Lu-ma-ga
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 4,780
- 3,227
Kikwete mtegoni tena
na Waandishi wetu-TANZANIA DAIMA
Maswawatishia kuandamana
Katika hatuanyingine, hatua ya Rais Kikwete kuunda mikoa mipya, imezua balaa baada ya mamiaya wananchi wa wilaya ya Maswa, mkoa wa Shinyanga kuandaa maandamano iwaposerikali itaamua kuyaweka makao makuu ya mkoa mpya wa Simiyu katika wilaya yaBariadi.
Wakizungumzakatika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Uwanja wa Nguzo Nane nakuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa wilaya hiyo, wananchi hao wamedai kuwa hawakotayari kutendewa hivyo na wataandamana hata ikilazimu kupigwa risasi.
Katika mkutanohuo ulioitishwa kwa ajili ya kutoa maoni ya mapendekezo juu ya nia ya serikaliya kupeleka makao makuu ya mkoa mpya wa Simiyu mjini Bariadi, wananchi haowamesema uamuzi huo ni dharau kwao na unataka kufanywa kwa ajili ya manufaa yaviongozi wachache.
Sisi wanaMaswa tutaandamana bila kujali itikadi za vyama kamahatutasikilizwa na tuko tayari kupigwa risasi. Hatuwezi kunyanganywa haki yetukwa ajili ya ubinafsi wa viongozi wachache, alisema mkazi mmoja wa Maswa,Thomas Nkola, na kushangiliwa na umati wa wananchi.
Walisema kuwaviongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa wilayaya Bariadi wamekuwa na desturi ya ubinafsi katika masuala yenye maslahi ya ummakitendo kilichodhihirika katika ujenzi wa barabara ya lami ya MwigumbiMaswa-Lamadi.
Viongozi wetuwa mkoa wa Shinyanga na wa Bariadi wametuona sisi wa Maswa watulivu sana hivyo wanatumiamwanya huo kutuchezea.
Mfano ujenziwa barabara ya lami ya Mwigumbi-Maswa-Lamadi ilitakiwa ianzie Mwigumbi kujaMaswa lakini kutokana na ubinafsi wao imeanzia Bariadi kwenda Lamadi, alisemamwananchi mwingine, Samwel Kidima.
Walisema lichaya mapenzi mema aliyonayo Rais Jakaya Kikwete ya kuanzisha mkoa huo, ni vizurimchakato wa kupata makao makuu yake ukaanza upya kwani wa awali haukupitiakatika vikao halali kama vile baraza lamadiwani na kamati za ushauri za wilaya (DCC) hali ambayo imezua mgogoro mkubwana kufanya kutokuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya wananchi wa wilaya hizo.
Rais Kikwetealipoamua kuanzisha mikoa na wilaya mpya alikuwa na nia nzuri sana lakini jambola kushangaza mchakato wa kutoa mapendekezo ya makao makuu ya mkoa wa Simiyuhayakufuata utaratibu kwani ilitakiwa uanzie katika vikao vya baraza lamadiwani na kamati za ushauri za wilaya ndiyo maana jambo hili limezua mgogoromkubwa na sasa mahusiano kati ya wananchi wa wilaya ya Maswa na Bariadi simazuri hivyo mchakato uanze upya, alisema Edward Bunyongoli.
Walisema iwaposerikali itabaki na msimamo wake huo basi wao wataendelea kubaki katika mkoa waShinyanga lakini hawako tayari kukubaliana na uamuzi huo uliofanywa kwa ajiliya maslahi ya watu wachache wabinafsi.
Kama serikali itabaki na msimamo kuwa Bariadi ndiyo makaomakuu ya mkoa wa Simiyu sisi tutabaki katika mkoa wa Shinyanga kwani hatukotayari kukubali uamuzi huo uliotawaliwa na vitendo vya kifisadi, alisema KulwaNangale.
Hii si mara yakwanza kudanganywa kwa Rais kwani ameshadanganywa zaidi ya mara 12 miongoni mwamambo aliyodanganywa ni pamoja na ile ya kuzindua mradi wa Bwawa la Manchiralililoko wilayani Serengeti wakati tayari wananchi wamekwishafungua kesiMahakama Kuu ya Mwanza wakidai fidia.
Kesi hiyoiliyofunguliwa ni matokeo ya viongozi wa serikali wilayani humo kuhusikakuwalipa fidia watu wasiohusika na kuwaacha walengwa waliofanyiwa tathmini.
Pia aliwahikudanganywa kwamba daraja la Mkenda lililoko Ruvumaambalo ni njia muhimu kuelekea Msumbiji, lilikuwa limekamilika.
Katika tukiojingine, Rais aliwahi kupewa taarifa zisizo sahihi kuhusu tuhuma za rushwazilizokuwa zikimkababili Anatory Choya kisha akamteua kuwa mkuu wa wilaya,lakini siku siku chache baadaye akafunguliwa mashtaka na TAKUKURU.
Mwaka juzi,akiwa ziarani Mbeya msafara wa Rais ulishambuliwa kwa mawe na watu, lakiniwasaidizi wake wakaja kutoa taarifa kwamba watu hao walikuwa ni wahuni nawalikuwa wakimsubiri Rais kwa muda mrefu bila mafinikio.
Hata hivyo,baadaye uchunguzi huru ulibainisha kwamba tukio hilo lilikuwa na mafungamano ya kisiasa namakovu ya mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM kwa mwaka 2005.
Mlolongo huomrefu wa upotoshaji taarifa kwa Rais uliibuka tena katika utoaji wa magari yamisaada ambapo badala ya kupewa mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Longidoalipewa wa Ngorongoro.
Tukio hilo lilimfanya mkuu huyowa nchi kukasirika na kumzodoa mkurugenzi huyo, lakini baadaye ikabainikamkurugenzi huyo alikwenda kutokana na makosa ya maafisa wa Ikulu.
Katikamlolongo huo, tukio kubwa kabisa ni Rais kutia saini kwa mbwembwe Sheria yaGharama za Fedha za Uchaguzi ambayo ilichomekwa vipengele nje ya Bunge kituambacho ni kinyume cha sheria.
Tukio hilo ambalo ni lauvunjifu wa Katiba, liliibuliwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa,ambaye awali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fedrerick Werema, alikanusha.
Hata hivyo,baadaye sheria hiyo ilirudishwa bungeni na kukarabatiwa kwa mgongo wamabadiliko ya sheria mbalimbali.
Mei mwakajana, Rais alipewa taarifa za upotoshaji kuhusu mazungumzo ya Shirikisho laVyama vya Wafanyakazi (TUCTA) na serikali, kwa kuelezwa shirikisho hilo halikuhudhuria mkutano wa saa 4:00 asubuhi kama ilivyopangwa.
Hata hivyo,TUCTA wakatoa ushahidi wa barua za mwaliko wa mkutano huo wa Aprili 22 mwakajana, ambazo zilikuwa mbili, moja ikionyesha walitakiwa kufika katikamazungumzo Hazina saa 4:00 asubuhi na nyingine saa 8:00 mchana.
Katikakuonyesha upotoshaji kwa Rais, wasaidizi hao walimpa barua iliyokuwa ikionyeshawalipaswa kukutana saa 4:00 asubuhi huku ile ya saa 8:00 wakawa wameificha.
Raisakizungumza na wazee wa mkoa wa Dares Salaam aliwashambulia viongozi wa TUCTAhasa Naibu Katibu Mkuu, Nicolas Mgaya, akimwita mnafiki, mzandiki, na mchochezi.