M'kiti wa kijiji amtandika fimbo mwalimu mkuu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,820
MWENYEKITI wa Kijiji cha Kemakorere, Zephania Chacha anadaiwa kumshambulia kwa viboko mkuu msaidizi wa Shule ya Sekondari Kemakorere, Juma Selemani Hango akimtuhumu kukata miti miwili ya shule hiyo.

Chacha ameshafikishwa kituo cha polisi kilicho kwenye Kata ya Nyarero wilayani Tarime na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kujibu shtaka la kushambulia kwa fimbo na kumsababishia mwalimu huyo maumivu makali.

Tukio hilo ni mwendelezo wa vipigo dhidi ya walimu ambavyo vilianza kusikika baada ya mkuu wa wilaya ya Bukoba, Albert Mnali kuamuru polisi wa kijeshi kuwatandika viboko walimu wa shule tatu kwa madai kuwa ni watoro kazini.

Lakini katika tukio la mkoani Mara, mwenyekiti huyo wa kijiji alichukua hatua hiyo baada ya kupata habari kuwa mkuu huyo msaidizi wa shule alikuwa akikata miti kwenye shamba la shule kwa ajili ya kutengenezea mlango wa choo.

Mkuu wa makosa ya jinai wa Tarime/Rorya, David Hiza alisema kuwa tukio hilo la shambulio hilo dhidi ya Hango lilitokea Julai 5 mwaka huu mchana wakati mwalimu huyo alipokata miti miwili ya shule kwa ajili ya kupasua mbao za kutengenezea mlango wa choo cha shule hiyo.

Hiza alisema kuwa baada ya mwenyekiti huyo kupata taarifa kuwa mwalimu huyo alikuwa akikata miti bila ya ruhusa yake, alienda eneo hilo na kumkuta Mwalimu hango akiendelea na shughuli ya kupasua mbao pamoja na mafundi na ndipo vurugu kubwa ilipozuka.

Alisema katika vurugu hizo, mwenyekiti huyo alichukua fimbo na kuitumia kumshambulia mwalimu huyo na kusababisha apate maumivu sehemu mbalimbali za mwili.

Hiza alisema baadaye mwalimu huyo alifungua jalada namba NY/IR/392/2010 kwenye kituo cha polisi cha Nyamwaga na kwamba mwenyekiti huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote ule.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kemakorere, Phafin Boroye alisema kuwa uongozi na kamati ya shule hiyo umesikitishwa na kitendo hicho cha mwenyekiti huyo wa kijiji kwa kumshambulia mwalimu wao.

Alisema kuwa miti hiyo ilikuwa kwa ajili ya kupasulia mbao ambazo zingetumika kutengenezea milango ya choo cha shule na kwamba mwalimu huyo hakuwa na nia mbaya kuikata.

Alisema angelipeleka suala hilo kwenye kamati ya shule kama lingekuwa na utata wa ukataji miti hiyo
 
Mbona walimu wanaonewa sana? Yaani kila mtu ni kuwatandika viboko tu. Hiyo profession kweli imeshushwa hadhi katika jamii yetu.
 
auwaye kwa upanga???.............wao wanatandika watoto wetu so arobaini zao zimetimia sasa
Wewe inaelekea ulikimbia shule. Waliosoma wakachapwa hivyo viboko sasa hivi wanawashukuru walimu wao kwa kichapo walichowapa. Mzazi kama wewe ni mmoja wa wale ambao mitoto yao shuleni ni mijinga inapiga walimu haitaki kusoma, ikichapwa, mzazi naye anaungana na mwanaye kuwachapa walimu. Halafu walimu wakiomba serikali iwaongezee kipato serikali nayo inatoa kauli zinazolingana na zile za wazazi wehu na watoto wendawazimu. Mwisho wa yote walimu wanaacha kutimiza wajibu wao ipasavyo na matokeo yake shule zinazalisha kundi kubwa la wavuta bangi, vibaka, majambazi na machangudoa. Mimi nawambieni watanzania tabia yenu ya kuwapiga walimu itaipeleka nchi pabaya. Walimu ndo walioshikilia uhai wa taifa kwa taarifa yenu.
 
Sipati picha siku ambayo tutapata Waziri Mkuu toka mitaa ya Tarime.
 
Huu ni udhalilishaji, kila siku wanacharazwa walimu tu mbona kuna watu wengi tu wanaostahili bakora!
 
Mbona viongozi wetu wengi hawana adabu, hata hawawezi kuthamini utu wa mtu. Hawana ethics kabisa za uongozi.:mad:
 
hiyo ndo tarime bwana na ili kuieka hii nchi kwenye dira tunahitaji watu toka huko kwa akina chacha , mwita, maranya na wambura ili kuongeza tija na uwajibikaji, huyo mwalimu si angeenda kununua mbao kwanini akate miti ya shule hali inayoharibu mazingira, safi sana mzee zephaniah chacha mwenyekiti wa kijiji.
 
mbona Alber Mnali hakufikishwa mahakamani,na nasikia ametangaza nia ya ubunge kupitia ccm,mzee sitta ajiandae pia kama akiwa hampi nafasi ya kuchangia muswada!!!!!!!!!
 
auwaye kwa upanga???.............wao wanatandika watoto wetu so arobaini zao zimetimia sasa

this is not fare jamani. oooh we mutu nahisi wanao watakuja kukutandika viboko siku moja. mtoto anatakiwa achapwe akikosa.na vitabu vya dini vinasema usimnyime mtoto kiboko,utamharibu zaidi,
 
abarikiwe mwalimu wangu alienichapa viboko vinginevyo ningekua nahenyeka sasa, wewe unaesema ni vema walimu kupigwa na kudhalilishwa ninahofu wanao watakushinda. tena nkimkuta yule mwalimu wa darasa la kwanza alienifinya na masikio nampa kifutajasho,manake zile nyimbo za

"hii ndio a, a a a ina mkia mreefuu. a a a.
"hesabu ni nzuri sana wee, mwalimu nifundisheee nipate uelewa.......

mh sitaki kukumbuka zaidi manake napata ushungu jinsi wanavowanyanyasa na kuwadhalilisha.
zamani waalimu waliheshimika sana,siku hizi mmmh ni huzuni tuuu
 
Mbona walimu wanaonewa sana? Yaani kila mtu ni kuwatandika viboko tu. Hiyo profession kweli imeshushwa hadhi katika jamii yetu.



hakuna llolote. kama ni unyonge walimu wenyewe wameendekeza. kwa nini wewe (msomaji) uruhusu mwanaume mwenzako kukupiga? ningekuwa mimi kama noma na iwe noma kinoma.
 
hakuna llolote. kama ni unyonge walimu wenyewe wameendekeza. kwa nini wewe (msomaji) uruhusu mwanaume mwenzako kukupiga? ningekuwa mimi kama noma na iwe noma kinoma.

Kaka sometimes inabidi busara itumike mkuu.
Ila kama akikwambia lala chini akutandike hapo hutomkubalia ila akianza kukushambulia ni bora ukimbilie polisi tu kuliko kupambana.
 
Kufuatwa kwa sheria za nchi ni kitu muhimu sana hasa hasa kwa watawala wenyewe kuwa mfano kwa hilo,
cha ajabu kwetu ni ndoto sana kutokana na hilo basi imekuwa kama sheria vile kila mwenye cheo fulani
kuvunja sheria kwake si hoja mifano ipo mingi tu, muhimu sheria zifuatwe na ziheshimiwe lakini cha kujiuliza
watawala wanaozivunja sheria inatekelezwa kwao?
 
Nyerere angekuwepo, je walimu wangedhalilika hivi?

Swala lisiwe waalimu tu, Tuhakikishe tunapin down vitendo vya wananchi kuchukuliana sheria mkonini wao kwa wao. Hapa tutatatua na Madaktari kuja kupigwa Ngumi pale jamaa anapofariki, Civil engr. kupigwa Risasi na mwenye nyumba pale nyumba inapoweka ufa wiki moja baada ya ujenzi!

Tunahitaji utawala wa sheria udhihirishwe na viongozi na wananchi wauzingatie!!!. Kinachoendelea ni wananchi kusombwa na mmomonyoko wa utawala wa sheria, na kila mtu kuamua na kuhukumu yeye mwenyewe, kwa utashi wake mwenyewe!!.

Tatizo liangaliwe kwa upana!! Kwa sababu huyu bwana hakumtandika huyu mwalimu kwa sababu yeye ni mwalimu, La! bali kwa sababu amekata miti miwili ya shule! Ina maana hata kama ungekuwa ni wewe ukepata bakora kutoka kwa mkuu huyu, ila kama ulipitia judo kidogo hapo mabo yangekuwa magumu kidogo, na kama mke(mume) wako yupo jirani na watoto kidogo wangekusaidia kupigana!!. Hali ingekuwa mbaya pale Mke wa muheshimiwa na mpwae wangewakuta mnampiga huyu bwana in revenge!, nao wangeingilia kati, tena kwa mapanga,bita ni bita bwana!!. tayari machafuko!!.

So lets advocate the rule of law, with our leaders being role models!!
 
Tatizo la mijitu ya mkoa wa mira inatumia minguvu mingi akili kidogo.
Sasa kwa kumcharaza mbarati mkuu wa shule amepata faida gani?
 
Back
Top Bottom