M'kiti wa kijiji Kilolo (CHADEMA) aswekwa lupango kwa kutochangia mwenge

Mi naona Mwenge uwe una waswa siku ya Uhuru tu. Badala ya kuuzungusha nchi nzima kwakisingizio cha kuzindua miradi ya maendeleo ifunguliwe na wakuu wa wilaya/mikoa nk.
 
dc kichaa kweli kweli anathamini koroboi, mwenge kwa kawaida unahamasisha ngono zembe kila unapolala, uacha virus watu 10
 
We ni kweli Mwenge umepita huko Juni 22? Mbona Kama unadanganya vile?
 
jambo hili linasikitisha sana kama hali ndiyo hii ya kuchanga pesa kwaajili ya mwenge kila kijiji Tshs.70,000 mara vijiji vyote TANZANIA bara na visiwani, ni shilingi ngapi? halafu kila mwaka serikali inatenga mamillioni ya pesa kwaajili ya mwenge! hamuoni kwamba huu ni mradi wa mafisadi? tunaomba mdhibiti na mkaguzi wa mahesabu ya serikali akague pesa hizi zinatumikaje halafu ripoti iwekwe wazi kisha uwekwe mjadala wa kitaifa kama tuendelee kukimbiza mwenge au uwekwe makumbusho ya taifa!?na pia tujue mnufaika ninani? wakijulikana hawa mashetani tuwatangaze kama MAADUI WA TAIFA LA TANZANIA! NA TUWATENGE TUSISHIRIKIANE NAO.:spy::spy::spy:
 
Tanzania ni nchi ya kipekee, bora koroboi itembezwe elimu baadaye
 
mwenge hata wana CCM wenyewe hawautaki leo unaambiwa Tanga hakukuwa na CCM mkoa wala CCM wailaya pangani kuupokea mwenge walipoulizwa wamesema akaulizwe mkuu wa mkoa Chiku Gallawa ,huyu mwenyekiti wa kijiji kichwa kafata taratibu yeye na kamati yake wameona watoto kwanza safiiiiiiiiiii
 
Mkuu wa wilaya, alichokifanya ni kitu kisichoeleweka, hapo tuseme ni chuki binafsi ya kisiasa.
Mwenge umefika wakati wa kwenda makumbusho ya Taifa. Kwa sababu tokea miaka
hamsini iliyopita, umeshachangia mambo ambayo hayana faida. Kwanza umaskini na
kuharibu kwa kiasi kikubwa cha mazingira nchini, yaani (out door air pollution).
Kwa sababu kuchoma mafuta ya taa kwa kuzunguka Tanzania nzima kila mwaka,
huo ni uzalishaji wa (Carbon Dioxide). Ambayo inawaathiri wagonjwa wa Pumu,
kuathiri miche mashambani na misitu kukauka, na kibaya zaidi kuleta (Acid Rain).
Ambayo uharibu mazao, maji na ardhi, sasa kuna faida gani ya kuendelea na mwenge
wakati hauna hata asilimia moja ya maendeleo kwa Watanzania.
 
hivi michango ya mwenge kwa kulazimishwa bado ipo? Mlichelewa wapi? Huku hata wafanyabiashara wanaombwa mchango hawalazimishwi. Mwenge unapopita hakuna ulazima wa kufunga duka lako; ni takabuli tu!
 
Hii ndio serikali ya Tanzania bwana, mwenge wa uhuru ni muhimu kuliko chaki za watoto mashuleni. Kweli tuna kazi watanzania.
 
Nakumbuka when i was form 3 pale darajan sec marangu,hii koroboi ili lala pale chuo cha walimu marang ili upandishwe mt k'njaro.the next day 2lifanya usafi pale uwanjani tukaokota USED CONDOM malboro moja! Since dat day i dont want to hear a thng call mwenge
 
Back
Top Bottom