Mkoa gani kuna wafugaji wa ng'ombe wengi, ambapo nitaweza kununua maziwa kwa wingi kuanzia lita 500 nakuendelea?

Habari zenu wana hili jukwaa? Mimi nipo Dar nilikua natafuta mahala au mkoa ambao uko karibu na Dar ambapo nitaweza kupata wafugaji wa ng'ombe kwa wingi ili niweze kununua maziwa mazuri ya ng'ombe hasa kuanzia lita 500 nakuendelea, naomba mnisaidie kwa wanaojua hata ikiwezekana contacts za wafugaji. Ahsanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
Njoo pm nina miniranch naweza kukusupply zaidi ya Lita mia 600 yakiwa fresh bila kuwa added na chochote.Pia nassupply maziwa safi ya mtindi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuanzia mlandiz mpk chalinze eneo la wafugaji wa ng’ombe wa maziwa kwa wingi hata ndugu yng nae yupo mbwawa pale anafuga na maziwa anauza nenda mkandizi stend uliza mkuu utapata jibu zuri


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
unahitaji kila siku au kwa interval gani?shambani kwangu yanapatikana lita 200 kila siku,nikichanganya na jirani 500 sio issue,na kama bei iko sawa yatakufikia popote kuanzia bunju hadi mwenge,njoo pm kama vipi
 
tumebarikiwa vitu vingi sana yan tuna mifugo na maziwa yakutosha ivi ila ndo ivo jaman,ilibidi wafugaji wawe matajiri wakubwa kwa soko la ndani na nje ya tz
 
Inawezekana hata kwenye mashule yale bording,au wanafunzi hawastaili kunywa maziwa
nashangaa tanzania mashule mengi hawapewi maziwa kabisa hasa za serikali nizosoma wakati tuna mabwawa ya maziwa na nyama zakutosha, ivi kwanini?
 
mkuu weka 2000 @ liter, visiga kibaha njiani kabisa unapata maziwa mazuri ambayo hayajaguswa, uhakika ni kuja na vipimo vyako tu mkuu
 
Naomba kuuliza kwa wafugaji miliko kuanzia kibaha mpaka mlandizi nasikia kunamajani Ngombe Mbuzi wakiyala wanakufa ghafla, hiichqngamoto nasikia ni kubwa mnakabiliana nayo vipi?. Ninashamba kongowe soga nataka nianze ufugaji wa ngombe wa maziwa na mbuzi. Naomba ushauri tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom