MkikiMkiki2015
Member
- Jul 2, 2015
- 20
- 23
View attachment 293617
Asilimia 78 ya wananchi wanasema hali ya rushwa imezidi kuwa mbaya kwa miaka kumi, asilimia 30 wakitaka waliochukua pesa kwa mgongo wa rushwa wazirudishe, asilimia 32 wakisema wafukuzwe kazi na wanyimwe pensheni.
Asilimia 92 ya wananchi wanaamini wagombea wanaotoa pesa kipindi cha uchaguzi ni rushwa na asilimia 55 ya wananchi wanasema rushwa ina athari kubwa kwenye maisha yao.
Kwa mara nyingine tena Mdahalo wa Mkikimkiki unawadia na unaweza kuuliza swali lako kwa vyama vya siasa kwenye mdahalo unaohusu Rushwa.
Tarehe: Jumapili October 4, 2015
Muda: 7:00 – 10:00am (Saa saba mchana hadi saa kumi jioni)
Mahali: Ukumbi wa Julius Nyerere International Conference Centre (JNICC) – Posta
Midahalo hii inalenga kuvipa vyama vyote fursa ya kunadi Ilani zao na kwa wananchi kuuliza maswali muhimu yatakayo pelekea maamuzi yao katika uchaguzi. Vyama vinavyoshiriki ni vile vyenye wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar na wagombea Ubunge angalau majimbo 65.
Midahalo hii itakuwa live hapa jukwaani kwa ushirikiano na JamiiForums na Fikra pevu. Pia Midahalo hii itarushwa moja kwa moja na Star TV na Redio RFA. Vyombo vya habari vinakaribishwa kushiriki lakini lazima wajiandikishe kabla ili kufanya hivyo.
Kupata nafasi ya swali lako kuulizwa kwenye mdahalo, uliza swali lako hapa jukwaani kwenye mada(Thread) hii.
Kama unapenda kuwa mmoja wa watazamaji ukumbini tuma neno KUSHIRIKI acha nafasi tuma jina na kazi yako kwenda 15678.
Utatozwa bei ya kawaida ya ujumbe wa simu (SMS). Hakuna gharama ya ziada.