Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
M. M. Mwanakijiji
Kuna ndugu zetu kwenye upinzani pamoja na kumpinga na kumkataa kwao kote Magufuli wanapenda awe kama Rais aliyetoka upinzani! Kwamba, yeye abebe ajenda za upinzani na hivyo aanze kukata tawi alilokalia na kuongeza mafuta ya kujikaanga mwenyewe.
Nimesoma mara kadhaa siku hizi za karibuni za jinsi gani wanataka Rais kuonesha uthubutu wake basi afanye a, b, na c ili wajue kweli amepania! Wanasema "apitishe Katiba ya Warioba", aondoe kinga ya marais waliopita, awakamate viongozi waliopita n.k Yaani, awe kama Rais aliyetoka kwenye upinzani akiwa na ajenda ya total reform ambayo mara nyingi hubebwa na chama cha upinzani.
Sasa huku ni kutokuwa wa kweli katika siasa. Hata sisi tuliomuunga mkono Magufuli hatukumuunga kwa sababu alikuwa amebeba ajenda ya upinzani; Magufuli hakuuza ajenda ya upinzani wala sidhani kama ana maslahi nayo. Sasa hili si la ajabu. yeye ametokana na chama tawala; chama ambacho - kama nitakavyoonesha na nilivyowahi kuonesha huku nyuma - kinahusika moja kwa moja na matatizo yetu mengi ya kiutawala leo hii. Yeye ni zao la chama hicho, yeye ametumikia serikali ya chama hicho, na yupo hapo alipo kwa sababu kubwa ya chama hicho.
Sasa kumdhania kuwa atakuwa ni Rais wa upinzani inashangaza. CHADEMA na wapinzani ambao wana ajenda yao ambayo wangependa waione inatokea ikiwemo Katiba Mpya, uwajibikaji, mabadiliko makubwa ya sheria na mifumo wasimtegemee Magufuli kuwafanyia kazi yao. Huo utakuwa ni uvivu na itakuwa ni sawa na kutafuta njia nyingine ya mkato ya kuingia madarakani!
Yaani, wao wawe wapiga kelele tu miaka nenda rudi, lakini wasishinde uchaguzi. Wasichukue Bunge, serikali za mitaa wala Urais lakini ajenda zao zitekelezwe tu! huu ni uvivu wa kisiasa na tusipoangalia ni unyonyaji wa aina fulani! Yaani, wao wao wawe wanasema tuu, wanasifiwa kwa kusema tu linapokuja la kufanya wajivuruge wenyewe halafu wategemee kiongozi wa CCM abebe ajenda yao, atekeleze ili wao waridhike!
Ombi langu ndugu znagu ni kuwa ili kutekeleza ajenda mbalimbali ikiwemo hata kuondoa kinga za Marais (kitu ambacho hakiwezekani labda kuiwekea mipaka mipya); kuwashtaki viongozi waliopita wakiwemo Marais n.k yanaweza kufanyika na kufanikiwa tu endapo itakuwa ni ajenda ya chama cha upinzani kilichoshinda Bunge!
Sasa, kama nilivyoandika juzi; hakuna njia ya mkato. Mkitaka kupitia mikataba yote, mkitaka kuwafunga wote, mkitaka kufanya yote ambayo wapinzani wanalalamikia njia rahisi na yenye kunyooka kama mstari - ni KUSHINDA UCHAGUZI.
Hakuna kubadili safari angani, hakubadili gia angani, na wala hakuna kubadili chombo cha usafiri! Shindeni uchaguzi vinginevyo endeleeni kuombea kiongozi wa CCM aje kuwaokoa kama mlivyofanya 2015 na mnavyoonekana kuendelea kufanya sasa 2017 na inavyowezekana mtafanya 2020!
Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com