Mkimaliza Kalenga,njooni Chalinze

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Namshukuru Mungu nimewasili salama hapa Chalinze nikitokea Dodoma. Sasa nipo hapa kata ya Miono utakapofanyika Mkutano wa Ufunguzi wa Watani wetu CHADEMA. Kila mwananchi anamtaja Dr.Slaa,kwani naye atakuja kweli jamani!? Chalinze yazizima.Yawasubiri mje mjionee. Mjionee sera na sura;raha na karaha. Njooni ndugu zangu watanzania.

Kwakuwa si chama changu,sitawawekea kitakachokuwa kikisemwa moja kwa moja.Lakini,nitaleta uchambuzi wangu kama ilivyo ada yangu. Niliulizia kuhusu ufunguzi wetu jana.Kila mtu anailaumu mvua. Siwezi kuwabishia kwakuwa sikuwepo. Nangoja hapa hapa Miono nione yatakayojiri.

Mkimaliza kule Kalenga-Iringa,njooni huku Chalinze-Pwani. Halali mtu hapa kwa siku hizi za kampeni

Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Chalinze)
 
...

...Wasalimie Chalinze !!!


WanaKalenga wanasema Mkoloni hatakiwi Kalenga since our Hero Mkwawa !!!!
 
Ila Chalinze pagumu sana kuiweka chini ya chadema,ila sijui nasubiri tu kitakachojiri
 
Kwa,mtindo huu chalinze pagumu sana
 

Attachments

  • 1394966256574.jpg
    1394966256574.jpg
    51.2 KB · Views: 149
mi natokea mwanza nakuja tu kusikiliza riz1 akipangua hoja zinazomkabili kwa nnavoijua mashine ya cdm haiwez kumuacha hata kidogo akijinadi kwa jukwaa
 
Liz ajipange sana,najua jimbo anachukua ila si kwa urahisi kama ilivyokuwa huko nyuma na kibaya zaidi watu wa chalinze kwa sasa hawatabiriki lolote linaweza tokea

Kila la kheri kwa wagombea wote,matokeo ya kalenga yatatupa picha kamili na kuona upepeo utakapoelekea
 
Back
Top Bottom