Mkeo au mume kwenda dinner na rafiki yake jinsia tofauti

entry

JF-Expert Member
Apr 11, 2018
248
464
Wakuu wazima, hivi unachukuliaje hili swala la mme au mke anamuaga mwenzie naenda dinner na rafiki yangu isitoshe ni jinsia tofauti. Nimeuliza baazi ya wanawake majibu yapo hivi.

1. Ke wa kwanza.
" Ni vizuri kwenda tu hii itamfanya imuume siku nyingine atanipeleka na yeye"
2. Ke wa pili
" Sio mbaya kutoka na rafiki yako"

Na majibu ya wanaume baazi
1. Me wa kwanza
" Utuzungu utawacost"

Je, wewe kwa mtazamo wako unalichukuliaje hili swala?

Karibuni
 
Note, a person (jinsia tofauti) ambaye anajifanya yupo karibu na mwenza wako ndio huyo huyo atakuja kukuchapia siku mkiwa na misunderstanding kwenye uhusiano wenu, huwa inaanzaga hivi hivi.


Let's meet at the top, cheers 🍻
 
Inawezekana tu, ikiwa huyo rafiki yake atakuja na partner wake. Na Mara nyingi ukitaka kujua kama hii iko vizuri, na wewe uende na rafiki ya mkeo aje na partner wake, halafu wewe uwe na partner wa rafiki wa mke wako na mke wako aendelee dinner na rafiki yake. Just have this proposal at the table halafu uone response yake.
 
Wengi wanakuja kugundua kuwa wanakosea baada ya mwenza wake kuchukua maamuzi tofauti na alivyokuwa akifikiria ila ni hatari sana hawa wanaojifanyaga ni marafiki tu
 
Back
Top Bottom