saba 2021, umeshindwa kabisa kuingiza hata shule moja kwenye shule kumi bora kitaifa, huku ukiachwa mbali na mikoa ya Mara, Geita, na kagera.

Je ni kitu gani kinakwamisha shule za Kilimanjaro kama mkoa unaosifika kwa kuwa na elimu nzuri kuingia top ten kitaifa.

Je inawezekana ni kweli, shule zipo za kutosha Ila wanafunz wake Wana akili za kawaida.

JamiiForums777398578.jpg
 
Nilikuwa napitia pitia kuangalia shule ya mkoani kwetu, imeshika nafasi ya 6 kati ya 72.
Imenifurahisha sana japokuwa mazingira ya shule si rafiki.

Nimejaribu kuangali shule za jirani zetu ambapo miundombinu karibia yote ipo, lakini tumewaacha mbali..
 
Mbona huulizii Dar es salaam?
Huyu amepanic baada ya mkoa wao kagera kutoingia hata top ten na hata halmashaur za mkoa wao Hakuna hata moja imeingia top ten kwahyo anajifariji Kilimanjaro ni level Nyingine,wao kagera wapambane na umaskini wao Kwanza elimu watuachie Kilimanjaro .

Hata kiuchumi kagera wapo hoi katika mikoa 20 mkoa wao ni wa 17 kuchangia Pato la Taifa(GDP) hawa watu tuwaonee huruma kwakweli kujilinganisha na baba yao KILIMANJARO.

IMG-20211030-WA0012.jpg
FB_IMG_16348381071992474.jpg
FB_IMG_16348387759125991.jpg
 
Pamoja na kushika nafasi ya 6 kitaifa kama mkoa, Kilimanjaro katika matokeo ya mtihani wa taifa wa darasa la Saba 2021, umeshindwa kabisa kuingiza hata shule moja kwenye shule kumi bora kitaifa, huku ukiachwa mbali na mikoa ya Mara, Geita, na kagera...
Dah kweli sasa kilimanjaro ndo inapotea kwenye ramani ya elimu bora
 
Nilikuwa napitia pitia kuangalia shule ya mkoani kwetu, imeshika nafasi ya 6 kati ya 72.
Imenifurahisha sana japokuwa mazingira ya shule si rafiki.

Nimejaribu kuangali shule za jirani zetu ambapo miundombinu karibia yote ipo, lakini tumewaacha mbali..
Mkoa upi vs mikoa ipi? Be specific
 
Back
Top Bottom