Mkigoma Jumatatu mnafutiwa leseni -Kandoro

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Nauli kupanda baada ya bajeti madereva jeuri kufutiwa leseni Dar
Na Kizitto Noya

SERIKALI imesema itaongeza nauli ya magari ya abiria nchini ikiwamo daladala zinazotoa huduma jijini Dar es Salaam, baada ya Bajeti ya Serikali kutangazwa.

Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), David Mziray alisema hayo jana kwenye mkutano na waandishi wa habari aliouitisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro kuzungumzia tishio la madereva wa daladala kugoma kutoa huduma kuanzia Jumatatu.

Mziray alisema Sumatra imepokea maoni ya Wamiliki wa Mabasi ya Abiria mkoani Dar es Salaam (Darcoboa) ya kutaka nauli ya daladala iongezwe na kwamba inachambua maoni hayo ili kuleta uwiano wa kupanda kwa nauli hiyo na gharama za maisha.

Kwa mujibu wa Mziray, baada ya kukamilisha uchambuzi huo, Sumatra itatangaza nauli mpya baada ya kujiridhisha kuwa haitawapa mzigo wamiliki na wafanyakazi wa magari ya abiria na abiria.

"Maombi ya Darcoboa kutaka kuongeza nauli ya daladala tumeyapokea na tunayafanyia kazi. Tunatarajia kutangaza nauli hizo mpya baada ya kuona mwelekeo wa bajeti ya mwaka 2008/2009," alisema Mziray.

Alitaka wamiliki wa magari ya abiria mkoani Dar es Salaam kuvuta subira na kuipa muda Sumatra kukamilisha kazi yake ya kuongeza nauli kama wanavyodai.

Alibainisha kuwa ingawa mapendekezo ya Darcoboa ni kupandisha nauli hiyo kwa asilimia 15, Sumatra itaiangalia upya na kuipitia kwa makini kabla ya kuidhinisha ianze kutumika.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro amesema serikali, itawafutia leseni madereva wa daladala watakaogoma kutoa huduma siku ya Jumatatu ili kuishinikiza Sumatra kupandisha nauli.

Kandoro alisema katika mkutano huo kuwa hata kama wana sababu za msingi, madereva hao hawapaswi kugoma kutoa huduma, badala yake wanatakiwa kupeleka madai yao Sumatra ili yafanyiwe kazi.

''Mimi nawataka waache kabisa, kwani baada ya taarifa hiyo serikali itachukua hatua kuhakikisha kuwa usalama wa madereva na wote watakaoshiriki mgomo huo, watafutiwa leseni,'' alisema Kandoro.

Kandoro alisema badala ya madereva kugoma, wanatakiwa kusubiri mpaka hapo Sumatra itakapotoa tamko kuhusu kupanda kwa nauli na viwango vyake baada ya kupokea madai yao.

"Kupandisha nauli kuna utaratibu wake ambao tayari umeshafanywa na Dacoboa kwa kupeleka mapendekezo yao SUMATRA hivyo madereva wanatakiwa kusubiri uamuzi wa Sumatra,"alisisitiza Kandoro.

Naye Katibu wa Umoja wa Madereva na Makondakta wa Mabasi ya Abiria Mkoani Dar es Salaam, (Uwamadar) Shukuru Mlawa, alisema umoja huo hauungi mkono mgomo huo.

''Sisi tumesikia tu taarifa hizo za mgomo na uthibitisho wake tumeupata hapa kwa Mkuu wa Mkoa, hivyo hatuhusiki katika maandalizi hayo,'' alisema Mlawa.

Juzi baadhi ya madereva wa daladala jijini Dar es Salaam, walipanga kusitisha huduma za usafiri kuanzia Jumatatu wiki ijayo kwa madai kuwa kiwango cha nauli wanazotoza ni kidogo ikilinganishwa na bei ya mafuta ya petroli na dizeli inayopanda kila siku.

Madereva hao wamekuwa wakisambaza taarifa hizo na kupeana vipeperushi vya kuhamasisha mgomo huo unaolenga kuishinikiza Sumatra kuongeza nauli ya daladala mkoani humo.

Baadhi ya vipeperushi hivyo vinasema: ''Tafadhali dereva utakapopata nakala hii umjulishe na mwenzio kuwa Jumatatu magari (mabasi) yote hayatakuwa barabarani''.
 
Nimetoka kuongea na Mwanahamisi muda mfupi kwenye messenger anasema yapata wiki ya 3 kuna mgomo wa maderva Uholanzi kisa wanataka pay rise .Tanzania madereva wanataka kugoma Jumatatu ijayo wakitaka nauli ipande , Kandoro kasema wakigoma leseni hawana .Mara zote tumekuwa tunaongelea utawala bora , haki za mtu za msingi ikiwepo kugoma kudai haki na kwa amani .Kandoro inakuwaje atangaze kutumia nguvu na kuchukua leseni za madereva ?
 
Acha wapandishe tu maana nchi sasa haina wenyewe. Wanaopandisha bei za mafuta hawatishiwi kuchulia lesseni zao sasa hawa daldala wazungushe gurudumu?
 
Mafuta yamepanda bei TZ jamani hii si lelemama, mimi niko na kupandishwa nauli kabisa!

Kandoro inakuwaje atangaze kutumia nguvu na kuchukua leseni za madereva ?

Huyu mheshimiwa anatangaza kutumia nguvu simply "Because He Can"!
 
Yaani kila kitu mpaka wagome? biashara ya daladala ni biashara uria kwa hiyo wataopenda kugoma wagome na wasiopenda waende barabarani kuzikusanya.
 
kwani sheri ainasemaje? sheria inaruhusu kufutiwa leseni au ndio serikali inataka kuwapa pesa za bure ma lawyers?
 
Miye naona wagome tu na kuparalyze the nation for a few days.. nguvu ya kutawala inatoka na kubakia na watu..! Kwanini serikali ipange bei anyway.. waache soko lishindane.. ndio haya haya mguu mmoja mnataka ubepari, mguu wa pili mnang'ang'ania ujamaa.. lakini tatizo ni kuwa huo ujamaa mnaotaka kwa wengine tu!!
 
Naye Katibu wa Umoja wa Madereva na Makondakta wa Mabasi ya Abiria Mkoani Dar es Salaam, (Uwamadar) Shukuru Mlawa, alisema umoja huo hauungi mkono mgomo huo.

''Sisi tumesikia tu taarifa hizo za mgomo na uthibitisho wake tumeupata hapa kwa Mkuu wa Mkoa, hivyo hatuhusiki katika maandalizi hayo,'' alisema Mlawa.

Kama kusingekuwa na nukuu, ungeweza kudhani Umoja wa Madereva unapinga mgomo. Lakini alichosema ni tofauti na mwandishi wa Mwananchi alivyo tafsiri.

Haya ndio matatizo ya Media Tanzania!
 
Kuhani I believe you can be smart than this .
Huu ndiyo unazi ninao usema hapa .
Hebu jiulize why kulikuwa na huu mkutano ? Nini kilisababisha huu mkutano ? Huyu Katibu kesha wekwa sawa na kutishwa nalabda kulambishwa na kutumika kama kinga ya akina Kandoro anageuka .Nadhani huhitaji PhD kujua kuna mgomo na ndiyomaana walipeleka barua ya kupandisha nauli na Sumatra wamekuja kwenye public domain na kusema msigome tutawasikia .Huyu Katibu wao ndiyo wale wale ambao hulambishwa na kukaa kimya .Si ajabu hana uongozi next term .

Lakini kuwanyima watu leseni kisa wamegoma ni maajabu makubwa , masikini madereva hawajui haki yao inapatikana wapi ndiyo maana watafyata .Hawa hawakuajiriwa na Serikali Kandoro hizi amri vipi ?
 
I think Kandoro is just using vitisho because he knows they work, it is his leadership style and it works in Dar. Time heals and we can wait to see his reaction when there is a strike!! Tanzania ndio inaanza maendeleo... industrial actions are key indicators of transitioning

.
 
mathalani mgomo unakuwepo na kisha kandoro anawanyang'anya
madereva leseni ndo kusema kutakuwa na upungufu wa mabasi na
usafiri utakuwa shida tuu. je huyu mheshimiwa anatarajia kutumia
madereva wa jeshi kusafirisha wananchi kama walivowatumia madaktari
wa jeshi wakati ule muhimbili?

hatua nyingine zawaza chochea wananchi hasa wakati huu ambapo
wananchi hao wameishapigwa na maisha na matumaini ya maisha
bora ndo yanayoyoma kwa kasi. kandoro chunga sana usije leta balaa!
 
Kwa mtazamo wangu kuhusu suala hili napenda kutofautiana kadri inavyowezekana na wengine....! This is a war btn HAVES & HAVE NOTS wewe kama wewe unasimamia upande upi wa mgomo huu....!
hebu kidogo tufanye mahesabu yasiyo rasmi....(bearing in mind fuel price,distance in km)
Take kwamba mr. x ana daladala( hiace) ya mwananyamala posta....... hesabu ambayo mr x anhitaji na kupata kwa siku ni 28,000/=
katika hesabu hiyo posho(malipo) ya dereva na kondakta pamoja na mtaji(mafuta) tayari......! 28,000 x 28 days= 784,000/= per moon
ukiondoa gharama za gari (kupigwa bao nk) say they simply get 700,000/=
TO OTHER SIDE OF THE SHILLING NOW...... MTANZANIA AMBAYE ANATUMIA BASI MOJA KWENDA NA MOJA KURUDI FROM KUTAFUTA KWA NAULI YA 250/= X 28 DAYS ANATUMIA 14,000, AKIWA ANATUMIA MABASI MAWILI 28,000/= .
KODI YA CHUMBA 7,000/= CHAKULA 1,000 X 28DAYS=28,000/= ( ETC)
MTU HUYU ANATUMIA ROUGHLY 70,000/= ( KWA KIWANGO CHA CHINI SANA)
LEO BADO KUNA MTU ANATAKA KUMKAMUA ZAIDI MTU HUYU.....!
MY STAND IS......... TUAMUE KWA BUSARA ZAIDI JAMBO HILI....!
NAWASILISHA
 
Kuhani I believe you can be smart than this .
Huu ndiyo unazi ninao usema hapa .
Hebu jiulize why kulikuwa na huu mkutano ? Nini kilisababisha huu mkutano ? Huyu Katibu kesha wekwa sawa na kutishwa nalabda kulambishwa na kutumika kama kinga ya akina Kandoro anageuka .Nadhani huhitaji PhD kujua kuna mgomo na ndiyomaana walipeleka barua ya kupandisha nauli na Sumatra wamekuja kwenye public domain na kusema msigome tutawasikia .Huyu Katibu wao ndiyo wale wale ambao hulambishwa na kukaa kimya .Si ajabu hana uongozi next term .

Lakini kuwanyima watu leseni kisa wamegoma ni maajabu makubwa , masikini madereva hawajui haki yao inapatikana wapi ndiyo maana watafyata .Hawa hawakuajiriwa na Serikali Kandoro hizi amri vipi ?

Unazi?

Sijui unaongea madudu gani hapo. Nilichosema mimi hakihusiana na unachokisema hapo. Mimi nimekosoa gazeti tu. Kwamba, ukisoma nukuu ya alichosema Mkuua wa Chama cha Madereza utaona ni tofauti na Mwandishi alivyo tafsiri. Mwandishi kasema Mkuu wa Madereva haungi mkono Mgomo. Lakini Mkuu wa Madereva hajasema kwamba anapinga Mgomo, yeye kasema wao hawakuhusika katika haya maandalizi. Ni hicho tu nimesema. Sijaongelea lolote kuhusu ishu zenyewe kwa undani.

Sasa wewe umekurupuka ukadhani mimi nimechukua upande wowote. Sio lazima ujadili kitu kwa kuchukua upande. Ukitafuta huyu jamaa yuko upande gani ndio mwanzo wa kukurupuka!
 
Marekani wana sheria moja inapinga masuala ya "CARTEL", yaani umoja wa watu wanaotoa huduma sawa za kibiashara kuungana ili kudictate na kupanga bei ya bidhaa zao. System hii ya CARTEL inaua ushindani wa haki katika soko huria na matokeo yake wanaonufaika zaidi ni wafanyabiashara hao huku mtumiaji akizidi kuumia. kuna wakati makampuni ya madawa kule Marekani yalikubaliana kufanya CARTEL ili kuuza dawa zao katika bei watakayopanga wao lakini serikali iliposhitukia ikayachukulia hatua.
na sisi Tanzania kama tumeamua kuingia katika soko la ushindani basi ni lazima tuunde sheria hii ya Kudhibiti Cartels kama hizi za watu wenye mabasi ya usafirishaji kukaa chini na kupanga bei ya nauli, ninadhani kama kuna ushindani wa soko na wa haki basi bei za bidhaa zingejiregulate zenyewe na kunufaisha pande zote mbili yaani mfanyabiashara na mtumiaji,
 
CARTEL kama OPEC ndo zinatuumiza kwa kupandisha bei ya mafuta........! ZIFUTWE.....! (FOR THE SAKE OF WALALAHOI)
 
Marekani wana sheria moja inapinga masuala ya "CARTEL", yaani umoja wa watu wanaotoa huduma sawa za kibiashara kuungana ili kudictate na kupanga bei ya bidhaa zao. System hii ya CARTEL inaua ushindani wa haki katika soko huria na matokeo yake wanaonufaika zaidi ni wafanyabiashara hao huku mtumiaji akizidi kuumia. kuna wakati makampuni ya madawa kule Marekani yalikubaliana kufanya CARTEL ili kuuza dawa zao katika bei watakayopanga wao lakini serikali iliposhitukia ikayachukulia hatua.
na sisi Tanzania kama tumeamua kuingia katika soko la ushindani basi ni lazima tuunde sheria hii ya Kudhibiti Cartels kama hizi za watu wenye mabasi ya usafirishaji kukaa chini na kupanga bei ya nauli, ninadhani kama kuna ushindani wa soko na wa haki basi bei za bidhaa zingejiregulate zenyewe na kunufaisha pande zote mbili yaani mfanyabiashara na mtumiaji,

Asante kwa comments zako, nimejifunza kitu.
Serikali kupanga bei na kulazimisha kibabe ...NO! Say NO to that.

.
 
Back
Top Bottom