MkikiMkiki: Mdahalo wa wagombea Urais Oktoba 18, 2015

Jul 2, 2015
20
23
View attachment 300167

Habari wakuu,
Ni mdahalo kwa wagombea Urais kuelekea uchaguzi mkuu 2015. Mdahalo huu unawapa fursa wagombea Urais kuweka wazi ajenda zao kwa nchi yetu ili wananchi wazipime.

Leo Jumapili Oktoba 18, 2015 tunawaletea mdahalo wa Mkikimkiki na leo utajikita kwenye kuwahoji wagombea wa Urais, wawakilishi wa vyama kwa leo ni wagombea Urais kupitia vyama vyao.

Kwa ushirikiano na JamiiForums, mdahalo huu utakuwa live hapa jukwaani. Pia mdahalo huu utarushwa na kituo cha televisheni cha Azam TV, Star TV na Clouds TV pia utasikika kupitia Radio Free Afrika.

Tuwe sote pamoja kujuzana yatakayojadiliwa.

TUWAHOJI TUWAPIME TUWACHUJE
======================




Mdahalo umeshaanza na zinaelezwa sheria za mdahalo pia chanzo cha maswali yatakayoulizwa kwenye mdahalo, mitandao ya kijamii ikitoa maswali zaidi ya mia tano. Wagombea watapewa swali la kwanza na watapewa dakika nne kulijibu kisha taratibu zitaendelea, wagombea watapewa sekunde 90 kwa maswali la muendelezo.

Swali la kufunga kila mgombea atapewa dakika tatu na sasa ni taarifa za wananchi.

Kati ya wagombea watano walioalikwa mdahalo wa MkikiMkiki, wawili wameshindwa kuhudhuria. Mgombea wa CHADEMA alitoa udhuru wa ratiba yake ya kampeni itambana kushindwa kuhudhuria na Magufuli alithibitisha lakini saa sita alitoa udhuru.

Swali(George Makunjo): Kwanini mnaamini mnaweza kutosha nafasi ya Urais

Anna Mgirwa: Suala la kuwa mwanamke halina tatizo kama unaweza kusimamia katiba, mimi ni mwanasheria kwa taaluma lakini pia nimesoma elimu ya theolojia ambayo inaleta watu pamoja ukiongeza na sheria katika haki za binadamu naamini naweza kulisogeza gurudumu letu mbele. Sio kweli kwamba mimi ni mpole sana, mimi ni mpole na si kwamba ni udhaifu, upole ni nguvu. Ni kusema neno linalofaa kwa wakati unaofaa, nimelea watoto wangu na wasio wangu, nimeishi vizuri na jamii, mwenyekiti wa chama cha siasa na sijaona watu wamelalamikia upole wangu, kuna wakati nchi inahitaji kuletwa pamoja.

Chief Yemba: Mimi natosha kwa sababu kwanza naweza kuthubutu na kwa wanaofikiri sina uzoefu, Urais ni taasisi, Urais hauna uzoefu, uzoefu wa utawala na uongozi unapelekea kuwa muadilifu, mimi ni sehemu salama ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Miongoni mwa kazi nilizofanya, sijawahi kufanya kazi isiyo na mafanikio. Nimekuwa mkusanyaji bora wa mapato, nimepandishi timu nne ikiwemo Kagera sugar na karibuni Mwadui FC.

Swali: Swala la Rushwa limekuwa ni tabia, wewe ukiwa Rais utawezeje kukomesha tabia hii.

Anna: Ni kweli rushwa ipo sehemu nyingi lakini zipo sehemu zinazoongoza. Kuna haja ya kuboresha mazingira ya kazi, pili tunahitaji kupambana na huu utamaduni ikiwemo kuingiza upambanaji na rushwa katika mtaala wa shule. Ili tuwe na mazingira bora lazima tuwe na mapato ya kutosha, tumejipanga kuhakikisha tunakusanya mapato kwa kiwango cha 25% ya pato la taifa, kudhibiti ukusanyaji kodi na kuweza kugawa mapato kwa usawa katika sehemu zinazotoa huduma

Swali(Cosmas Raphael): Utawezezaje kuondoa tatizo la rushwa katika ajira, ipi mikakati katika kutatua tatizo hilo?

Chief Yemba: Kuhakikisha tunafanya kazi masaa 24 badala ya masaa manne na tutaongeza watu wengine wawili katika kila kazi na litatibu ikiwemo kuwapa uzoefu wa wanafunzi wanaotoka chuoni.

Anna Mgirwa: Rushwa ni utamaduni nami ni muathirika kwa mwanangu alipomaliza masomo, tunahitaji kuondoa rushwa kama utamaduni ikiwemo kuwafundisha watoto, kutoa na kupokea rushwa ni kosa.

Swali(Isaya Mbeya): Je ahadi hizi zitatekelezwa vipi?

Chief Yemba: Mimi sijatoa ahadi nyingi ambapo kwa wengine nadhani ndio sababu ya kukimbia mdahalo, ahadi za msingi huwa zinaweza kutekelezeka, siwezi kutoa ahadi isiyotekelezeka kwa sababu kuna jicho la tatu linaloniangalia.

Anna Mgirwa: Kutoa ahadi si tatizo bali zitatekelezeka namna gani, tumetengeneza mikakati ambayo wananchi watafahamishwa na pia mikaakti ya utekelezaji.

Swali (Chahali): Nini kifanyike kustawisha uzalendo uliopotea?

Chief Yemba: Uzalendo na kuondoa ufisadi unategemea na yule anayeongoza na mfumo wa kwanza watu washirikishwe na kutafanya watu wawe wazalendo.

Anna Mgirwa: Chama chetu kinaitwa chama cha wazalendo, tumezungumzia maadili ya uongozi na tumerejesha azimio la Arusha kupitia azimio la Tabora.


Chief Yemba: Lengo la kiongozi ni kuwaunganisha watanzania, ninachohitaji lazima turudi kwenye katiba ya jaji Warioba na kuangalia vitu gani vilistahili kuingia viingie, hata ya jaji Warioba ina mapungufu mengi.

Anna Mgirwa:Nilitamka awali, mchakato wa katiba utarejeshwa mpaka pale maoni yalipoishia, nipaona umuhimu wa kurejesha maoni kwa wananchi wayapitie tena. Rasimu ipi, katiba inayopendekezwa bado hairidhishi.

Swali: Viashiria vibaya vya mgawanyiko, ninyi hali hiyo mnaionaje na mtaikomesha vipi ili tuendelee kuwa wamoja?

Chief Yemba: Tatizo kubwa ni kufikiri sana tumbo zaidi ya watu, tatizo hili litaondolewa na mtu anaefikiri watu kwanza na huyo ni mimi. Lazima viongozi hao waondoke wote, wametugawa kwenye tabaka la dini. Nawashauri watanzania waichague ADC, ndio chama pekee kinachotambua uwepo wa Mungu.

Anna Mgirwa: Nafikiri ubaguzi upo kwa viongozi zaidi na sio wananchi, wananchi wanashiriki shughuli zao ikiwemo misiba kwa kushirikiana, mfano sajapata ubaguzi kwa kuwa mwanamke labda watu waondoke wasisikilize. Tuna mbunge ambae ni muislamu lakini anagombea kwenye jimbo

Swali(Akonali JF): Unadhani ni kero zipi zinaandama muungano wetu na ACT inaahidi nini kwa hili jambo?

Anna Mgirwa: Muungano wetu utokane na ridhaa ya wananchi, binafsi sikerwi kwa sababu ndio tulivyo, mwanzo tulikuwa watanganyika. Naona changamoto kubwa ya muungano ni ridhaa.

Chief Yemba: Kero kubwa ni haki sawa kwa watu wote, utapowapa watu haki sawa kwa wote, serikali mbili wala tatu haiwezi kuwa tatizo, tunahitaji kutekeleza haki sawa kwenye elimu, afya, uchumi na mengineyo. LLazima watu watahisi tukiwa peke yetu tutaendelea.

Lakson JF: Mabadiliko yatainua vipi watanzania?

Chief Yemba: Mabadiliko yanahitajika sio kubadilisha watu lakini ni kuondoa ujinga, maradhi na umasikini. Mimi ningependa kuwa na serikali ya kitaifa, kuondoa CCM madarakani na kufanya kazi ya CCM haina tija.

Anna Mgirwa: Sisi tunataka kuleta mbadala wa kushughulikia kero za jamii, mabadiliko tunazungumzia mageuzi.

Swali(JF): Ni kitu gani utafanya kuhakikisha wataalamu wanalipwa stahiki zao kulingana na utaalamu wao na ugumu wa kazi tofauti na wanasiasa?

Chief Yemba: Wataalamu hawapewi mishahara stahiki, kazi ya kutawala inaletwa bungeni lakini sisi tunasema tunaheshimu tafiti na ubunge ni wito.

Anna Mgirwa: Ni kweli wanasiasa wana mapato makubwa kuliko wataalamu na bado tumeendekeza siasa chafu. ACT tutakuza sekta ya uzalishaji na kuhakikisha tunashughulikia maswala ya kitaaluma.

Swali: Sekta ya umma, binafsi na NGO's, sekta ya NGO's inaonekana imewekwa pembeni, Je unatazamaje ushirikiano kati ya sekta zote hizi?

Chief Yemba: Serikali inawatenga wale wanaoweza kuweka huru matatizo, nataka sote kwa pamoja tuwe na ushirikiano, urafiki katika utawala ni tatizo.

Anna Mgirwa: Utendaji wa mashiriki ya kijamii yananyooshea vidole sekta ya umma na wenyewe hawataki kukosolewa. Sisi tutaunda serikali ya umoja wa kitaifa kama njia ya kuboresha mahusiano kati ya haya makundi.

Mgombea wa TLP amefika na kupewa dakika nne za kujieleza

Swali(Kweka):
Sekta ya uchumi na viwanda imepewa kipaumbele, kumuinua mtanzania wa chini

Anna Mgirwa: Hili jambo lina changamoto nyingi ikiwemo umeme wa kuaminika, maji hasa vijijini. Kuzalisha umeme kwa kutumia upepo na miaka ya kwanza tutapitia miundombinu ili tujua viwanda gani tunaweza kufufua na kuanzisha. Hatutachukua maamuzi magumu ya kiuchumi bila kuwashirikisha wananchi, mikataba yote itakuwa wazi.

Chief Yemba: ADC tumesema tutaongeza viwanda kutokana na jiografia ya nchi, tunaamini tukiwa na mifumo mizuri hatutapata shida.

Macmillan Lyimo: Tutakuwa na mfumo mpya, soko ambalo wahusika wanashughulika katika lile soko. Dhahabu tuna 2.2 bilioni tani, ukiwa na hii fedha hakuna kitu kisichowezekana.

Swali (Jingalao JamiiForums): Kujiunga na mifuko ya afya iwe ni lazima au hiyari?

Anna Mgirwa: Tukifanikiwa kuinua uchumi wa nchi yetu, tutachukua jukumu la kugharamia sekta ya afya kwa kuinua pato la serikali ili kuweza kugharamia. Huduma za afya zigharamiwe na serikali kutokana na mifuko yake.

Macmillan Lyimo: Mfumo wetu unaunganisha jamii yote kuwa na maamuzi ya jumla, tutafanya mikoa yote iwe Tanzania, leo tuna taifa ambalo ni Dar es Salaam. Serikali unapaswa uongoze watu, jambo hili linawezekana, kinachotakiwa ni mfumo wenye majibu ya mambo hayo.

Chief Yemba: Serikali ya ADC lazima iwaondolee watu wake maradhi, ukifanya uwekazaji wa uchumi wa viwanda katika jiografia, wakipata pato lao serikali imewekee sehemu ya pato lake katika sekta ya afya.

Swali(Ajua JamiiForums): Kwanini sekta ya serikali zinakosa dawa muhimu kuliko duka za dawa na hili mtashugulikia vipi?

Chief Yemba: Kwanza ni serikali isiyokuwa na hofu ya Mungu inazimisha watumishi wasiwe na hofu ya Mungu, hakuna adabu katika utawala, lazimatuondoe tabaka la wasio nacho na walio nacho, serikali legelege linaruhusu na ADC ni vita yetu kubwa.

Macmillan Lyimo: Ukishatengeneza system ambayo ni corrupt, utacorrupt kila kitu, ni nchi ambayo vipimo peke yake milioni moja. Serikali unaweza kuiweka kwenye kiganja na kumulika.

Swali(JamiiForums): Umejiaandaaje kumaliza deni la taifa sambamba na kuondoa utegemezi kwa wahisani

Chief Yemba: Kwanza lazima wale waliojilimbikizia mali wazirejeshe, ukiongeza huduma unaongeza uzalishaji. Matumizi mabovu ya serikali yataondolewa, posho ni nyingi kuliko mshahara.

Macmillan Lyimo: Niliwahi kuandika kitabu Tanzania ni nchi ya Eden, rasilimali tulizonazo tunaweza kuendesha bajeti za Afrika, Ulaya na Amerika. Utalii tu naweza kukusanya trilioni 100. Mapato katika taifa yanahitaji mtu mwenye knowledge hiyo, baada ya kutoka chuo, nimefanya utafiti kwa miaka 15.

Anna Mgirwa: Matumizi ya serikali yamekuwa makubwa, tumepanga kuzalisha kwa wingi hasa sekta ya kilimo ambayo bado tuna mamlaka nayo. Pia tunahitaji kuangalia thamani ya deni hilo.

Swali(Christian): Mauaji ya albino, wagombea watatumia njia gani kuhakikisha tatizo linaisha, Rais ajaye anaahidi nini kwa walemavu?

Macmillan Lyimo:
Kipengele chetu cha sita ni haki katika taifa, kila mtu atakuwa na mtu hivyo kupata mahala pa kusemea, albino kuuawa wanatokana uchawi, taifa linaongozwa kichawi kichawi, viongozi wanavyokufa wakati wa uchaguzi, hamstuki! Tuwape jimbo kwenye bunge ili wasikiwe, hakuna mtu anaeweza kununua kiungo cha albino kwa milioni 500 kama sio mtu mkubwa.

Anna Mgirwa: Swala la haki za makundi maalum tumelichukulia uzito wa kutosha, utu na uzalendo pia uadilifu kupotea kwake ndiko kunaleta matatizo haya na tumeliweka wazi wakati wote. Tutaimarisha huduma ya usimamizi wa sheria kwa polisi kuhakikisha watuhumiwa wanashikwa.

Chief Yemba: Kwanza linanikera na natoka kanda ya ziwa ambako suala hili ni tatizo kubwa, lazima tutengeze mfumo wa utawala utakaowalinda. Hakuna kiungo cha albino kinachompa mtu utajiri. Wagombea urais wanalindwa kipindi hiki, kwanini tunashindwa kulinda maalbino.

Rungwe amefika ukumbini


Hashim Rungwe: Ndugu wananchi wenzangu, nimeshindwa kufika mapema kwa sababu nilikuwa Mtwara kwa ajiri ya kampeni lakini ndege niliyopangiwa ilipitia Comoro na kujikuta nafika Dar dakika 40 zilizopita na foleni zetu kila mtu anajua

Swali(Kashushu&JamiiForums): Mtahakikishia vipi wananchi kukubali matokeo na kuipa nafasi amani? Tanzania ni moja nchi zenye amani duniani, ukishidwa utashauri vipi na ukishinda utatekeleza vipi?

Anna Mgirwa: Misingi iliyoasisi ndio imetufanya kuwa wamoja na kuwa na amani tuliyonayo, tuweke miundombinu ya amani na ni pamoja na kutoa fursa sawa kwa wote, pia ningependa amani iingizwe kwenye mitaala ya shule kuanzia chekechea mpaka vyuo vikuu.

Chief Yemba: Amani haitawaliwi na matokeo bali inatawaliwa na haki, nikiwa Rais nitahakikisha nailinda amani na nikishindwa matokeo natakubali matokeo. Nani anaestahili kuilinda amani? Haki na matendo, tume isishawishi umma kuvunja amani, si uchaguzi tu, tunaweza kutoka kwenye uchaguzi ukaja uvunjifu mkubwa wa amani. Haki pekee ndio mlinzi wa amani.

Macmillan Lyimo: Dunia haiendi peke yake ndio maana hamna jambo jipya duniani, shida ipo kutoka kwa kiongozi wa nne kwenda wa tano, tunaenda kwenye siasa mpya za dunia. Siasa ya dunia inaenda kugeuka, kama hatutasoma ishara ya nyakati tutaingia katoka machafuka, information is power, tusiache mabadiliko yakatuongoza, amani ikivunjika nani mesababisha? Hakuna uislamu imara pasi na Ukristo imara na kinyume chake.

Hashim Rungwe: Kwanza kuhusu amani, amani ni tunda linalotokana na haki na haki inatokana na mgawanyo sawa wa mali tulizonazo, watanzania wanaweza wakabadilika kutokana na shida inayowakabili. Watanzania wana njaa na njaa haina rika, njaa ni mbaya, tumeona mapinduzi ya ufaransa. Kama watu wana njaa hata ukiwaambia maneno zuri namna gani, hali za wananchi ni mbaya, unataka amani vipi watu hawajala. Daktari na nesi wanaficha mafaili, mahakamani njaa.
 
Last edited by a moderator:
Twambieni ni nani na nani hadi sasa wamethibitisha kushiriki?
 
nawauliza ccm swali
endapo kwa bahati ya mtende wakashinda je watatumia katiba ipi ?
katiba pendekezwa?
katiba ya mwaka77
au watarudi kwenye maoni ya wananchi yaliyopo kwenye rasimu ya warioba?
 
Kwa bahati mbaya mgombea Urais kupitia UKAWA hatoshiriki kutukana na kubanwa na ratiba ya campaign mikoani, mdaharo ungenoga sana!
 
Duh!!! Mimi Ukawa,ila nashauri kwenye Mdahahalo Rais wetu EL awakilishwe na Mbatia au Mbowe. Mweee!!!!
 
Kwa bahati mbaya mgombea Urais kupitia UKAWA hatoshiriki kutukana na kubanwa na ratiba ya campaign mikoani, mdaharo ungenoga sana!

Ratiba ya mdahalo inajulikana muda mrefu. Ni kwamba haoni umuhimu wa mdahalo fullstop.
 
Nasubiri Kwa hamu kusikiliza hoja za mwanasiasa mahiri Edward Lowasa, nahisi Magufuli hatahudhuria kwakuwa anamuogopa sana Lowasa kwa jinsi anavyojua kujenga hoja na kuzidadavua
 
Ninawauliza CHADEMA
Kwanini wameisaliti LIST OF SHAME?

Je Lowassa kasafishwa na nani?

Kwanini MAKAMANDA wameguka na kuwa MIGAMBO?

Ufisadi kama ajenda yao KUU kwanini wameicha inabebwa na CCM?

...ntaendelea..
 
Mtu huyohuyo-muandaa midahalo huyohuyo mtafiti wa uchaguzi-huyohuyo mchambuzi anaitwa kwenye mada-huyohuyo-mpiga kampeni twitter-huyohuyo-mwandishi wa makala kwenye magazeti kuhusu uchaguzi: Nafikiri kuna watu wangetamani wapige kura kwa niaba ya watanzania
 
nawauliza ccm swali
endapo kwa bahati ya mtende wakashinda je watatumia katiba ipi ?
katiba pendekezwa?
katiba ya mwaka77
au watarudi kwenye maoni ya wananchi yaliyopo kwenye rasimu ya warioba?
Mimi swali langu ni kwa lowasa alipoulizwa kuhusu suala LA katiba mpya alijibu nini; na Leo amejiunga ukawa kwa sababu gani?
 
Back
Top Bottom