Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,890
Nauli kupanda baada ya bajeti madereva jeuri kufutiwa leseni Dar
Na Kizitto Noya
SERIKALI imesema itaongeza nauli ya magari ya abiria nchini ikiwamo daladala zinazotoa huduma jijini Dar es Salaam, baada ya Bajeti ya Serikali kutangazwa.
Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), David Mziray alisema hayo jana kwenye mkutano na waandishi wa habari aliouitisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro kuzungumzia tishio la madereva wa daladala kugoma kutoa huduma kuanzia Jumatatu.
Mziray alisema Sumatra imepokea maoni ya Wamiliki wa Mabasi ya Abiria mkoani Dar es Salaam (Darcoboa) ya kutaka nauli ya daladala iongezwe na kwamba inachambua maoni hayo ili kuleta uwiano wa kupanda kwa nauli hiyo na gharama za maisha.
Kwa mujibu wa Mziray, baada ya kukamilisha uchambuzi huo, Sumatra itatangaza nauli mpya baada ya kujiridhisha kuwa haitawapa mzigo wamiliki na wafanyakazi wa magari ya abiria na abiria.
"Maombi ya Darcoboa kutaka kuongeza nauli ya daladala tumeyapokea na tunayafanyia kazi. Tunatarajia kutangaza nauli hizo mpya baada ya kuona mwelekeo wa bajeti ya mwaka 2008/2009," alisema Mziray.
Alitaka wamiliki wa magari ya abiria mkoani Dar es Salaam kuvuta subira na kuipa muda Sumatra kukamilisha kazi yake ya kuongeza nauli kama wanavyodai.
Alibainisha kuwa ingawa mapendekezo ya Darcoboa ni kupandisha nauli hiyo kwa asilimia 15, Sumatra itaiangalia upya na kuipitia kwa makini kabla ya kuidhinisha ianze kutumika.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro amesema serikali, itawafutia leseni madereva wa daladala watakaogoma kutoa huduma siku ya Jumatatu ili kuishinikiza Sumatra kupandisha nauli.
Kandoro alisema katika mkutano huo kuwa hata kama wana sababu za msingi, madereva hao hawapaswi kugoma kutoa huduma, badala yake wanatakiwa kupeleka madai yao Sumatra ili yafanyiwe kazi.
''Mimi nawataka waache kabisa, kwani baada ya taarifa hiyo serikali itachukua hatua kuhakikisha kuwa usalama wa madereva na wote watakaoshiriki mgomo huo, watafutiwa leseni,'' alisema Kandoro.
Kandoro alisema badala ya madereva kugoma, wanatakiwa kusubiri mpaka hapo Sumatra itakapotoa tamko kuhusu kupanda kwa nauli na viwango vyake baada ya kupokea madai yao.
"Kupandisha nauli kuna utaratibu wake ambao tayari umeshafanywa na Dacoboa kwa kupeleka mapendekezo yao SUMATRA hivyo madereva wanatakiwa kusubiri uamuzi wa Sumatra,"alisisitiza Kandoro.
Naye Katibu wa Umoja wa Madereva na Makondakta wa Mabasi ya Abiria Mkoani Dar es Salaam, (Uwamadar) Shukuru Mlawa, alisema umoja huo hauungi mkono mgomo huo.
''Sisi tumesikia tu taarifa hizo za mgomo na uthibitisho wake tumeupata hapa kwa Mkuu wa Mkoa, hivyo hatuhusiki katika maandalizi hayo,'' alisema Mlawa.
Juzi baadhi ya madereva wa daladala jijini Dar es Salaam, walipanga kusitisha huduma za usafiri kuanzia Jumatatu wiki ijayo kwa madai kuwa kiwango cha nauli wanazotoza ni kidogo ikilinganishwa na bei ya mafuta ya petroli na dizeli inayopanda kila siku.
Madereva hao wamekuwa wakisambaza taarifa hizo na kupeana vipeperushi vya kuhamasisha mgomo huo unaolenga kuishinikiza Sumatra kuongeza nauli ya daladala mkoani humo.
Baadhi ya vipeperushi hivyo vinasema: ''Tafadhali dereva utakapopata nakala hii umjulishe na mwenzio kuwa Jumatatu magari (mabasi) yote hayatakuwa barabarani''.