Mkewe Chenge amepitishwa ubunge viti maalum CCM!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkewe Chenge amepitishwa ubunge viti maalum CCM!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ntemi Kazwile, Sep 14, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hata baada ya tuhuma lukuki za rushwa na ubadhilifu, familia ya mwanasiasa wa kinyantuzu, Andrew Chenge, imezidi kujiimalisha kisiasa baada ya mkewe kupitishwa na chama chake kuwania ubunge viti maalum mkoa mpya wa Simiyu.
  Na taarifa za kuaminika ni kwamba Chenge atashinda kwa kura nyingi sana kwani wananchi wa huko bariadi, wanyantuzu, wanachojali ni pesa, hata kama zitatolewa na majini ya Sheikh Yahya wao hawana noma. Hapa kama kuna mwenye matumaini ya kupambana na ufisadi inabidi ajiulize upya na ikiwezekana kubadilisha mbinu kuwahamasisha waondokane na wendawazimu wa aina hii
  Na kuna taarifa pia kuwa kuna wachina wamepelekwa kule na mwenyekiti wa chama Twawala ndugu Jakaya kwenda kuwaghiribu wapiga kura kuwa barabara ile inawekewa lami, wakati hakuna bajeti ya kitu kama hicho mwaka huu.
   
 2. Oluoch

  Oluoch Senior Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama kinachokosa mwelekeo na shabaha madhubuti ya kupambana na UFISADI,huzilinda,huzitetea na kuzikumbatia familia za maaskari walio mstari wa mbele kuimairisha ufisadi kama Chenge na mkewe.
  Suluhisho ni wananchi kuwapiga stop kwa kumchagua DR. SLAA kuwa rais ili apambane nao vyema kwani CCM wanalindana!
   
 3. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  CCM wamempitisha mke baada ya kuona kuwa mumewe hatoingia tena bungeni msimu huu kwa sababu anayo kesi ya kujibu.Kazi kwelikweli wata tapatapa hadi mwisho lakini wasome alama za nyakti kuwa Wananchi aka WATANZANIA wameichoka ccm
   
 4. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu ninasikitika kukujuvya kuwa kuna watu huku Tanzania wanajua kuwa tanzania = ccm = tanzania, kule usukumani nadhani ndiko tatizo kubwa kuliko yote. Kama ni malazi basi ni kasa au ukimwi uliokolea
   
 5. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  what? are you serious guys? oh nooooo!
   
 6. minda

  minda JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  sasa rafiki yangu post hii haijashiba vizuri;
  je, huyo candidate alipitishwa lini na anaitwa nani? au ndiye huyo aitwaye Tinner Andrew chenge?
  elimu ya uraia inahitajika sana nchi hii kwani sehemu kubwa wa watanzania bado hawaelewi misingi ya demokrasia na nini cha kufanya na hii imekuwa mtaji mkubwa kwa baadhi ya vyama hapa tanzania.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  This is politicl rape of voters' mentals!
  Lakini hawa watu wa Simiyu waashindwa nini kula hela za huyo vijisenti, na kumpa kura mgombea wa upinzani?...Mikoa mingine ina ukabilaukabila usio hata na sababu!
   
 8. D

  Dick JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Au ndiyo waliyosema wahenga kuwa mkono wenye kiltu hulambwa?
   
 9. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kwani mke wake naye ni fisadi?!
   
 10. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,802
  Likes Received: 2,748
  Trophy Points: 280
  Hata baada ya tuhuma lukuki za rushwa na ubadhilifu, familia ya mwanasiasa wa kinyantuzu, Andrew Chenge, imezidi kujiimalisha kisiasa baada ya mkewe kupitishwa na chama chake kuwania ubunge viti maalum mkoa mpya wa Simiyu.

  Kama Chenge hagombei tena, hii ni habari njema! Kama mke wake anachaguliwa kuziba pengo lake, ni uthibitisho uwezo wa JK kufikiri ni mdogo kuliko tulivyofikiria. Hakuna shida: Piga chini JK, mpigie Dr Slaa
   
 11. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Yaani kama nchi ya kifalme vile.
  Viongozi wanapokezana tu 'neema'
   
 12. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  huyu jamaa si hakimu alisema ana kesi ya kujibu, sasa kwa nini asisimamishwe kugombea ubunge, maana sheria inasema anayeshitakiwa na aliyewahi kushitakiwa haruhusiwi, sasa yeye kaua watu jamani
   
 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mpaka mbwa wake ni fisadi!
   
 14. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama hatutofanya maamuzi sahihi Oktoba 31 itafika wakati hata watumishi wao wa ndani watapitishwa kugombea udiwani na ubunge kwa mgongo wao.
   
 15. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  lazima mlalamike hela inafuata hela mwenzake ,usitegemee wewe kanyaboya mkeo atachaguliwa kuwa mbunge no,value to value ''quid pro quo""ila slaa anatisha tuache utani;;;du natamani ashinde
   
 16. Homo Habilis

  Homo Habilis Senior Member

  #16
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 189
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  VOTE FOR Dr Slaa.
   
 17. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,719
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Whaaat?????? jamani jamani jamani tunatafutana ubaya sasa nini hii???
  Wewe unayeitwa mke wa Chenge mwogopeni mungu huu ufisadi utawaisha lini?
  Mwanamke unakosa haya hivi ni lini mtaelewa watanzania wamewachoka mpaka tufanye kwa matendo maana maneno ya ustaarabu kwenu hayana tija...sasa tusilaumiane mbele ya safari. Mlaaniwe kwa jina la Tanzania na watu wake.Laana iwafikie ninyi akina Chenge na vizazi vyenu vyote vijazo..
   
 18. E

  Estmeed Reader Senior Member

  #18
  Sep 14, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  La wabunge huru:

  Kulikuwa na na sheria ya kutaka kuwepo na wabunge huru...wengine wanawaita "binafsi", yaani wasiotegemea baraka za chama cha siasa.!

  Wengine wapo wenye kufikiria kuwa kukataliwa kwa sheria hiyo ni kufinya maendeleo ya demokrasia nchini.

  Kuna wengine wenye kufikiria kuwa kwa kukataliwa kwa sheria hiyo ni njia mojawapo ya kudhibiti mafisadi, ambao kule watokapo wananchi wanawaona kuwa ni wakombozi wao: Chenge na Mramba ni mifano mizuri. Wanaweza kupigiwa na kushinda kura, endapo wangesimama kama wagombea binafsi!
   
 19. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nafasi ya shetani haiendi kwa malaika asilani.
  Ila malaika humshinda shetani baada ya kumpa kisago cha wakati
  Mungu anaona
   
 20. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #20
  Sep 15, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Hivi Hosea atamkamata lini Chenge kwenye kesi ya rada? Badala ya kumshughulikia Chenge wao wanagombea zile pesa zilizozidishwa wapewe serikali! Na BAE hawataki kwani wanajua zitamrudia Chenge na kundi lake tena, yaani itakuwa double commission! Kwa nini JK asitumie utaratibu wa EPA wa kumuomba mwizi arudishe alichoiba yaani Idrissa na Andy warudishe ile mifedha iliyoko visiwa vya Jersey?
   
Loading...