Mkesha wa kusherehekea mawasiliano na majigambo ya wanasiasa wetu

Possibles

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
1,776
1,857
Taarifa ya Habari ya TBC 1 Imeripoti wanakijiji wa vijiji vinne vya kata ya Kitere wakikesha kusherehekea kupata mawasiliano ya simu. Laiti wanajamvi mngepata nafasi ya kuona hali ya watu wale na sherehe yao UCHUNGU ungewapata mnapohusianisha na majigambo ya baadhi ya wanasiasa tulionao kuwa nchi imepiga hatua kubwa ya maendeleo.Hivi wanasiasa wetu wanayapimaje maendeleo!!?Au ndo kama 'mheshimiwa' mmoja aliyesema kuongezeka kwa foleni ni kiashirio cha maendeleo kwa kuwa watu wananunua sana magari!?
Seriously; MUNGU atujalie viongozi wanaojua kueleza ukweli wa hali za wananchi majukwaani badala ya kujitapa.IT PAINS JAMANI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom