Mkiondoa elimu bure mtaokoa walimu kwenye ugumu wa maisha

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
14,304
29,834
Hii elimu bure imekuwa ngumu sana kwenye utekelezaji huko mashuleni, yani mwalimu utakuta anataka kuwapa wanafunzi weekly test ila shida nikuchangisha. Wazazi hata wakiambiwa wachange miamia tu kwa week nikimbembe. Hapo zamani walimu kidogo walikuwa wanapata vihela vya michango ya wazazi kwa mwanvuli wa kuwalipa walimu wanajitolea kumbe zile pesa walikuwa wanatafuna

Elimu bure imezidisha umasikini mkubwa sana kwa walimu kwani Kuna baadhi ya academic project hazipo kwenye bajeti ya fedha ya elimu bure kwahiyo inamlazimu mwalimu kutoa pesa yake mfukoni ili anunue vitabu, kuprint mitihani na kazi mbalimbali zakiofi. Ushauri wangu serikali futeni elimu bure maana kinachotea mashuleni siku hizi ni aibu maana wanafunzi wanatoka kapa kichwani kwa sababu hawapati elimu bora kama ya mwanzo kabla ya mwendazake
 
.
1658730766811.jpg
 
Back
Top Bottom