MkikiMkiki: Mdahalo wa Rushwa na Maadili kwa vyama vya siasa Oktoba 04, 2015

Jul 2, 2015
20
23
Habari wakuu,

Leo Jumapili Oktoba 4, 2015 tunawaletea midahalo ya Mkikimkiki na leo utajikita kwenye Rushwa na Maadili, wawakilishi wa vyama kwa leo ni;

1. Onesmo Kyauke ambae ni mshauri wa ilani UKAWA
2. Mwigulu Nchemba akiwakilisha Chama Cha Mapinduzi
3. Gibson Kachingwe akiwakilisha ACT - Wazalendo
4. Eugine Kabendera akiwakilisha CHAUMA
5. Jacob Samuel akiwakilisha ADC

Kwa ushirikiano na JamiiForums na Fikra Pevu mdahalo huu utakuwa live hapa jukwaani pia mdahalo huu utarushwa na kituo cha televisheni cha Star TV na kusikika Radio Free Afrika. Tuwe sote pamoja kujuzana yatakayojadiliwa.

View attachment 294478
=========

Mdahalo umeshaanza na kinachoendelea kwa sasa ni kueleza tathmini ya rushwa nchini, tulipotokea, tulipo na tunapoelekea.




SWALI: Wahenga wanasema toa boriti kwanza, Je chama chako kimeweka mifumo gani na mtu akipatikana na hatia anachukuliwa hatua gani?

Gabson ACT: Kwa kuzingatia hali ya rushwa, kimeweka miiko ya maadili kwa kuzingatia azimio la Tabora, pasipo miiko ya uongozi tutakuwa tunajidanganya. Kwanza anaondolewa na kushitakiwa na atatakiwa arejeshe mali zilizopatikana kwa njia ya rushwa.

Jacob Samuel ADC: Kwanza inafaa tufahamu rushwa inayozungumziwa ni nini? Corruption ni pana sana, ndani yake kuna bribery na embezzlement. Ndani yake kuna hongo, unatoa pesa kusukuma au kushawishi na embezzlement ni ule ubadhirifu kwa ujumla wake. Makundi haya ya rushwa kila moja inakuja kwa namna yake, kundi la rushwa ndogo kwa wafanyakazi wa kawaida na rushwa kubwa hasa katika mikataba pia rushwa ya kimfumo.

Mwigulu Nchemba CCM: Kwanza rushwa ndani ya chama, sisi kwenye CCM la kwanza ni kukiri kuwa rushwa ni adui ya haki na tumeiweka katika imani ya chama, sitatoa rushwa wala kupokea rushwa wakati wa kuapa. Tuna kamati ya maadili, hatua ndani ya chama huwa zinachukuliwa ambazo chama zina mamlaka nazo kama kumuondolea uongozi na nyingine ni kumnyima sifa atapotaka kugombea nafasi katika dola.

Hatua nyingine, vikao vina fursa ya kuielekeza serikali kuchukua hatua kwa makada wake wenye matatizo ya rushwa kwa sababu ni chama dola. Kamati kuu pia inafanya kazi hio, kwa vyama vya siku nyingi ni CCM imeweza kuishi katika maneno yake.

Kabendera Eugine CHAUMA: Ndani ya chama tumejikita katika sheria kwa maana ya katiba ya chama na elimu. Watanzania mumchague Hashim Rungwe ili tukatekeleze katika serikali, tutanataka mtu alieiba mbali na kuiba, vitu alivyopata kwa mgongo wa rushwa vitaifishwe. Elimu ikiwa juu wananchi wataacha kulaghaiwa na kutoa rushwa, mfano tangazo la TRA la tin namba limewafumbua wafanyabiashara, ndio CHAUMA tutaenda kufanya hivyo.

Vincent UKAWA: Tumepewa tathmini nzuri ya rushwa, kihistoria hata zile himaya kubwa duniani zilikufa kutokana na kuwa na mifumo mibaya ikiwemo rushwa. Katika taifa letu pia watu wengi wanaliongeleo hivyo kuonyesha taifa letu na sisi linaenda kuanguka.

Siku 100 za mwanzo tutahakikisha tunarudisha katiba ya wananchi ambayo ndio unaunda jina letu la UKAWA, kuna sehemu inayozungumzia miiko ya uongozi, hatua ya kati itakuwa ni kuibomoa mifumo ya rushwa na kurudisha nguvu kwa umma. Swala la mwisho ni kuzingatia elimu na tutatoa elimu.

Swali:
Maoni ya wengi Tanzania ni nchi yenye uwazi pasina uwajibikaji, Je tunahamaje kutoka kufichua rushwa hadi kuzuia kabisa rushwa isitendeke?

Jacob: Wengi wazungumzia kutengeneza sheria kali lakini sheria hizo zipo Tanzania, tatizo sio sheria, kwanza ni kuzitambua aina za rushwa na vianzio vyake. Mfano rushwa ya kimfumo inaweza kusababishwa na mishahara midogo na ukosefu wa marupurupu. Tutaboresha mishahara ya watumishi wa serikali.

Mwigulu Nchemba: Baada ya kuziimarisha taasisi na kushighulikia baadhi ya sheria, jambo la msingi baada ya kuimarisha na uwazi ni kuchukua hatua kali na ndani ya muda mfupi ili mtu aogope kuchukua rushwa. Kwenye ilani tumeandika mahakamu maalum ili ichukue muda mfupi, itaondoa uwezekano mtu kuchukua rushwa na kuchukua rushwa nyingine kabla hajamaliza kesi.

Eugine Kabendera: CHAUMA tukichukua madaraka tumejikita katika sheria kwa sababu sheria zetu ziko legelege, kama watu wamechukua rushwa na watu wakaona anafaidi kutokana na kuchukua rushwa watu hawawezi kuacha. Tutatengeneza mazingira sawa kwa wafanyakazi wote, kama chakula kiwe kwa wote ofisini.

Vincent Mashindi: Rushwa katika nchi yetu imeshakuwa ni kansa na lazima kuwe na mkakati kuondoa, jicho la wananchi lazima liachwe wazi kwa vyombo vya habari kuweza kufichua uovu.

Gibson: Lazima kuwe na ukaguzi kwa sababu unasaidia kufichua, ilani yetu tunasema sheria igeuzwa kwa mtuhumiwa yeye ndie athibitishe kwamba hajahusika na rushwa akituhumiwa, msingi wa nne katika ilani yetu ni uadilifu, elimu ya ubaya wa rushwa ni muhimu pia.

Swali: Kuna uwezekano wa kutumia sheria kama ya taifa la China kuondoa tatizo hili Tanzania(Mkosaji kupigwa risasi na gharama ya risasi kulipwa na familia)?

Mwigulu Nchemba:
Kutumia mfumo wa kawaida na kuchukua muda mrefu, na kwa kuwa yupo nje anaweza kumaliza rushwa kwa rushwa, hatua itayofata baada ya kuanzisha chombo maalum, kuchukua maoni ya watanzania na kuona hatua ambayo inaweza ikafata.

Eugine CHAUMA: Sisi kwa asilimia zaidi ya 85 tumelalia kwa wananchi, wengi wanasema ziko chini sana, Dar kuna adhabu kwa bodaboda akienda mjini sh 70,000. Adhabu kwa alieiba jela miaka miwili na akitoka anatanua kwa pesa zetu, hatujafikia katika hatua ya kunyonga lakini tutakupa kifungo ambacho ukitoka hutathubutu tena na wengine hawataiga.

Vincent: Sisi tunajitahidi adhabu ya kifo isiwepo kabisa. Kama rushwa ni ya kimfumo na karibu mfumo mzima unakula rushwa, sisi lazima tufumue.

Gibson: Kifo hapana maana sio njia pekee ya kuondoa hilo tatizo, kiongozi ashitakiwe, ahukumiwe na kisha afilisiwe, adhabu hio ni kali japo sio kifo. Tutatoa elimu.

Jacob Joel:
Kwa mtazamo wangu na chama changu, hata tukijenga magereza nyingi hazitatosha, kuhusu kifo China pamoja na sheria hiyo rushwa bado haijaondoka hata katika 20 bora zenye rushwa kidogo haipo. Namna ya kutekeleza sheria kali zilizotungwa ndio tatizo.

SWALI: Rushwa ya ngono kwa vijana wa kike wakati wa kutafuta Ajira itatatuliwa vipi na chama kitakachoingia madarakani?

Kabendera (CHAUMA):
Adhabu inayotolewa kwa wanaotuhumiwa kwa rushwa ni ndogo, ni sawa na kuambiwa 'Asante' kwa kuiba. Ofisi za umma zinatumika kama vile majumba ya watu binafsi. Adhabu ya anayeiba mabilioni ya shilingi inatakiwa iwe kali. Ukiiba inatakiwa unazirudisha fedha za wananchi..

Dr Mashinji (UKAWA):
Nawapa pole sana mabinti waliokutana na rushwa ya ngono makazini, hii inatokana na ukiritimba maofisini. Kuhakikisha masuala ya ajira yanakuwa ya uwazi kuanzia matangazo yake na usaili kuondoa rushwa ya ngono

Gipson (ACT):
Baada ya viongozi kuingia madarakani & miezi 6 kabla ya kumaliza, lazima wachunguzwe kama hawajajilimbikizia mali. ACTwazalendo: Tunaamini katika Uelimishaji. Tutawachukulia hatua kali sana viongozi wote watakaobainika kuhusika na rushwa za ngono makazini.

Kabendera (CHAUMA): Tunataka tuondoe tatizo la ngono ktk maofisi. Wateja wanakwenda sehemu husika kutaka huduma sio kusaidiwa.

Mwigulu Nchemba: Mgombea pekee anayeweza kusimama mbele ya Watanzania na kusema anachukia rushwa ni Dr. Magufuli tu. Lazima wewe mwenyewe uwe msafi kabla ya kupambana na rushwa...

Vicent (UKAWA):
Lazima tuondoe suala la interiew zinazofanywa kwa siri. Nafasi za kazi ni finyu sana nchini.

Gipson (ACT):
Kiongozi kama huyu akijulikana kujihusisha na suala hili la rushwa ya ngono tunamuondoa mara 1 kwenye nafasi yake

Samweli (ADC);
Suala la rushwa ya ngono kwa ujumla wake ADC ndiyo chama pekee chenye ilani ya aina yake.

Mwigulu (CCM);
Zamani kulikuwa na makosa manne ya rushwa. Sasa yako 24 ikiwemo rushwa ya ngono.

Mwigulu:
Tusiwatanie watanzania, mgombea pekee anayeweza kukemea rushwa kati ya wagombea wengine wote ni Magufuli.

Mwigulu (CCM): Kuna vyama vilikuwa hadi na nyimbo zinazokemea rushwa lakini kwa sasa haipigwi.

SWALI: Rushwa katika Maliasili na Utalii!

Vicent (UKAWA):
Watu ktk eneo husika wachukue nafasi kwa niaba ya watanzania wote (wawe mabalozi). Tupunguze ukiritimba..

Gibson (ACT):
Kupitia uwajibikaji, tunataraji kwamba uadilifu kiwe kigezo kikuu cha kuajiri mtu. Mtu asiyemcha Mungu lazima asiwe mtekelezaji wa vitu vinavyoahidiwa. Tumpe kura Mama A. Mngwira ataleta mabadiliko..

Samweli (ADC):
Tutatokomeza rushwa kwenye sekta ya Utalii kwa kuondoa maslahi duni, kukosekana kwa uwazi & motisha kwa wafanyakazi.

Mwigulu (CCM):
Magufuli ni mchapakazi na hana genge la wapiga dili. Wala rushwa watashughulikiwa. Tumewaletea Magufuli ili aondoe tatizo hili kwani yeye hana genge la wahuni wanaomdai..

Kabendera (UKAWA):
Kule Zimbabwe walimuua Simba lakini hapa kwetu habari za wanyama zinaisha siku 2 tu..

SWALI: Ni lini mara ya mwisho wamesimamia mtu asiye na maadili au mla rushwa?

Gibson (ACT):
Niliwahi kushitaki kampuni ya nje ya nchi Mahakamani & nilishinda.Nina miaka 10 ninasimamia rushwa na maadili.

Samweli (ADC): Huwezi kuzungumzia suala la rushwa bila kuitumia serikali. Binafsi sijawahi kushitakiwa kwa masuala ya rushwa.

Mwigulu (CCM):
Nimewahi kushughulikia suala la rushwa serikalini. Nilisema wasiolipa kodi nitawashukia & wengi walirejesha pesa.

Mwigulu:
Suala la rushwa hata ndani ya chama tunawakemea & kuwaadhibisha watu wanaovunja maadili. Rushwa haitakiwi ndani ya CCM..

Kabendera (CHAUMA); Suala la rushwa lisiishie serikalini bali iende hadi kwa watu binafsi. Maadili yaguse viongozi wote nchini.

Vicent (UKAWA);
Umoja wetu kwa muda umekuwa ukipinga suala la rushwa. Kuna watu wanasema Lowassa anahusishwa na Richmond lakini hawampeleki mahakamani. Mpelekeni mahakamani.

Swali: Je, mkipata ridhaa ya kuongoza watanzania, mtaifunga au mtaboresha nini TAKUKURU? Na pia Tume ya Maadili mtaiboresha vipi?

Mwigulu (CCM); Kwa kuwa taifa ni letu, tumeanza kuipa meno TAKUKURU ili watanzania waridhike na utendaji wake. Awamu ya nne tumeboresha hadi kwenye uchunguzi wa kawaida wanashughulikia kesi za namna hii ili isichukue muda mrefu..

Kabendera (CHAUMA): Tutaongeza elimu kwa watu wetu. Tunataka kuwapa elimu ili wajue mipaka na kikomo katika suala la rushwa.
Tutaainisha masuala ambayo yataonekana kuwa ni rushwa na yale ambayo yatakuwa sio rushwa.
Vicent (UKAWA): Mahakama inatakiwa ipewe mamlaka ya kuchagua hata Majaji wenyewe kuliko kuwaingilia katika maamuzi.
CCM inataka kuwaadhibu watu kwa mawazo yaliyopitwa na wakati. Naomba tupande kwenye boti ya mabadiliko.

Gibson (ACT): Tume ya Taifa ya Maadili na TAKUKURU zimepewe mamlaka makubwa lakini hayatekelezeki..

ACT: Tunataka uteuzi wa viongozi uteuliwe na sheria na sio mtu (sheria ikiunda hali hii itasaidia kuwajibisha kwa sheria).

Samweli (ADC);
TAKUKURU ni chombo cha dola, chombo hiki kinatekeleza sheria ya makosa ya rushwa.
Sisi tumeshasema tutafanya mabadiliko ya kimfumo ili kuonekane nia ya dhati ya kupambana na rushwa kuliko sasa.

Kabendera CHAUMA:
Ktk kutoa elimu wananchi wanapaswa kuelezwa wanapaswa kufanya nini wanaohitaji huduma ktk taasisi za serikali.


SWALI: Je, rushwa ni asili au utamaduni wetu?

Kabendera: Suala la rushwa sio asili ya Tanzania (watu wengi hawajui mipaka ya haki zao).

Vicent (UKAWA):
Mazingira ya rushwa yametengenezwa, hata kama aje malaika kuongoza hii nchi hataiondoa. Ni tatizo la mfumo.. UKAWA tuna ajenda za kukabiliana na tatizo la rushwa ambalo sugu! Katiba ya wananchi waliyoisigina tutairudisha kwa namna ya pekee kutatua tatizo la Rushwa..

Gibson (ACT);
Kuna dhana imejengeka kwa jamii kuwa chama fulani ndicho kinachoruhusiwa kuongoza nchi ambalo si kweli.. Lazima tuwafundishe watu ubaya wa rushwa. Imekatazwa hadi na Muumbaji. Adhabu ya mla rushwa ni kifo kwa mujibu wa msaafu.

ADC:
Kinachoendesha nchin ni mfumo sio mtu. Mfumo ni vyombo vinavyofanyakazi kwa kutegemeana. ADC ndicho chama kinachojua matatizo ya watanzania ili na namna ya kuyatatua. Ninaomba mchague ADC ili kuondoa utamaduni huu.

Mwigulu; Mazingira ya sasa yanaonyesha Magufuli mtu sahihi wa kurekebisha tatizo lolote la mfumo linaloonekana kuwa ni tatizo.. Aina ya mtu asiyeweza kemea uovu hawezi kuongoza nchi. Ndiyo maana tumewaletea Magufuli ili kuondoa giza la rushwa.

#Mkikimkiki iliyokuwa ikiendelea LIVE Star TV na Radio Free Africa pamoja na Live Stream kwa hisani ya JamiiForums imekwisha..
 
Last edited by a moderator:
Hakika kijana wa kazi wa Chama cha Mapinduzi Fieldmarshall Mwigulu Nchemba hii leo anakwenda kupambana na vyama 6 kwenye Mdahalo wa wazi"LIVE" kupitia star tv.
Vyama hivyo ni UKAWA TEAM...ACT ..TLP.
NACHUKUA muda huu kuangalia kwa Makini mdahalo huu unaohusisha msomi wa daraja la kwanza kwenye uchumi hon.Mwigulu
 
Hakika kijana wa kazi wa Chama cha Mapinduzi Fieldmarshall Mwigulu Nchemba hii leo anakwenda kupambana na vyama 6 kwenye Mdahalo wa wazi"LIVE" kupitia star tv.
Vyama hivyo ni UKAWA TEAM...ACT ..TLP.
NACHUKUA muda huu kuangalia kwa Makini mdahalo huu unaohusisha msomi wa daraja la kwanza kwenye uchumi hon.Mwigulu

Tupe muda mkuu lazima tu tune tv zetu hapo. Big up saana Mwigulu.
 
Hakika kijana wa kazi wa Chama cha Mapinduzi Fieldmarshall Mwigulu Nchemba hii leo anakwenda kupambana na vyama 6 kwenye Mdahalo wa wazi"LIVE" kupitia star tv.
Vyama hivyo ni UKAWA TEAM...ACT ..TLP.
NACHUKUA muda huu kuangalia kwa Makini mdahalo huu unaohusisha msomi wa daraja la kwanza kwenye uchumi hon.Mwigulu

Muda gani watakuwa hewani
 
MWAKILISHI WA ACT anaitwa Dickson, yupo wa Alliance for Democratic Change wameulizwa ndani ya vyama vyenu mnashughulikiaje ufisadi .Hapa kichwa cha habari ni rushwa na maadili-muongozaji ni maria tesfai-CCM wamemleta Mwigulu Mchemba-anasema rushwa wao wameikiri na inaapwa kwa imani ya mwana CCM na kuna tume ya chama ya maadili ameva masweta yake
 
Mwigulu: Tunawaondolea sifa ya kuwa wagombea nafasi za uongozi.

Kabendera -CHAUMA-tunatumia katiba na elimu kwa wananchi-anaomba tumchague Hashim Rungwe ashughulikie rushwa
 
Dr Vicent Mashinji-UKAWA: dOLA KAMA oTTOMAN ILIANGUKA RUSHWA NA VIONGOZI KUPENDA ANASA hata Roman empire ilianguka pia -Rushwa ya Tanzania ni ya kimfumo-Hivyo siku 100 za mwanzo tutarudisha katiba ya wananchi ambayo inaunda jina letu UKAWA.HATUA YA PILI NI KUWAPA MAMLAKA WANANCHI YA KUHOJI VIONGOZI HII NDIO NGUVU YA UMA-kISHA ITAFUATA ELIMU ,ELIMU ,ELIMU hii ndio approach yetu
 
Mwigulu: Tunawaondolea sifa ya kuwa wagombea nafasi za uongozi.

Kabendera -CHAUMA-tunatumia katiba na elimu kwa wananchi-anaomba tumchague Hashim Rungwe ashughulikie rushwa

mwigulu anaongea nini, wanawaondolea sifa ya kugombea wakati mifisadi kibao inagombea,
 
Huyu Dr wa UKAWA NI NONDO HAKUNA TENA NAONA ACHUKUE UKATIBU MKUU HARAKA SANA -anajiamini na anajua kuunganisha maswala bila jazba Mwigulu anamcheki sana Vicent Mashinji
 
Kwa sababu Mwigulu Nchemba anawakilisha chama kilichopo madarakani, ni vizuri atoe mifano hai inayodhihirisha kwa vitendo utayari wa ccm katika kupambana na rushwa.
 
Dr Vicent yupo chama gani? Jamaa yupo vizuri sana. Mwigulu na wenzeka kama wamekwisha potezwa
 
ACT-tunasisitiza misingi na tabia ambayo ndio maadili-elimu juu ya ruhwa itatolewa

Anyway jamaa wa twaweza ndio wanamiliki mambo ya uchaguzi

je tunaweza kutumia sheria kama za china kupigwa risasi ama kunyongwa tunaweza kutumia?

MWIGULU-adhabu haitolewi na chama bali taasisi husika-tumeamua kuwa na mahakama maalumu na itakayochukua muda mfupi

amedai watu hawa wanaachiwa wanatumia rushwa kushinda kesi zao hajatoa solution kama watapewa dhamana au la
 
SASA Kama MWIGULU Anasema Wanaachiwa Tu Ktk. Mahakama Hizi Zilizopo, Kwa Vile Watuhumiwa Wanatumia RUSHWA Ktk.Kesi Zao!! HEBU MTUAMBIE Ni Watuhumiwa Wangapi Waliofikishwa Mahakamani Ambao WAMESHINDWA Kuwatia HATIANI!!?? Ninachokiona Ni Mgogoro Na Mhimili Huo Wa Mahakama!! Kusema Hivyo MWIGULU, WANATAKA Tuanini Kuwa WAO, Kama SERIKALI Wamefanya Sehemu Yao, Ila Mahakama Zetu NDIO Tatizo, Kwani Ni Wala RUSHWA!! Hivyo Watuhumiwa Wanatumia Njia Hiyo Kushinda Kesi Zao!!
 
Honegara sana comrade kwa kuwaelimisha watanzania. Huwezi kukmabithi mpiga dili lowasa nchi eti awashughulikie wapiga dili wenzie. Kama aliweza kutaka kumnyamazisha Dr Slaa juu ya sakata la richmond, je akipewa nchi si ndiyo atapiga dili na kuhakikisha kila jambo linakuwa siri.

CHAGUA Dr Magufuli, CHAGUA CCM!
 
Back
Top Bottom