Mkoa wa Kilimanjaro ni mdogo kuliko Wilaya ya Liwale

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,553
44,722
Kilimanjaro Ina 13,250 km2 wakati liwale iliyopo Lindi ambao ni mkoa wa tatu kwa ukubwa Tanzania Ina zaidi ya hizo. Cha kuchekesha ni kwamba Burundi ukubwa wake ni mara mbili ya Kilimanjaro lakini ukicheki population utaona Kilimanjaro Ina watu zaidi ya 1.6 M wakati Lindi ina watu chini ya 1 M Na sababu kubwa inasemekana Lindi kihistoria ilikuwa war zone enzi za wakoloni pia Kawawa na sera zake za ujamaa ilifanya wahindi wengi wafanyabiashara kukimbia Lindi kuja Kariakoo.

Pia Kilimanjaro imekuwa kwa sababu ya kuwa na vyama vya ushirika imara historia inasema hivyo. Ombi la msingi ni kwamba tunaomba mkoa wa Lindi ugawanywe

Pia ingependeza Kilimanjaro itangazwe zaidi kwani Kenya wanaitumia sana kujitangaza maana mlima Kilimanjaro unaonekana tokea Nairobi.

Nadhani ujanja ujanja tu umetumika kuifanya Kilimanjaro iwe hivi Ilivyo ila sio kesi ipeni hadhi ya jiji ili utalii ukue.
 
Halafu Lindi shughuli za kiuchumi hazipo sasa ukigawanywa utabaki na nini,vilevile kigezo kikubwa katika kugawa Mkoa na Wilaya ni Idadi ya Watu.
 
Mkoa wa Lindi ni kati ya Mkoa wa hovyo hapa Tanzania,ukifuatiwa na Dodoma-angalau kidogo Nachingwea.
Dodoma umewahi fika? Halafu unatumia vigezo vipi kujua uhovyo wa hii mikoa. Shida mnatoka vijijini mkishaenda Dar nakuzura manzese kariakoo na tandika basi mnajua hayo ndomaisha kumbe kiuhalisia binadamu hutakiwi kujibana kwenye misongamano kama hiyo inabidi uishi sehemu nzuri yenye upepo na uwazi wa kutosha ikiwemo lindi na dodoma ni mikoa inayofaa sana kwa binadamu kuishi
 
Lindi baada ya kukamilika kwa barabara kwanda Mtwara na Songea, maisha yamebadilika sana kimaendeleo,

Tofauti na zamani wakati tunatumia pantoni kuvusha magari au kupanda meli ya mv maendeleo
 
Dodoma umewahi fika? Halafu unatumia vigezo vipi kujua uhovyo wa hii mikoa. Shida mnatoka vijijini mkishaenda Dar nakuzura manzese kariakoo na tandika basi mnajua hayo ndomaisha kumbe kiuhalisia binadamu hutakiwi kujibana kwenye misongamano kama hiyo inabidi uishi sehemu nzuri yenye upepo na uwazi wa kutosha ikiwemo lindi na dodoma ni mikoa inayofaa sana kwa binadamu kuishi
Dodoma maji ya chumvi,hayafai kwa matumizi sio kwa kunywa,ukioga unapauka ngozi-nguo ndio usiseme lazima utenge bajeti kabisa maana zinapauka zinakuwa kama poda.

Upepo tena ule wa hovyo,unapukutisha vumbi-ndio maana Dodoma ina vipofu wengi.
Jua linachoma balaa,tena sio lile kama LA Mikoa mengine ni kali vibaya sana.

Kiuchumi,ndio useseme ardhi ni mbaya tena kupita kiasi.
 
Mhmmmm Shida ya watoto wa mdogole kwa kopa kwa bibi nyau
 
Back
Top Bottom