Mkoa wa Kilimanjaro una makabila matatu na sio mawili

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
3,134
3,568
Kuna watu ukiwatajia kuwa unatoka mkoani Kilimanjaro wanajua wewe ni Mchanga!
Si kweli na kuna baadhi wanajua yakuwa Kilimanjaro kuna Wapare na Wachaga tu ngoja nikusanue.

Kilimanjaro kuna makabila matatu;
1, Wachaga
2, Wapare
3, Wagweno.

Leo nazungumzia wagweno kwa ufupi;
Wagweno wanapatikana katika milima ya Ugweno mkoani Kilimanjaro na kwa bahati mbaya wengi wamekuwa wakiwachanganya na wapare na wengine wakiwafananisha na wachaga kimuonekano:

1. Ni warefu sio wafupi kama wapare

2. Wanaongea lugha yao waiitayo kigweno isiyofanana kabisa na kipare japo inafanana na kichaga cha Rombo.
3. Majina yao Mshana, Msangi, Kimaro, Shirima, Mfinanga, Mbaga nk ukitumia majina unaweza kumwita mchaga au Mpare.

Kigweno ni kleori yani mchanganyiko wa lugha mbili yani kichaga na kipare japo kichaga ni dominant ktk lugha ya kigweno ambapo kihistoria baada ya wagweno kutoka Kenya kupitia Taveta kipundi hicho wakiwa makundi mawili ya wapare na wachaga walivyokutana ktk milima ya ugweno walikuwa wanaongea lugha mbili tofauti ambapo mkanganyiko huo ulipelekea kutokea kwa lugha mpya waliyoiita Kigweno yani ni mfano wa Kibantu na Kiarabu kupatikana lugha adhimu ya kiswahili.

Kwanini nasema kuwa Wagweno ni kabila?

Sifa za kabila;

1, Kuwa na Lugha ___Kigweno
2,Kuwa na tamaduni __ Kutambika
3, Kuwa na eneo ____ Ugweno kifula, Msangeni, Vuchama, Raa, Masumbeni nk
4, Shughuli za kijamii; Ufuaji wa vyuma bila kusahau kuwa Washana ndio watu wa kwanza weusi kufua vyuma duniani ambapo ilisaidia shughuli za kilimo, uwindaji nk

Hii mada ni ndefu sana japo kuna waliopotosha kuhusu mila na tamaduni za Kigweno kama Prof Kimambo katika kitabu chake "The History of Tanzania" but mlio tayari kujua kuhusu hili nakuja na full package ya Kitabu ambacho ni full of reseach kikikamilika nitawajuza namna ya kukipata kwa wale watakaopenda.

Wito wangu ni kwamba tusiishi kwa kukariri Waafrika tupende kujifunza.
 
Sio kweli hao wagweno wamechangiana mambo mangi sana na wasangi ambao ni jina moja linapatikana na kutambulika kama wapare.

Katika uchambuz wako umewasahau watu wa same ambao nao wanavaa kofia ya wapare je na wao wawekwe katika kundi gan?

Wapare wanakaa katika wilaya mbili wilaya ya Mwanga na wilaya ya same katika izo wilaya ndio wanapopatikana wapare

Sasa wewe umekurupuka tu huko na porojo zako ambazo sio za kweli

Ngoja kwanza nikale

Kishumba
Ugali wa ibada
Uji wa makafi
Kihombo
Makande
 
Ambiele Kiviele,

Wasangi ni kabila dogo sana Ugweno wengi wao wapo Usangi ambapo ndio upareni

Nina mashaka na level ya elimu yako, exposure na umri wako sitaki kubishana na wewe.
 
Wasangi ni kabila dogo sana Ugweno wengi wao wapo Usangi ambapo ndio upareni

Nina mashaka na level ya elimu yako, exposure na umri wako sitaki kubishana na wewe.
Hakuna lolote juu ya ichi ukisemacho utofaut wao haimanish kuwa wao sio wapare

Ndio mana mgweno au msangi popote pale akienda lazma atasema yeye ni mpare na sio msangi wala mgweno
 
Akili yako ndio ilikuwa inakujibu kuwa Kilimanjaro kuna Makabila Mawili na si Historia au hali halisi ilivyo... na Hayo ni mastory tu ya kale right now ukiitisha ukabila almost makabila yote yatajitokeza... Kuna Sehemu inaitwa Njoro kuna Wasambaa balaa huko na Makabila ya kila aina Wachagga unaweza ukawahesabu kwa uchache....

Kilimanjaro kasome historia kwanza ndio uje ujishebedue shebedue JF maana unaidharaulisha sana kwa ufinyu wa Historia kichwani mwako... Thread hii ungesema watu wenye asili haswa na mkoa huo kieneo n.k Maana Kuna Masai wapo karne kadhaa huko nyuma tokea walipotokea kwao Sudan...

Kuna Kina NGASA nalo ni Kabila japo ni dogo hilo huko Kilimanjaro...Kuna kabila la OngamoI sio wachaga kama wa Ngassa hao ila walibadilisha lugha yao tu na kutumia kichaga but wana umasai fulani ndani mwao , Wachagga na Wapare wapo kwa Wingi Kenya Haswa Wataveta ni mambabu za wachagga na Wapare na Wana Majina ya kikabila za kenya... Siri Moja Makabila ya mipakani usijitoe ufahamu kabisa utajichanganya...

Haswa Makonde,Waha,Waluo,Kurya,Wanyakyusa,Wanyassa,Wapemba,Waunguja,Wadigo,Yao n.k
Wagweno Lugha yao ina uchagga na upare na Kikamba cha Kenya ndio asili yao kubwa
 
Huyu Jamaa nadhani kaleta thread hii ili apate ufahamu zaidi asaidiwe tu


Huna unalolijua wewe kaa kimya mm nmekaa moshi zaidi ya 30 na nmefanya tafiti we endelea kuleta hadithi za babu zako huku
 
Back
Top Bottom