Mkimaliza kuwanunua nini kitafuata?

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
2,932
4,534
Labda niwakumbushe tu historia rahisi Sana ambayo mlipaswa kuitafakari kabla ya kujitia ujuha.
1.Hayati Dr Waridi Kabur alikuwa kiongozi mwenye nguvu kubwa mno CHADEMA, mkamshawishi akajitoa CHADEMA na kujiunga CCM Sina kumbukumbu sahihi endapo alirejea nyumbani CCM au ndo alianza rasmi kuwa nanyi.
2.Hamkuishia hapo, Mkamrubuni Zitto mkidhani kuwa CHADEMA ingekufa, bado chama kilibakia imara tu.
3.Hamkukata tamaa bado tu mkamvaa Dr Slaa, mkidhani huo ndo mwisho wa CHADEMA, lakini bado mligonga mwamba.
Sasa hivi mnahangaika na kununua madiwani na wabunge eti wanamuunga mkono Rais kwa nzuri, Kazi nzuri ipi hiyo? Kwani Kama anafanya Kazi nzuri hawawezi kumuunga mkono wakiwa huko huko?
Mnadhani upinzani utakufa kwa roho za chuki na hila mlizonazo?
Upinzani upo ndani ya mioyo ya watu na siyo hao wabunge na madiwani wajinga.
CCM imeshakufa, mnalazimisha kupendwa wakati hampendwi, CCM inapumua kwa nguvu za vyombo vya dola.
Mkimaliza kuwanunua nini kitafuata?kitakachofuata mtaanza kupoteza wananchi wasioipenda CCM, namwona Idd Amin ndani ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom