Mkoa wa Chato na siasa za Kanda ya Ziwa nyuma ya pazia

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
MKOA WA CHATO NA SIASA ZA KANDA YA ZIWA NYUMA YA PAZIA

Nimesoma maandiko kadhaa kuhusiana na kuundwa kwa Mkoa wa Chato. Huwezi kuelewa vizuri kinachoendelea sasa bila kujua siasa za Kanda ya Ziwa zilizopo nyuma ya pazia.

Labda niwaeleze kidogo mambo ambayo yako nyuma ya Pazia na huwa hayaelezwi katika forum rasmi ili maamuzi ya busara yafanyike katika hili.

Kwanza kabisa nataka niwajulishe jambo moja. Chato ipo katikati ya Bukoba na Mwanza. Kutoka Chato hadi Bukoba ni takribani km 200 kama ilivyo kutoka Chato hadi Mwanza km 200.

Kusini mwa Chato kabla ya kulifikia Jiji la Mwanza kuna mji wa Geita yapata kama km 100. Na Kaskazini mwa Chato kabla ya kuifikia Bukoba kuna mji wa Muleba yapata km 132.

Mashariki mwa Chato mwanzo mwisho kuna Ziwa Victoria na Magharibi mwa Chato kuna Biharamulo yapata km 61, na Ngara yapata km 130.

Ukweli ni kwamba wilaya ya Ngara iko mbali sana na Bukoba. Ni km 300! Pia wilaya ya Kakonko iko mbali sana na Kigoma. Ni km 284! Haya ni maeneo ambayo zamani yalikuwa mapori lakini kwa sasa yana makazi mengi ya watu wanaohitaji huduma ya karibu.

Ukiangalia kwa makini hasa kwa masuala ya huduma, Runzewe ni kama imeunganika na Nyakanazi. Na Nyakanazi kihuduma imeunganika na Kakonko kuliko Kakonko na Kibondo. Nyakanazi pia imeunganika na Lusahunga. Lusahunga imeunganika na Biharamulo. Runzewe imeunganika na Bwanga. Bwanga imeunganika na Biharamulo. Maeneo yote hayo pamoja na Ngara yako mbali na mikoa yao yaani Kigoma, Kagera na Geita ukilinganisha na Chato ambayo iko katikati ya maeneo hayo.

Idadi ya watu Kanda ya Ziwa imekuwa inakua kwa kasi sana na kuzaliwa kwa Mkoa wa Chato kunatoa solution ya umbali wa huduma ya mkoani kati ya Kakonko kwenda Kigoma na Ngara kwenda Bukoba.

Sasa mzizi wa tatizo linaloibuka kuhusu ukinzani wa kuanzishwa Mkoa wa Chato nyuma ya Pazia umegubikwa na sababu za kikabila hasa ugomvi wa kiasili kati ya Biharamulo na Chato. Na pili watu waliojeruhiwa na Mwendazake Mwendazake wanahakikisha hakuna kizuri cha Mwendazake kinakatisha bila kukitia nyongo. Hawataki Mwendazake "apate furaha yoyote" huko aliko wakidhani ni fursa yao ya kulipiza kisasi.

Kwanza ieleweke kwamba Chato ilikuwa mojawapo ya tarafa za wilaya ya Biharamulo ambayo ni wilaya iliyoko Mkoa wa Kagera. Wakazi wa wilaya ya Biharamulo ni Wasubi ambao kutokana na kuwepo Mkoa wa Kagera kwa muda mrefu wamekuwa wakichukuliwa kama jamii ya Wahaya. Ukiwa nje ya Mkoa wa Kagera watu hujua Wahaya tu.

Migration ya Wasukuma kutoka Geita iliwafanya waijaze Chato kiasi kwamba baadaye Chato ikawa kama Sukumaland. Japo Chato kuna makabila mengi (Wasukuma, Wasubi, Wahaya, Wazinza na Wajita) lakini kabila ambalo limekuwa dominant ni Wasukuma.

Ukiwa pale Chato mjini lugha kuu ni Kisukuma. Ukiingia kwenye Kata za Chato Kisukuma ndio lugha kuu kasoro kata moja iliyoko karibu na Biharamulo inayoitwa Kasenga.

Sasa baada ya Wasukuma kuwa dominant Chato, wakawa wanaona shida kwenda mkoani Bukoba. Walitamani kuwa sehemu ya Mwanza lakini Mwanza ilikuwa kushoto kwao kwa sababu ili ufike Mwanza lazima uvuke maji.

Ulipoanza mkoa wa Geita, Chato ikapumua kwamba "tumetoka Uhayani". Lakini Hayaland wakaona eneo Lao limemegwa kwenda sukumaland.

Mtakumbuka kwamba mkoa wa Kagera awali ulikuwa na wilaya tano. Bukoba, Biharamulo, Muleba, Ngara na Karagwe. Wilaya zote hizo zilionekana kama ni Hayaland.

Mwendazake alipambana kuwa Mbunge wa Biharamulo kuanzia mwaka 1990 lakini alishindwa kwa sababu hizo za "anatoka usukumani".

Katika uchaguzi wa mwaka 1990 Mwendazake alishinda kata zilizoko Mashariki mwa Biharamulo (Chato) ambako kuna Wasukuma wengi waliohamia kutoka Geita.

Hata asili ya Mwendazake ni kwenye visiwa vya Nkome vilivyopo Kaskazini Magharibi mwa Geita ambavyo vinapakana na visiwa vya Rubondo kuliko na Hifadhi ya Taifa.

Biharamulo wanatoka Wasubi ambayo ni kama jamii ya Wahaya. Ni watu conservative sana. Ikaonekana ili Mwendazake apate jimbo lazima Biharamulo igawanywe. Ile Sukumaland ya Biharamulo iitwe Biharamulo Mashariki. Na baadaye ikaitwa Chato.

Kipindi cha utawala wa Mzee Mwinyi, Biharamulo ikagawanywa na kupatikana Biharamulo Mashariki ambayo ndio Chato. Ulipofanyika uchaguzi 1995 Mwenzazake akashinda kirahisi hilo Jimbo.

Hayaland wakaona eneo lao limetekwa usukumani na kubadilishwa jina kuitwa Chato. Kukawa na uhasama wa maneno ya kisiasa kati ya Chato na Biharamulo.

Mwendazake alivyoingia tu madarakani kama Mbunge 1995 akawa Naibu Waziri wa Ujenzi. Wakati huo vuguvugu la Chato Biharamulo lilikuwa limepamba moto.

Baada ya kukosa kura 1990 na kushinda 1995 na hasa alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi ukaibuka uvumi kuwa Mwendazake kawaapia watu wa Biharamulo kwamba lami wataisikia tu kwenye radio.

Ni uvumi ulioenea kwa kasi sana. Kwamba Mwendazake aliongea kwa Kisukuma. Eti alisema "Butabaaba du eebiharamulo mutaleebona elami" (Haki ya Mungu nyie watu wa Biharamulo lami mtaisikia tu).

Eti pia aliwaapia kwamba Chato itasonga mbele kwa kasi kubwa kuliko Biharamulo kwa sababu Wasukuma ni watu wa kazi. Wasubi na Wahaya ni wavivu walikuwa wanawachelewesha Wasukuma.

Uvumi huo ulitamalaki zaidi hasa baada ya Mwendazake kuanza kujenga barabara ya lami inayopitia Chato kutoka Bukoba badala ya kupitia Biharamulo.

Ili muweze kunielewa vzr labda kwanza niwaeleze jiografia ya barabara inayounganisha Tanzania na Kanda ya Ziwa Magharibi yaani barabara anayetoka Kahama hadi Kagera. Ni kwamba ili ufike Kagera kutokea Kahama unaweza kuamua upitie Chato au Biharamulo. Ukipita Chato unapita Ziwani kama Dar Chalinze kupitia Bagamoyo na Ukipita Biharamulo unapita "Bara" kama Dar Chalinze kupitia Kibaha&Mlandizi.

Junction ya kufanya maamuzi ya kupitia Chato au Biharamulo iko kwenye mji mmoja unaitwa Runzewe ambao uko karibu na Nyakanazi.

Sasa ukiamua kupitia Biharamulo maana yake ni kwamba kutoka hapo Runzewe utaenda mpaka Nyakanazi-Lusahunga-Biharamulo-Kyamyorwa-Muleba-Bukoba.

Na ukiamua kupitia Chato kuanzia hapo Runzewe route itakuwa Runzewe- Bwanga - Chato -Kyamilyorwa-Muleba-Bukoba.

Sasa, sehemu kubwa ya route ya Biharamulo barabara hiyo inapita porini katika pori la hifadhi la Biharamulo ambalo kwa sasa imekuwa Mbuga ya Burigi Chato, Lakini ukipitia Chato unapita ukanda wa Ziwani ambao ndio una miji mingi ya watu.

Kutokana na hilo, Mwendazake wakati akiwa Waziri wa Ujenzi na kutokana na ushawishi wake alianza kujenga barabara inayopitia Chato ambayo sio barabara ya Kitaifa. Barabara ya kitaifa ni ile inayopitia Biharamulo.

Hoja ya Mwendazake ni kwamba ni Bora kuanza kujenga lami kwenye makazi mengi ya watu kuliko kuanzia "porini" maana jukumu la serikali ni kuwasogezea huduma wananchi. Hiyo hoja watu wa Biharamulo hawakuielewa kwa kuwa kama Taifa kipaumbele kilitakiwa kuwekwa kwenye barabara ya kitaifa badala ya barabara ya Mkoa.

Baada ya barabara hiyo kujengwa gari nyingi sana za Mwanza - Bukoba zikawa zinapitia Chato. Mji wa Chato ukakua kwa kasi ukilinganisha na Biharamulo.

Kutokana na uwingi wa watu unaoongezeka kwa kasi kanda ya Ziwa upo umuhimu wa kuanzisha Mkoa wa Chato lakini changamoto zinazoibuliwa zina harufu ya ukabila kwamba kwanini Wahaya kutoka Ngara na Bukoba wahamishiwe usukumani.

Ni kweli Mwendazake alikuwa anapapenda sana nyumbani kwake. Na alitamani pawe na maendeleo makubwa. Nadhani haya pia ni matamanio ya mwanasiasa yoyote mwenye akili timu. Lakini uamuzi wa kupeleka maendeleo kwake kwa nia ya kuanzisha Mkoa wa Chato ameujengea hoja zinazoingia akilini.

Why Mkoa wa Chato ni muhimu. Utasababisha kuyaunganisha maeneo ya Kakonko, Nyakanazi, Lusahunga, Ngara, Biharamulo, Bwanga, Runzewe na kupata huduma ya mkoani karibu kwa umbali chini ya km 150 badala ya kulazimika kusafiri mpaka km takribani 300 unaenda mkoani.

Na Teacher Wa Professors Captain Enough (Negrosign).
 
Mama Tibaijuka na Mwendazake wote ni Wakabila tu.
Ila Mwendazake alizidisha Sana visasi....
 
Ni kweli Mwendazake alikuwa anapapenda sana nyumbani kwake. Na alitamani pawe na maendeleo makubwa. Nadhani haya pia ni matamanio ya mwanasiasa yoyote mwenye akili timu. Lakini uamuzi wa kupeleka maendeleo kwake kwa nia ya kuanzisha Mkoa wa Chato ameujengea hoja zinazoingia akilini.
Hivi nyumbani kwa Mwanasiasa Rais ni Wapi ?

Kweli mtu mzima na akili zako timamu unaona ni sawa kwa Kiongozi wa nchi (sio Kabila wala Mkoa) kuonyesha nepotism ? , Na unabariki kabisa kwamba ni sawa kwa mwanasiasa mwenye akili timamu ?

Wale wanaoona kwamba Rais kwao ni Tanzania na sio kijiji au kasehemu hawana akili ? Hii italeta precedent gani ?, Kwahio Samia akusanye kodi ajenge Zanzibar na sio penye tija au uhitaji zaidi ?..., Wewew hii Tanzania kuna sehemu huwezi kwenda mpaka utumie passport ? Kweli Awamu ya Tano imeharibu sana kazi kubwa ya Waasisi wa Taifa...
 
Mama waache walumbane ila usipitishe Chato kuwa mkoa.

Tumecheleweshwa sana au nasema uongo ndugu zangu?
 
MKOA WA CHATO NA SIASA ZA KANDA YA ZIWA NYUMA YA PAZIA

Ukiangalia kwa makini hasa kwa masuala ya huduma, Runzewe ni kama imeunganika na Nyakanazi. Na Nyakanazi kihuduma imeunganika na Kakonko kuliko Kakonko na Kibondo. Nyakanazi pia imeunganika na Lusahunga. Lusahunga imeunganika na Biharamulo. Runzewe imeunganika na Bwanga. Bwanga imeunganika na Biharamulo. Maeneo yote hayo pamoja na Ngara yako mbali na mikoa yao yaani Kigoma, Kagera na Geita ukilinganisha na Chato ambayo iko katikati ya maeneo hayo.
Siioni Chato kuwa katikati ya maeneo uliyotaja, labda Lusahunga itakuwa sahihi zaidi kwa maana ya kuingiza Kakonko, Ngara, Runzewe, Biharamulo, na Chato katika mkoa huo. Kama kuna maeneo yalimegwa Geita yakaingizwa Chato, hayo yarudishwe Geita.
Pili hoja za ukabila hazina mashiko; hatuundi mkoa wa wasukuma au wahaya. Hoja za ukabila zinafaa zaidi kwenye matambiko! Tanzania tushatoka huko, tunajenga Tanzania ya Watanzania na ndio maana wewe mwenyewe umeandika kuwa wasukuma wengi walihamia Chato.
 
Mbowe kwenye mizunguko yake yote anatetea wachaga
 
Ufafanuzi mzuri sana. Ila mwendazake asingekuwa na siasa za kisasi na chuki alipaswa kuendeleza Biharamulo maana ndo katikati kabisa na hizo wilaya zinazotakiwa kuunda mkoa wake. Kuweka makao makuu Chato bado watu wa Ngara wataendelea kwenda umbali mrefu.
 
"Ni kweli Mwendazake alikuwa anapapenda sana nyumbani kwake. Na alitamani pawe na maendeleo makubwa. Nadhani haya pia ni matamanio ya mwanasiasa yoyote mwenye akili timamu". Kwahiyo Nyerere, Mwinyi, Mkapa...hawakuwa na akili timamu? Maana wao walijali maendeleo ya nchi kwa ujumla na sio ya nyumbani kwao!
 
Hata Mbowe anatetea wachaga tu
 
MKOA WA CHATO NA SIASA ZA KANDA YA ZIWA NYUMA YA PAZIA

Nimesoma maandiko kadhaa kuhusiana na kuundwa kwa Mkoa wa Chato. Huwezi kuelewa vizuri kinachoendelea sasa bila kujua siasa za Kanda ya Ziwa zilizopo nyuma ya pazia.

Labda niwaeleze kidogo mambo ambayo yako nyuma ya Pazia na huwa hayaelezwi katika forum rasmi ili maamuzi ya busara yafanyike katika hili.

Kwanza kabisa nataka niwajulishe jambo moja. Chato ipo katikati ya Bukoba na Mwanza. Kutoka Chato hadi Bukoba ni takribani km 200 kama ilivyo kutoka Chato hadi Mwanza km 200.

Kusini mwa Chato kabla ya kulifikia Jiji la Mwanza kuna mji wa Geita yapata kama km 100. Na Kaskazini mwa Chato kabla ya kuifikia Bukoba kuna mji wa Muleba yapata km 132.

Mashariki mwa Chato mwanzo mwisho kuna Ziwa Victoria na Magharibi mwa Chato kuna Biharamulo yapata km 61, na Ngara yapata km 130.

Ukweli ni kwamba wilaya ya Ngara iko mbali sana na Bukoba. Ni km 300! Pia wilaya ya Kakonko iko mbali sana na Kigoma. Ni km 284! Haya ni maeneo ambayo zamani yalikuwa mapori lakini kwa sasa yana makazi mengi ya watu wanaohitaji huduma ya karibu.

Ukiangalia kwa makini hasa kwa masuala ya huduma, Runzewe ni kama imeunganika na Nyakanazi. Na Nyakanazi kihuduma imeunganika na Kakonko kuliko Kakonko na Kibondo. Nyakanazi pia imeunganika na Lusahunga. Lusahunga imeunganika na Biharamulo. Runzewe imeunganika na Bwanga. Bwanga imeunganika na Biharamulo. Maeneo yote hayo pamoja na Ngara yako mbali na mikoa yao yaani Kigoma, Kagera na Geita ukilinganisha na Chato ambayo iko katikati ya maeneo hayo.

Idadi ya watu Kanda ya Ziwa imekuwa inakua kwa kasi sana na kuzaliwa kwa Mkoa wa Chato kunatoa solution ya umbali wa huduma ya mkoani kati ya Kakonko kwenda Kigoma na Ngara kwenda Bukoba.

Sasa mzizi wa tatizo linaloibuka kuhusu ukinzani wa kuanzishwa Mkoa wa Chato nyuma ya Pazia umegubikwa na sababu za kikabila hasa ugomvi wa kiasili kati ya Biharamulo na Chato. Na pili watu waliojeruhiwa na Mwendazake Mwendazake wanahakikisha hakuna kizuri cha Mwendazake kinakatisha bila kukitia nyongo. Hawataki Mwendazake "apate furaha yoyote" huko aliko wakidhani ni fursa yao ya kulipiza kisasi.

Kwanza ieleweke kwamba Chato ilikuwa mojawapo ya tarafa za wilaya ya Biharamulo ambayo ni wilaya iliyoko Mkoa wa Kagera. Wakazi wa wilaya ya Biharamulo ni Wasubi ambao kutokana na kuwepo Mkoa wa Kagera kwa muda mrefu wamekuwa wakichukuliwa kama jamii ya Wahaya. Ukiwa nje ya Mkoa wa Kagera watu hujua Wahaya tu.

Migration ya Wasukuma kutoka Geita iliwafanya waijaze Chato kiasi kwamba baadaye Chato ikawa kama Sukumaland. Japo Chato kuna makabila mengi (Wasukuma, Wasubi, Wahaya, Wazinza na Wajita) lakini kabila ambalo limekuwa dominant ni Wasukuma.

Ukiwa pale Chato mjini lugha kuu ni Kisukuma. Ukiingia kwenye Kata za Chato Kisukuma ndio lugha kuu kasoro kata moja iliyoko karibu na Biharamulo inayoitwa Kasenga.

Sasa baada ya Wasukuma kuwa dominant Chato, wakawa wanaona shida kwenda mkoani Bukoba. Walitamani kuwa sehemu ya Mwanza lakini Mwanza ilikuwa kushoto kwao kwa sababu ili ufike Mwanza lazima uvuke maji.

Ulipoanza mkoa wa Geita, Chato ikapumua kwamba "tumetoka Uhayani". Lakini Hayaland wakaona eneo Lao limemegwa kwenda sukumaland.

Mtakumbuka kwamba mkoa wa Kagera awali ulikuwa na wilaya tano. Bukoba, Biharamulo, Muleba, Ngara na Karagwe. Wilaya zote hizo zilionekana kama ni Hayaland.

Mwendazake alipambana kuwa Mbunge wa Biharamulo kuanzia mwaka 1990 lakini alishindwa kwa sababu hizo za "anatoka usukumani".

Katika uchaguzi wa mwaka 1990 Mwendazake alishinda kata zilizoko Mashariki mwa Biharamulo (Chato) ambako kuna Wasukuma wengi waliohamia kutoka Geita.

Hata asili ya Mwendazake ni kwenye visiwa vya Nkome vilivyopo Kaskazini Magharibi mwa Geita ambavyo vinapakana na visiwa vya Rubondo kuliko na Hifadhi ya Taifa.

Biharamulo wanatoka Wasubi ambayo ni kama jamii ya Wahaya. Ni watu conservative sana. Ikaonekana ili Mwendazake apate jimbo lazima Biharamulo igawanywe. Ile Sukumaland ya Biharamulo iitwe Biharamulo Mashariki. Na baadaye ikaitwa Chato.

Kipindi cha utawala wa Mzee Mwinyi, Biharamulo ikagawanywa na kupatikana Biharamulo Mashariki ambayo ndio Chato. Ulipofanyika uchaguzi 1995 Mwenzazake akashinda kirahisi hilo Jimbo.

Hayaland wakaona eneo lao limetekwa usukumani na kubadilishwa jina kuitwa Chato. Kukawa na uhasama wa maneno ya kisiasa kati ya Chato na Biharamulo.

Mwendazake alivyoingia tu madarakani kama Mbunge 1995 akawa Naibu Waziri wa Ujenzi. Wakati huo vuguvugu la Chato Biharamulo lilikuwa limepamba moto.

Baada ya kukosa kura 1990 na kushinda 1995 na hasa alipoteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi ukaibuka uvumi kuwa Mwendazake kawaapia watu wa Biharamulo kwamba lami wataisikia tu kwenye radio.

Ni uvumi ulioenea kwa kasi sana. Kwamba Mwendazake aliongea kwa Kisukuma. Eti alisema "Butabaaba du eebiharamulo mutaleebona elami" (Haki ya Mungu nyie watu wa Biharamulo lami mtaisikia tu).

Eti pia aliwaapia kwamba Chato itasonga mbele kwa kasi kubwa kuliko Biharamulo kwa sababu Wasukuma ni watu wa kazi. Wasubi na Wahaya ni wavivu walikuwa wanawachelewesha Wasukuma.

Uvumi huo ulitamalaki zaidi hasa baada ya Mwendazake kuanza kujenga barabara ya lami inayopitia Chato kutoka Bukoba badala ya kupitia Biharamulo.

Ili muweze kunielewa vzr labda kwanza niwaeleze jiografia ya barabara inayounganisha Tanzania na Kanda ya Ziwa Magharibi yaani barabara anayetoka Kahama hadi Kagera. Ni kwamba ili ufike Kagera kutokea Kahama unaweza kuamua upitie Chato au Biharamulo. Ukipita Chato unapita Ziwani kama Dar Chalinze kupitia Bagamoyo na Ukipita Biharamulo unapita "Bara" kama Dar Chalinze kupitia Kibaha&Mlandizi.

Junction ya kufanya maamuzi ya kupitia Chato au Biharamulo iko kwenye mji mmoja unaitwa Runzewe ambao uko karibu na Nyakanazi.

Sasa ukiamua kupitia Biharamulo maana yake ni kwamba kutoka hapo Runzewe utaenda mpaka Nyakanazi-Lusahunga-Biharamulo-Kyamyorwa-Muleba-Bukoba.

Na ukiamua kupitia Chato kuanzia hapo Runzewe route itakuwa Runzewe- Bwanga - Chato -Kyamilyorwa-Muleba-Bukoba.

Sasa, sehemu kubwa ya route ya Biharamulo barabara hiyo inapita porini katika pori la hifadhi la Biharamulo ambalo kwa sasa imekuwa Mbuga ya Burigi Chato, Lakini ukipitia Chato unapita ukanda wa Ziwani ambao ndio una miji mingi ya watu.

Kutokana na hilo, Mwendazake wakati akiwa Waziri wa Ujenzi na kutokana na ushawishi wake alianza kujenga barabara inayopitia Chato ambayo sio barabara ya Kitaifa. Barabara ya kitaifa ni ile inayopitia Biharamulo.

Hoja ya Mwendazake ni kwamba ni Bora kuanza kujenga lami kwenye makazi mengi ya watu kuliko kuanzia "porini" maana jukumu la serikali ni kuwasogezea huduma wananchi. Hiyo hoja watu wa Biharamulo hawakuielewa kwa kuwa kama Taifa kipaumbele kilitakiwa kuwekwa kwenye barabara ya kitaifa badala ya barabara ya Mkoa.

Baada ya barabara hiyo kujengwa gari nyingi sana za Mwanza - Bukoba zikawa zinapitia Chato. Mji wa Chato ukakua kwa kasi ukilinganisha na Biharamulo.

Kutokana na uwingi wa watu unaoongezeka kwa kasi kanda ya Ziwa upo umuhimu wa kuanzisha Mkoa wa Chato lakini changamoto zinazoibuliwa zina harufu ya ukabila kwamba kwanini Wahaya kutoka Ngara na Bukoba wahamishiwe usukumani.

Ni kweli Mwendazake alikuwa anapapenda sana nyumbani kwake. Na alitamani pawe na maendeleo makubwa. Nadhani haya pia ni matamanio ya mwanasiasa yoyote mwenye akili timu. Lakini uamuzi wa kupeleka maendeleo kwake kwa nia ya kuanzisha Mkoa wa Chato ameujengea hoja zinazoingia akilini.

Why Mkoa wa Chato ni muhimu. Utasababisha kuyaunganisha maeneo ya Kakonko, Nyakanazi, Lusahunga, Ngara, Biharamulo, Bwanga, Runzewe na kupata huduma ya mkoani karibu kwa umbali chini ya km 150 badala ya kulazimika kusafiri mpaka km takribani 300 unaenda mkoani.

Na Teacher Wa Professors Captain Enough (Negrosign).
Ni Mungu tu alimwahi angefanya Chato kuwa makao makuu ya nchi na East African Community!
 
Back
Top Bottom