Mkoa mpya Simiyu: Wananchi kuweka kando tofauti za kisiasa kwa kudai haki yao

Mzee,Asante kwa rekodi zako na utafiti ulioufanya kama data hizi ni za kweli.Ni kweli kabisa Bariadi iko mbele kiuchumi na Kimaendeleo kwa ujumla. Kwa vile Maswa iko nyuma basi ni busara kuifanya makao makuu ili nayo ipae hadi kuipita Bariadi. Naamini hii ndo njia pekee ya kuikwamua Maswa. Tatizo la Mswa ni kama "Land locked state". Haina access na barabara kuu yoyote inayotoka nje ya nchi. Imewekwa kati na wilaya zote.Bariadi ina- enjoy kuwa mwishoni mwa mkoa wa Shy ikipakana na Arusha. Naomba busara kidogo tu itumike kerejesha makao makuu Maswa kama ilivyokuwa imepangwa awali. Tusilete siasa na ubinafsi hapa.
 
Tunakukumbuka Mh. Dr. Pius Yasebasi Ng'wandu mazuri yote uliyoyafanya maswa yanaonekana machukizo kwa MAFISADI.Maswa uliiweka katika dunia mpya kwa kuwa hukuwa fisadi rasilimali zilitumika vizuri kwa kutumia ubunge wako leo Manyang'au yanakuja na ajenda mpya yanasema SIMIYU wakati maswa ni baba wa bariadi na meatu.TUTAPAMBANA HADI KIELEWEKE.Tunamsubiri mbunge wetu MH.KASULUMBAI JEMBE ULAYA watanyoosha maelezo tuuuuuuuu.
Lumaga tumia lugha nzuri ili ujumbe uweze kufika vizuri.

Nakubaliana na wewe Maswa ni wilaya kongwe kuliko Bariadi na Meatu lakini hiyo haiwezi kuifanya ikawa makao makuu. Tatizo la Maswa ni kuwa toka iachiwe majengo na mkoloni ni yale yale haiyaendelezi, hata town master plan ya Maswa ni ya enzi ya mkoloni imebanana ukilinganisha na ya Bariadi ambayo ina mitaa (streets)na barabara zenye nafasi ya kuufanya kuitwa jiji baadae.

Ki uchumi:
Hali ya hewa ya Maswa ni kame haina ardhi ya rutuba ya mazao ya chakula, ardhi ya Bariadi inakidhi mazao ya biashara pamba na chakula mahindi na mtama. Bariadi (Wanyantuzu) ni wafugaji wakubwa wa ng'ombe asilimia kubwa ya mifugo Tanzania inatoka wilaya ya Bariadi na Arusha wamasai waliopakana nao. Bariadi iko karibu na ziwa Victoria km 20 tu kwa hiyo mbali na kilimo wakazi wa Bariadi wengi hujishughulisha na uvuvi katika ziwa Victoria.

Sehemu ya mbuga ya Serengeti iko Bariadi kuna usafiri wa ndege na viwanja vya ndege kwenye mahoteli ya kitalii yanayoendelea kujengwa kwa hiyo Bariadi kama makao makuu itafaidika na Biashara ya watalii tofauti na Maswa iliyo kame.

Bariadi ina viwanda vingi vya kusindika mafuta ya mbegu ina viwanda vingi tu vya kuchambua pamba, ina viwanda vya kuzalisha magogo nk kifupi ki uchumi Bariadi iko juu sana kulinganisha na Maswa.

Mji kuitwa mji unategemea na population ya pale Maswa ni ya zamani sawa lakini haikui, p'pln ya Bariadi ni karibu mara 2 ya Maswa na eneo la Bariadi ni karibu mara 4 ya eneo la Maswa hivi vyote ni vigezo vilivyotumika, kuwa hata hapo mbeleni mji unaweza kujitanua na kuaccommodate viwanda na biashara kubwa zaidi.

Bariadi ina Bwawa lake kubwa tu la maji kwenye mto Bariadi unaopeleka maji yake ziwa Victoria lisilotegemea mvua linaweza kunywesha hadi wilaya za jirani. Kuhusu nishati Bariadi iko kwenye Gridi ya Taifa umeme unaotoka Mwanza kwenda Mara Musoma.

Infrastructure: Bariadi leo hii ninapoandika kuna barabara ya rami inajengwa Bariadi-Lamadi (30km?) kuunganisha Bariadi na barabara kuu itokayo Mwanza-Musoma-Sirali. Bariadi iko karibu na ziwa Victoria kwa usafiri na usafirishaji. Kuna eneo kubwa limetengwa kwa uwanja wa ndege lakini kabla ya huo uwanja kwisha ni mwendo wa masaa mawili au matatu tu kwenda Mwanza kwenye uwanja mkubwa wa Ndege.

Kuna mpango wa kuunganisha Mwanza na Arusha kwa barabara ambayo itapitia Bariadi mpango huu upo lakini ni long plan.

Kuhusu Maswa kuwa iko katikati au mji wa kihistoria nafikiri hizo siyo sababu kubwa hata hivyo unaposema Bariadi iko mbali na wapi je mtu wa Lamadi au Nasa kwenda Maswa utasemaje.

Sababu hizi na zingine nilizozitaja ndizo zilizosababisha Bariadi kuwa makao makuu ya Mkoa wa Simiyu lakini kubwa ni hilo la uchumi na population.
 
Back space kaka. Taarifa hii niliisikia juzi wakati nimetembelea maswa. Siku waliyotangaza kwamba wamepeleka makao makuu Bariadi nilishuudia wazee kwa vijana pale maswa wamechanganyikiwa na walikuwa wanahaha kuwasiliana na waziri na aliwajibu wapeleke pingamizi zao ndanin ya siku ishirini na moja
 
Mzee K.K Nangale amefariki siku ya 9/12/2012 Maswa na amezikwa tarehe 12/12/2012.....alifanya kazi ya watu,Mungu amempenda zaidi...
 
Back
Top Bottom