Mkimchagua huyu mbunge wangu, nitawaongeza kipande cha kilometa kumi cha barabara

concrete15

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
882
323
Magufuli hivi muda mwingine sijui anatumia nini kufikiria hii ni rushwa kama mpaka tumchague mtu ndo utoe msaada serikali yake itakuwaje baada ya wabunge wake kukosa viti poor thinking capacity now ndo nimegundua kwa nini alirudia kidato cha nne. Siasa za kale sana hizi. Kiukweli leo kaniudhi sana na hiyo pumba alioongea.:mmph:
 
Hajui hata sadam husein alikuwa rais wa wapi, nahsi hata taarifa ya idadi ya samak mbwa na ngombe alikua anaropoka tu..mana huyu kwa minajiri ya kuropoka na kukurupuka kimaamuzi hajambo. Yani sijui anagombea urais ile awe rais wa namna gani sijui. Duh bas bana.
 
Hili nalo la kujadili unaacha kujadili ya lowassa na kauri zake tata kama atawachia wafungwa. Heri hata anaye ahidi kipande cha barabara
 
Hata mimi ninashindwa kabisa kumwelewa Magufuli na hizi ahadi zake za kilometa 10. Kwa mujibu wa kumbu kumbu zangu huu ni mkutano wa tano namsikia akiahidi kilometa 10. Musoma, Geita, Chato, Tanga na Iringa.

Halafu ahadi hizi ukizichunguza sana utaona zimekaa kaa kama ahadi za kirushwa rushwa.
 
Hata mimi ninashindwa kabisa kumwelewa Magufuli na hizi ahadi zake za kilometa 10. Kwa mujibu wa kumbu kumbu zangu huu ni mkutano wa tano namsikia akiahidi kilometa 10. Musoma, Geita, Chato, Tanga na Iringa.

Halafu ahadi hizi ukizichunguza sana utaona zimekaa kaa kama ahadi za kirushwa rushwa.
Bahati mbaya sana Watanzania tumezoeshwa ahadi wakati wa kampeni na tunaona anayetoa ahadi nyingi ndiyo nguli wa siasa. Wagombea ubunge wanaona raha kumwomba mgombea uraisi kilomita kumi za barabara za lami naye anaitikia kwa ahadi na watu wanashangilia na kumwita jembe!
 
Hivi tume huru ya uchaguzi nchini Tanzania inawezekana kweli, kwa maana naona ndio mwarobaini wa matatizo tuliyo nayo.
 
Wanadai sheria ni msumeno, chaajabu Tanzania sheria ni Mundu, aliyetangaza kuzuia watu kufanya mihadhara ya siasa kwake mambo ni Motoo! Kwahili mimi sio Mtanzania nina akili kuliko viongozi wetu wanavyotutawala...sidanganyiki.
 
Back
Top Bottom